CHUMA BLOG
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Na Dustan ,Morogoro.
Baadhi ya majirani wanaoishi jirani na Makabuli hayo baada ya kushuhudia makabuli hayo yakiteketea kwa Moto
Wakizungumza baadhi ya wananchi hao walisema.
" Hii sio sawa moto umeunguza mpaka alama'kumbukumbu' za maji ya marehemu sasa ndugu wa marehemu watakapo amua kuja kudhuru kwenye makaburi ya wapendwa wao watawatambuaje ili hali alama za majina ya wapendwa wao zimeunguzwa na moto"Alisema mmoja wamashuhuda hao Juma Athuman
Baadhi ya wananchi walipoulizwa kama wanajua sababu za wahusika kuchoma makaburi hayo walisema.
" Tunahisi moto huo umechomwa na mwendawazimu ambaye hupenda kukaa kwenye makabuli hayo huku akivuta sigara hivyo kutokana na ukavu wa majani baada ya kutupa kichungi cha siraha kilizaa moto huu "alisema mmoja wawananchi wa eneo hilo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
lkumbukwe siku za nyuma Uongozi wa Kanisa Katoriki Jimbo la Morogoro kupitia Jumuiya zake za mitaa 'Vigango' walijiwekea zamu za kusafisa makaburi hayo Wakristo na Waislam kila mwezi, ambapo kwa sasa jambo hilo halipo tena jambo lililosababisha makabuli hayo kuzingirwa na msitu mkubwa.