Msanii nyota wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini,Khadija Shaban maarufu kama ‘Keisha’ amejifungua mtoto wa kiume siku ya Jumatatu (Mei 5) katika hospitali ya Mount Mkombozi Kinondoni.
Keisha amesema anashukuru Mungu amejifungua salama na mtoto anaendelea vizuri…..“Nimejifungua mtoto mwingine wa kiume katika hospitali ya Mount Mkombozi Kinondoni.
Namshukuru Mungu nimejifungua salama na mtoto anaendelea vizuri,” amesema.
Keisha anawatoto wawili…..Wakwanza ni wa kiume alijifungua kwa njia ya upasuaji na kumpa jina la Jam Key Machi 2011,