CHUMA BLOG
Chumba cha kulala wageni.
Ukumbi mdogo.
Chumba maalum cha mazoezi.
Chumba cha kulala Angelina Jolie.
Chumba cha kupumzika wageni.
Pembezoni mwa bwawa la kuogelea.![jolie-6]()
Sehemu ya chakula.![jolie-8]()
sebule.
Bwawa la kuogelea. ![jolie-13]()
Mwonekano wa nje wa nyumba hiyo.













NEW YORK MAREKANI: Gumzo kubwa ulimwenguni kwasasa kwenye masuala ya burudani ni kuachana kwa wanandoa maarufu Angelina Jolie na Brad Pitt.
Baada ya wawili hao kutalakiana, Angelina Jolie sasa anahamia kwenye mjengo uliopo pembezoni kabisa mwa Malibu huku akiondoka na watoto wake wote, ambao jumla yao wako sita.
Kwenye nyumba hiyo ya kifahari, Angelina atakuwa akilipa kodi $95,000 kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni 209 kwa mwezi).
Inadaiwa kuwa muigizaji huyo alipanga kwenye nyumba hiyo yenye thamani ya $12m, wiki tatu kabla ya kudai talaka toka kwa Pitt.
Ina ukubwa futi za mraba, 4,409, ikiwa na vyumba vitano na mabafu matano na itatumiwa na yeye na watoto wao, Maddox, 15, Pax, 12, Zahara, 11, Shiloh, 10, mapacha Vivienne na Knox, 8.
Jolie na Pitt walianzisha uhusiano mwaka 2004 wakati wakishoot filamu ya Mr. & Mrs. Smith, wakati huo Brad alikuwa amemuoa Jennifer Aniston kabla ya kuachana naye na kumuoa Jolie.