CHUMA BLOG
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group, Said Salim Bakhresa, alipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa huko Fumba wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi leo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu, Ayoub Mohamed Mahmoud.
Shein (wa pili kushoto) akiwa na Said Salim Bakhresa (kushoto) na viongozi wa Serikali wakati alipotembelea mradi huo.
Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Said Salim Bakhresa(kulia) wakati alipotembelea mtambo wa kutengenezea lami katika Kampuni ya Azam Group leo.
…Akipanda ngazi ya moja ya nyumba zinazojengwa.
…Akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa mashine za kutengenezea lami wa Kampuni ya Ujenzi ya Azam Group, N.P.Singh (wa pili kulia).




