Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all 2614 articles
Browse latest View live

RUGE Awachana Basata...Adai Wamekuwa Kama Polisi Badala ya Kuendeleza Sanaa Tanzania

$
0
0
CHUMA BLOG

Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amesema Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA linapaswa kubadili mfumo wa ufanyaji kazi kwakuwa kwa sasa linafanya kazi kama polisi kuliko kuuendeleza muziki wa Tanzania.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL Ijumaa hii, Ruge alisema baraza hilo limekuwa likionekana zaidi katika kuwaadhibu au kuwafungia wasanii kuliko kusaidia kukua kwa muziki ikiwemo kutoa milango zaidi kwa watu wanaotaka kuanzisha tuzo.

“Mlolongo wa tuzo unakuwa ni mgumu wakati ni jambo ambalo linatakiwa kupewa msukumo mkubwa sana. Baraza la sanaa, na vyombo vingine vimekuwa vikifanya zaidi ya upolisi kuliko kusukuma,” alisema.

Amedai kuwa kutokana na BASATA kupenda kufungia video au nyimbo, wasanii wamekuwa wakifanya makusudi kwakuwa kazi zao hupata kiki na video zao Youtube kupata views zaidi zinazowapa fedha kuliko kazi kuchezwa kwenye TV.

Anaamini kuwa baraza hilo linapaswa kuwa mbele kiteknolojia na kimawazo kuliko hata wasanii wenyewe na kuweza kwenda na mabadiliko ya muziki duniani.

Ruge amedai kuwa hata muziki wa dansi umeporomoka kwasababu hakuna chombo cha muziki ambacho kinawasaidia.

Sakata la Moto Mkubwa Israel..Washukiwa 12 wakamatwa

$
0
0
CHUMA BLOG
Maafisa wa polisi nchini Israel wamewakamata watu 12 kwa tuhuma za uchomaji wa makusudi kufuatia msururu wa moto ambao umekuwa ukilichoma taifa hilo kwa siku nne sasa.
Zima moto wameudhibiti moto huo katika mji wa kaskazini wa Haifa ambapo takriban watu 80,000 walilazimishwa kuondoka.

Lakini maafisa wanasema moto midogo midogo bado inaendelea kukabiliwa katika maeneo tofauti.
Netanyahu: Moto mkubwa Israel umesababishwa makusudi
Moto huo umesababishwa na hali ya kiangazi pamoja na upepo mkali.
Watu kadhaa wametibiwa kwa kuvuta moshi lakini hakuna majeraha yalioripotiwa.
Ndege zinazosaidia katika harakati ya kuuzima moto mkubwa unaonedelea kulichoma taifa la Israel

Ndege zinazosaidia katika harakati ya kuuzima moto mkubwa unaonedelea kulichoma taifa la Israel
Waziri mkuu wa Israel awali alisema kuwa iwapo moto huo ulianzishwa kwa makusudi basi washukiwa watakabiliwa na mashtaka ya ugaidi

Waziri wa elimu Naftali Bennet ,kiongozi wa chama cha Jewish Home Party ,aliashiria kwamba huenda kuna mkono wa Waarabu ama Wapalestina kupitia ujumbe wake wa Twitter uliosoma: Ni wale wasiotoka katika taifa hili ambao wanaweza kulichoma pekee.

Vuguvugu la rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Fatah limesema kuwa maafisa wa Israel wanatumia moto huo kuwalaumu Wapalestina.

RC Makonda Awataka Watendaji wa Kata Kuwa na Taarifa Zote za Miradi ya Maendeleo

$
0
0
CHUMA BLOG
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Kata ya Msigani mtaa wa Temboni juu ya watendaji wote wa Kata kuwa na taarifa zote za miradi ya maendeleo vinginevyo atawachukulia hatua stahiki leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimsikila Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole  alipokuwa akitolea ufafanuzi kuhusu mradi wa maji huo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikangua mradi wa maji ambao ulikuwa ukiratibiwa na kamati ya maji ya Mtaa ambapo ulionesha mapungufu na kwasasa mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASCO
Mkazi wa Mtaa wa Temboni, Moroen Goube akifafanua jambo katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambapo leo ni siku ya nane tangu aanze ziara hiyo, akiwa katika ziara yake ndani ya Wilaya ya Ubungo Kata ya Msigani mtaa wa Temboni RC Makonda ametoa agizo kwa Watendaji Kata wote katika Mkoa wake.
RC Makonda amewataka watendaji wote wa Kata kuwa na taarifa zote za miradi ya maendeleo vinginevyo atawachukulia hatua stahiki.
“Sitaki Kumkuta Mtendaji yeyote wa Kata ambaye hajui jambo lolote kwenye kata yake” Alisema RC Makonda.
Pia RC Makonda amemuagiza RPC Mkoa wa kipolisi Kinondoni Suzan Kaganda kwa kushirikiana na TAKUKURU kumshikilia na kumfanyia uchunguzi aliyekuwa Mtendaji wa Kata hiyo Neema Kalumbe ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa Kata ya Makongo kujibu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa Barabara ya kutokea Msuguri na Msingwa ambao ulitengewa milioni 17 na hakuna barabara iliyojengwa.
Wananchi wa Mtaa wa Temboni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka mwenyekiti wa wa Mtaa huo wa Msigani Israel Mushi kutofanya kazi kwa upendeleo kwani kuna Mkazi aliyefahamika kwa jina la Maureen Gomba ambaye amelalamikia kuwa mwenyekiti huyo amekuwa akigawa vizimba kwa watu anaowafahamu.
RC Makonda amewatoa hofu wakazi hao kuhusu huduma ya maji na kwani kwasasa mradi huo upo chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASCO, huku Mkuu wa Wilaya hiyo akihaidi kukutana na wananchi hao ili kumaliza kero hiyo kabisa ifikapo Desemba 21.

MZEE wa Upako Aachiwa na Polisi...Agoma Kusema Kulichotokea Mpaka Kuwekwa Ndani

$
0
0
CHUMA BLOG
 

Anthony Lusekelo 
Siku chache zilizopita Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako wa Kanisa la Maombezi lililopo Ubungo, jijini Dar es Salaam alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanyia fujo jirani yake huku akimtolea maneno yasiyo sahihi.

Inadaiwa kuwa,Mchungaji Lusekelo alifikia atua hiyo baaada ya kukerwa na tabia ya jirani yake huyo kutangaza kuwa yeye ni mlevi na hivyo hapaswi kuwa mchungaji.

Tangu aachiwe na Polisi, jana alifika kanisani kwake katika ibada ya Ijumaa kama ilivyo kawaida ambapo wengi walitegemea kuwa angewaeleza waumini wake kuwa ni kitu gani hasa kilitokea hadi akakamatwa na Polisi.

Tofauti na matarajio ya wengi, Mchungaji Lusekelo alisema hatozungumzia suala hilo na akasema kuwa ambao tayari wameanza kulizungumziawao wanendelee sababu inaonekana kama wao ndio wanajua ukweli sana.

“Kuna kitu nilikuwa nataka nikiseme, lakini sitakisema ili waendelee kusema hao hao waliokuwa wanasema. Sisemi chochote, hao waliosema wakawaulize wenyewe” alinukuliwa Mzee wa Upako akitoa maneno hayo wakati wa ibada.

Wakati akinendele na mahubiri yake kanisani hapo, alisema kuwa kuna watu walitamani asiwepo tena. Najua wapo na watashindana lakini hawatashinda na nina amini Mungu atawalipa sawa sawa na matendo yao.

Jamhuri yaweka pingamizi tena leo kwenye Rufaa ya Godbless Lema

$
0
0
CHUMA BLOG
lemaARUSHA: Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, leo, anatarajia kujua hatima ya dhamana ya kesi ya uchochezi inayomkabili.
Lema anashikiliwa katika mahabusu ya Magereza ya Kisongo mjini Arusha.
Wakili wake, Peter Kibatala amesema walikata rufaa chini ya hati ya dharura kuomba Mahakama isikilize kesi hiyo mapema.
Amesema waliamua kufuata maelekezo ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Mosha ya kuwataka kukata rufaa.
Katibu wa mbunge huyo, Innocent Kisanyage amesema rufaa hiyo itasikilizwa leo saa tatu asubuhi baada ya kukamilisha mambo yanayotakiwa.
Lema alirudishwa mahabusu kutokana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kukataa kupokea ombi lake la kufanya marejeo ya uamuzi wa kunyimwa dhamana.
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mosha alisema uamuzi uliofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi umeegemea kifungu cha Sheria cha Makosa ya Jinai CPA 148, hivyo kilimtaka mshtakiwa kukata rufaa siyo kuomba Mahakama hiyo kufanye rejea,
Rufaa hiyo itasikilizwa na Jaji Fatuma Massengi, huku Lema akitimiza siku ya 26 tangu apelekwe Gereza la Kisongo.

Lady Jaydee Aijibu Kauli ya Ruge kuhusu Clouds FM Kuwa yupotiali Kuchezwa Nyimbo zake

$
0
0
CHUMA BLOG
Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alidai kuwa vituo vyake vinaweza kuanza kucheza kazi za Lady Jaydee iwapo akiwaruhusu wafanye hivyo.

Kupitia Instagram, Lady Jaydee ameijibu ofa hiyo kwa dongo lililowaendea wasanii waliowahi kumshirikisha kwenye nyimbo zao lakini kwa kuogopa kuingia matatani na kituo hicho chenye nguvu nchini, walifuta sauti yake.

“Kwahiyo wale mlio omba collabo sijui feat baadae mkaenda kufuta chorus zangu mtafanyaje ??. Habariiiiiiiiiii zenu buaaaaaana 🏃‍♀️ #SawaNaWao #TofautiNaHesabuZao,” aliandika Jide.

Ruge alitoa kauli hiyo Ijumaa iliyopita kwenye mahojiano na kipindi cha XXL.

“Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.



Ruge pia alisema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’

Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Lady Jaydee na muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.

“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita hayo.”

Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee, NavyKenzo wametajwa kwenye Tuzo za SoundCityMVP2016

$
0
0
CHUMA BLOG
Mastaa ambao wako A-List kwenye muziki wa BongoFlava kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, NavyKenzo, Vanessa Mde na Alikiba wametajwa kwenye list ya wasanii wanaowania tuzo za SoundCityMVP zinazoandaliwa na kutolewa na kituo cha TV kutoka nchini Nigeria cha Sound City TV.
Tayari majina na category zote za wasanii watakawania tuzo hizo yametangazwa na kituo hicho huku zikiwa na ushindani mkubwa kwa namna vipengele vilivopangwa. Diamond Platnumz anawania tuzo mbili ikiwemo Msanii Best African Of The Year pia atachuana na mastaa wengine kwenye tuzo ya “Best Male” ambao ni rapa Emtee kutoka South Africa, Wizkid (Nigeria), Patoranking (Nigeria), Falz (Nigeria), Olamide (Nigeria) na Phyno (Nigeria).
Alikiba anawania tuzo ya Video Bora akicompete na mastaa wengine kama Mr. Eazi – SkinTight, Patoranking – No Kissing, Eddy Kenzo – Mbilo Mbilo, Emtee – Roll Up, DJ Maphorisa – Soweto Baby, Phyno – Fada Fada, Olamide – Who You Epp, Harry Song – Raggae Blues na Mastecraft – Finally. 
Wizkid ndiye ameongozwa kuwania tuzo nyingi zaidi zikiwa ni category 8 zikiwemo nne za number 1 hit single ya ‘Baba Nla’ inayowania tuzo ya Best Song, Best Video, Viewers’ Choice na Listeners’ Choice akifuatiwa na rapa kutoka South Africa, Emtee na Olamide. Soundcity MVP2016 zitatolewa na kuoneshwa Live Alhamisi, 29 December kutoka ndani ya ukumbi wa Expo Center of the Eko Hotel & Suites, Jijini Lagos Nigeria.
scity2
Baada ya kitambo cha kutotajwa kwenye tuzo yoyote hatimaye mwimbaji Davido ametajwa kwenye kipengele cha Digital Artiste of the Year akiwa na Tekno, A.K.A, P-Square, Tiwa Savage, Wizkid na Casper Nyovest. Warembo kutoka East Africa Victoria Kimani (Kenya), na Vanessa Mdee (Tanzania) watachuana kwenye category ya Female MVP of The Year wakiwa na msanii kutoka Ghana, MzVee. 
Wakati huo huo Navyo Kenzo wanawania tuzo ya Best Grouo or Duo wakiwa na Sauti Sol (Kenya), Mafikizolo (South Africa), Micasa (South Africa), R2Bees (Ghana), Toofan (Togo), P-Square – Nigeria na VVIP (Ghana).
SAUTI SOL (KENYA)MAFIKIZOLO (SOUTH AFRICA)MICASA (SOUTH AFRICA)NAVY KENZO (TANZANIA)R2BEES (GHANA)TOOFAN (TOGO)PSQUARE (NIGERIA)VVIP (GHANA)
Nimekuwekea hapa Full List ya mastaa wanaowania tuzo hizo.
BEST MALEDIAMOND PLATNUMZ (TANZANIA)EMTEE (SOUTH AFRICA)WIZKID (NIGERIA)FALZ (NIGERIA)OLAMIDE (NIGERIA)PATORANKING (NIGERIA)PHYNO (NIGERIA)
BEST FEMALETIWA SAVAGE (NIGERIA)VICTORIA KIMANI (KENYA)YEMI ALADE (NIGERIA)VANESSA MDEE (TANZANIA)CYNTHIA MORGAN (NIGERIA)MS VEE (GHANA)SIMI (NIGERIA)
BEST HIP HOPCASSPER NYOVEST (SOUTH AFRICA)OLAMIDE (NIGERIA)CDQ (NIGERIA)EMTEE (SOUTH AFRICA)EL (GHANA)RIKY RICK (SOUTH AFRICA)STANLEY ENOW (CAMEROON)PHYNO (NIGERIA)
BEST POPWIZKID (NIGERIA)KISS DANIEL (NIGERIA)TEKNO (NIGERIA)YEMI ALADE (NIGERIA)ADEKUNLE GOLD (NIGERIA)TIMAYA (NIGERIA)TIWA SAVAGE (NIGERIA)
DIGITAL ARTISTE OF THE YEARPSQUARE (NIGERIA)WIZKID (NIGERIA)A.K.A (SOUTH AFRICA)TIWA SAVAGE (NIGERIA)DAVIDO (NIGERIA)CASSPER NYOVEST (SOUTH AFRICA)TEKNO (NIGERIA)
BEST COLLABORATIONMR EAZI FT EFYA – SKINTIGHT (NIGERIA / GHANA)PATORANKING FT SARKODIE – NO KISSING (NIGERIA / GHANA)EDDY KENZO FT NINIOLA – MBILO MBILO REMIX (UGANDA / NIGERIA)EMTEE FT WIZKID & AKA – ROLL UP (SOUTH AFRICA / NIGERIA)DJ MAPHORISA FT WIZKID & DJ BUCKZ – SOWETO BABY (SOUTH AFRICA / NIGERIA)PHYNO FT OLAMIDE – FADA FADA (NIGERIA)OLAMIDE FT WANDE COAL – WHO YOU EPP (NIGERIA)HARRY SONG FT OLAMIDE, KCEE – RAGGAE BLUES (NIGERIA)MASTERKRAFT FT FLAVOUR & SARKODIE – FINALLY (NIGERIA / GHANA)
VIDEO OF THE YEARPANA BY TEKNO DIRECTED BY CLARENCE PETERS (NIGERIA)AJE BY ALIKIBA, DIRECTED BY MEJI (NIGERIA)BABANLA BY WIZKID DIRECTED BY SESAN (NIGERIA)ONE TIME BY A.K.A DIRECTED BY AKA & ALESSIOSIN CITY BY KISS DANIEL DIRECTED BY H2G FILMS (NIGERIA)EMMERGENCY BY D’BANJ DIRECTED BY UNLIMITED L.A (NIGERIA)MADE FOR YOU BY BANKY W DIRECTED BY BANKY W (NIGERIA)GBAGBE OSHI BY DAVIDO DIRECTED BY SLASH (NIGERIA)PRAY FOR ME BY DAREY DIRECTED BY MEX (NIGERIA)
BEST GROUP OR DUOSAUTI SOL (KENYA)MAFIKIZOLO (SOUTH AFRICA)MICASA (SOUTH AFRICA)NAVY KENZO (TANZANIA)R2BEES (GHANA)TOOFAN (TOGO)PSQUARE (NIGERIA)VVIP (GHANA)
SONG OF THE YEARKWESTA FT CASSPER NYOVEST – NGUD (SOUTH AFRICA)MR EAZI – HOL UP (NIGERIA)PATORANKING FT SARKODIE – NO KISSING (NIGERIA)WIZKID – BABANLA (NIGERIA)TEKNO – PANA (NIGERIA)EMTEE FT WIZKID – ROLL UP (SOUTH AFRICA / NIGERIA)DJ MAPHORISA FT WIZKID & DJ BUCKZ – SOWETO BABY (SOUTH AFRICA / NIGERIA)OLAMIDE FT WANDE COAL – WHO YOU EPP (NIGERIA)D’BANJ – EMMERGENCY (NIGERIA)
BEST NEW ARTISTEKOKER (NIGERIA)YCEE (NIGERIA)MR EAZI (NIGERIA)EMTEE (SOUTH AFRICA)SIMI (NIGERIA)NINIOLA (NIGERIA)TEKNO (NIGERIA)NASTY C (SOUTH AFRICA)
VIEWERS CHOICEMR SOLDIER – FALZ FT. SIMI (NIGERIA)BABANLA – WIZKID (NIGERIA)OSINACHI BY HUMBLESMITH FT DAVIDO (NIGERIA)PANA BY TEKNO (NIGERIA)HOLLUP BY MR EAZI (NIGERIA)PICK UP – ADEKUNLE GOLD (NIGERIA)MAMA – KISS DANIEL (NIGERIA)
LISTENERS CHOICELAGOS TO KAMPALA – RUNTOWN FT WIZKID (NIGERIA)BABANLA – WIZKID (NIGERIA)OMO ALHAJI – YCEE (NIGERIA)PANA BY TEKNO (NIGERIA)WHO YOU EPP – OLAMIDE FT WANDE COAL (NIGERIA)OLUWA NI – REEKADO BANKS (NIGERIA)PICK UP – ADEKUNLE GOLD (NIGERIA)SKINTIGHT – MR EAZI FT EFYA (NIGERIA / GHANA)
AFRICAN ARTISTE OF THE YEARWIZKID (NIGERIA)VANNESSA MDEE (TANZANIA)DIAMOND PLATINUMZ (TANZANIA)SARKODIE (GHANA)YEMI ALADE (NIGERIA)OLAMIDE (NIGERIA)
AFRICAN PRODUCER OF THE YEARDJ MAPHORISA (SOUTH AFRICA)GOSPEL ON THE BEAT (NIGERIA)MASTERKRAFT (NIGERIA)YOUNG JOHN (NIGERIA)LEGENDURY BEATS (NIGERIA)SESS THE PROBLEM KID (NIGERIA)

Trump Aaanza Kuitibua China

$
0
0
CHUMA BLOG
cda-china_20160601Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina, Wang Yi
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Uchina, inasema kuwa imepeleka malalamiko kwa upande unaohusika wa Marekani, baada ya Rais mteule Donald Trump, kuzungumza kwa simu na rais wa Taiwan.
483208412-real-estate-tycoon-donald-trump-flashes-the-thumbs-up-jpg-crop-promo-xlarge2Rais mteule Donald Trump
Uchina inaona Taiwan kuwa ni jimbo lake lilojitenga na siyo nchi. Msemaji wa wizara alisema, Uchina ni moja, na ndio msingi wa kisiasa katika uhusiano baina ya Marekani na Uchina.
Mazungumzo ya simu baina ya Bwana Trump na Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, yamevunja msimamo wa kidiplomasia kwa Marekani.
tsai-ing-wen 
Hapo awali, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina, Wang Yi, alisema mazungumzo hayo ya simu ni “ujanja wa Taiwan usiokuwa na maana”.
Imeelezwa kuwa, ikiwa simu hiyo ni ishara ya mabadiliko ya sera za Marekani kuhusu Taiwan, basi Uchina itajibu kwa hasira.


Meli za mizigo na abiria katika ziwa Nyasa itahimarisha uchumi wa wananchi wa Mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma

$
0
0
CHUMA BLOG
 Kaimu Meneja  wa bandari ya Itungi na Kiwira Eng. Juma Kisavara (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati) kuhusu namna ya kuondoa mchanga katika kingo za ziwa Nyasa ili kuwezesha meli zinazotengenezwa kuingizwa katika maji kwa urahisi.
Meneja wa Wakala wa barabara Mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa akifafanua jambo kwa  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipokagua ujenzi wa barabara ya Kikusya-Ipinda hadi Matema KM 34.6 ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami.Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


Imeelezwa kuwa uchumi wa wananchi wa Mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma utaimarika kwa kasi kama watatumia vizuri fursa ya uwepo wa meli za mizigo na abiria katika ziwa Nyasa.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa meli mbili za mizigo za Mv. Njombe na Mv. Ruvuma na ujenzi wa meli ya abiria ya Mv. Mbeya ni fursa mpya ya kiuchumi kwa wakazi wa mikoa hiyo.

“Tumejipanga kuhakikisha tunafungua ukanda huu wa nyanda za juu kusini kiuchumi hivyo ni jukumu la wananchi kuchangamkia fursa za kibiashara zinazoweza kusafirishwa ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi”.amesema Eng. Ngonyani.

Naibu Waziri Ngonyani ameelezea kuridhishwa kwake na hatua ya ujenzi wa meli za Mv.Njombe na Ruvuma ambao umefikia asilimia tisini na tisa na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwaamini makandarasi wazawa wanaofanya kazi kwa ubunifu, uadilifu na uaminifu ili kutoa fursa nyingi za ajira kwa watanzania.

Kaimu Meneja wa bandari ya Itungi na Kiwira Eng. Juma Kisavara amemhakikishia Naibu Waziri Ngonyani kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kuhaikikisha bandari zote kumi na tano zilizopo katika ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania zinafufuliwa na kutumika kupakia na kushusha mizigi ikiwemo vifaa vya ujenzi, makaa ya mawe,mbolea na mazao ambayo yana soko ndani na nchi za jirani.

Eng. Kisavara amemhakishia Naibu wa Ujenzi kuwa tayari wametafuta soko la kutosha la kusafirisha mizigo hivyo kuiomba Serikali kuendelea na kasi ya ujenzi wa meli nyingine zitakazotumika katika ziwa Nyasa.

Zaidi ya shilingi bilioni 11 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Meli ya Mv.Ruvuma na Mv. Njombe zinazojengwa na kampuni ya Songoro Marine Transport ya hapa nchini na meli hizo zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali mwezi Januari mwakani.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ngonyani amekagua ujenzi wa barabara ya Kikusya-Ipinda hadi Matema KM 34.6 wilayani Kyela inayojengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuwa Serikali italipa fedha kwa mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili kuiwezesha kukamilika kwa muda uliopangwa.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

WAZIRI POSSI ATEMBELEA VITUO NA SHULE ZA WATU WENYE ULEMAVU MIKOA YA MWANZA NA SIMIYU

$
0
0
CHUMA BLOG
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu)Mhe. Dkt. Abdallah Possi akipokea mafuta maalumu ya ngozi kwa watu wenye ualbino kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha kuhudumia watoto wenye Ualbino cha Lamadi Bi. Hellen Ntambulwa ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa ziara yake kituoni hapo. Novemba 20, 2016
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye ualbino wanaolelewa na Kituo cha Lamadi Wilayani Busega Mkoa wa Simiyu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimsikiliza Mwandishi wa habari wa ITV Bw. Berensi China wakati wa ziara yake Kituo cha kulelea watoto wenye Ualbino cha Lamadi Simiyu.

Dimpoz Afunguka Kuhusu Mubenga

$
0
0
CHUMA BLOG
Msanii Ommy Dimpoz amekanusha tetesi za kuwa na ugomvi na aliyekuwa ‘business partiner’ ambaye pia alikuwa meneja wake maarufu kwa jina la Mubenga, baada ya kila mmoja kuchukua hamsini zake na kufanya yake.

Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television Ommy Dimpoz amesema Mubenga ameamua kufanya biashara zake mwenyewe bila kushirikiana naye, kitu ambacho ni jambo zuri kwake na kwa maendeleo pia, lakini hawana tofauti na hata akihitaji msaada wake, yupo tayari kumsaidia.

“Mubenga ameenda kuanzisha kitu chake, hiyo ni pongezi na hayo ni maendeleo, mnataka kila siku awe chini ya Ommy! yeye ameenda kuazisha kitu chake, kampuni yake, ana wasanii wake anawasimamia, anajua kwamba afanye vipi anahitaji ku’move on’, kwa hiyo ilikuwa ni movement yake yeye kwamba ameamua kufanya kazi zake mwenyewe which is good, na mimi hata leo akisema Ommy nataka suport hii kwa wasanii wangu i’m ready”, alisema Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz amesema hata tetesi za kuchukua hela za Mubenga na gari hazina ukweli wowote, ni maneno tu ya uzushi ya mashabiki, na bado anamchukulia kama ndugu yake.

MAGAZETI YA LEO 22 NOV JUMANNE

Sasa Inang’aa Kama Airport,Hii Ndiyo Stendi Mpya ya Mabasi Msamvu Morogoro

$
0
0
CHUMA BLOG
msamvu-1Upande wa kuingilia abiria kwenye stendi hiyo.
msamvu-2Abiria wakisubili usafiri.
msamvu-3 
 Moja ya mabasi hayo likiingia eneo la stendi na kupakia na kushusha abiria.msamvu-4Muonekano wa mbele wa stendi hiyo. msamvu-5Pia kama huna tiketi kuingia kwenye stendi hiyo utarazimika kulipia Tsh. 200, ichani mmoja wawafanyakazi wa stendi hiyo akikusanya pesa hizo.msamvu-6Basi la Kisbo baada ya kushusha na kupakia abiria lilikaguliwa na polisi kisha kuruhusiwa kutoka kwenye geti la stendi hiyo na kuendelea na safari. msamvu-7msamvu-8msamvu-10Bustani zikichanua.
msamvu-11Muonekano wa nyuma wa stendi hiyo kulia mwenye T-shirt ya Bluu Jumanne Mtangwa beki wa zamani wa Klabu ya Reli ya Morogoro ‘Kiboko ya Vigogo’ ambaye kwa sasa ni mpiga-debe kwenye stendi hiyo akimuongoza mwandishi wetu kumuonesha maeneo mbalimbali ya stendi hiyo.
msamvu-12
HATIMAYE baada ya ukarabati wa takribani miaka miwili, hatimaye Stendi ya Mabasi ya Mikoani ya Msamvu iliyopo Morogoro imefunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita huku ikiwa na muonekano wa kisasa kabisa na wengine kuifananisha na uwanja wa ndege ‘Airport’.
 
Leo asubuhi tovuti yetu imetinga ndani ya stendi hiyo ya kisasa ambayo iko kwenye hatua za mwisho za kumalizia ukarabati kwa kiwango cha hali ya juu, ambapo picha zilizopigwa zinaonesha namna ambavyo mandhari ya stendi hiyo yanavyovutia kwa sasa tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya ukarabati.
 
Wameshuhudiwa abiria wengi wakipanda na kushuka kwenye mabasi kama wako uwanja wa ndege huku wengine wakisubili usafiri ili kuelekea sehemu mbalimbali.
 
Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa viongozi wa Stendi hiyo, ameeleza kuwa, endapo wakimkamata mtu yoyote akitupa takataka ama kukanyaga bustani atatozwa faini ya Tsh. 50,000/= papo hapo.

UNDP, ESRF wafanya uzindua Ripoti ya Maendeleo Afrika 2016

$
0
0
CHUMA BLOG
 Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi katika halfa ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2016.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika halfa ya  uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2016.
 Wageni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya halfa ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2016.


Na Mwandishi Wetu
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) likishirkiana na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) limefanya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2016 ambayo imekuwa na kauli mbiu ya Kuongeza Kasi ya Kuweka Usawa wa Kijinsia na Kuwawezesha Wanawake.

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo alisema kuwa ripoti hiyo inaonyesha jinsi gani watu wanaoishi Afrika wanapiga hatua kupata maendeleo lakini wakikabiliwa na changamoto usawa wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake.

"Kupitia ripoti hii UNDP inaonyesha jinsi gani watu wanaoishi Afrika wanajihusisha na shughuli za maendeleo lakini bado kuna changamoto ya usawa wa kijinsia, jambo la kijisnia linagusa kila sehemu kuanzia serikalini, taasisi za kijamii, mashirika binafsi na hata kwenye vyombo vya habari,

"Kwa sasa Afrika ndiyo ya mwisho kwa maendeleo ya binadamu kulinganisha na sehemu zingine duniani na jambo la usawa wa kijinsia linabaki kuwa muhimu, UNDP itaendelea kushirikiana na serikali kusaidia kupatikana usawa wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake ili kumaliza vitendo hivi ambavyo vinachangia Afrika kuwa nyuma kimaendeleo," alisema Dabo.

Nae mgeni rasmi katika uzinduzi wa ripoti hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga alisema serikali inafahamu kuwepo kwa changamoto hiyo na imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwepo kuwapa nafasi za uongozi wanawake.

Alisema ripoti hiyo itaisaidia Serikali kuweza kuweka mikakati bora na ambayo itaweza kumaliza tatizo la usawa wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuangalia kwa jinsi gani watawawezesha wanawake ili waweze kujihusisha na shughuli za maendeleo ambazo ziwasaidia kukuza kipato chao lakini pia taifa kwa ujumla.

"Ripoti hii itasaidia kupata mipango ambayo inaweza kutumiwa kwa ajili ya changamoto iliyopo ya usawa wa kijinsia, ripoti inaonyesha jinsi gani wanawake wanaweza kusaidia kuleta maendeleo lakini bado wanakabiliwa na tatizo la usawa na hivyo kukwamisha ukuaji wa uchumi,

"Naomba niwahakikishie serikali ya Tanzania itakwenda kuitumia ripoti kuboresha sera, mipango na vitendo ili kupatikana usawa wa kijinsia na pia kusaidia kukuza uwezeshaji kwa wanawake wa Tanzania, serikali imekuwa ikisaidia kuweka usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na hata makamu wetu wa Rais ni mwanamke na katika hili tutahakikisha wanawake wanaendelea kupata nafasi na kusaidia kuleta maendeleo," alisema Nkinga.

Kwa upande wa ESRF kupitia Mkurugenzi Mtendaji, Dk. Tausi Kida alisema "Tunafahamu kuwa usawa wa kijinsia ni jambo ambalo limekuwa likitafutiwa ufumbuzi tangu tukipata uhuru na katika hilo (ESRF) tumekuwa tukiunga mkono jitihada za serikali kwa ajili ya kuweka usawa kwa Watanzania, tunaamini ripoti itasaidia kuleta maendeleo kwa Tanzania katika mpango wa maendeleo ulizindiliwa Dodoma"

Mastaa Wa Bongo Washinda Tuzo Za Abryanz Style & Fashion Awards 2016, Kampala Uganda

$
0
0
CHUMA BLOG
fashionMwanamitindo Hamisa Mobeto akiwa na tuzo ya Fashionista Of The Year East Africa baada ya kushinda.uganda-4Msanii wa Nigeria, Waje.
14334371_306248876400642_1179069908_n
Akosua Veronica
uganda-6uganda-9Vanessa Gyan
uganda-10uganda-11Mastaa mbalimbali wakiwa katika mapozi tofauti.
uganda-12 
Zynell Zuh
Usiku wakuamkia leo zilifanyika tuzo za Fashion zinazojulikana kama Abryanz Style & Fashion Awards (ASFA 2016) katika hoteli ya Serena,  Kampala Uganda, tuzo hizi zilihusisha mastaa mbalimbali  kutoka Afrika wakiwemo mastaa wa Tanzania. Mastaa  wa Tanzania walioshinda tuzo hizo ni Millen Magese,  Martin Kadinda, Vanessa Mdee,  Alikiba, Hamisa Mobetto, Alikiba, Wema Sepetu na Idris Sultan
List ya washindi wa tuzo za ASFA 2016
Humanitarian award – Millen Magese (Tanzania)
Best Dressed Celebrity West Africa – Deborah Vanessa(Ghana)
Continental Style & Fashion Influencer Female – Bonang Matheba (South Africa)
Continental Style & Fashion Influencer Male – David Tlale (South Africa)
Fashion Designer Of The Year UG – Anita Beryl (Uganda)
Fashion Designer Of The Year East Africa – Martin Kadinda (Tanzania)
The Most Stylish Artiste in Uganda – Eddy Kenzo (Uganda)
The Most Stylist Artiste East Africa Female – Vanessa Mdee (Tanzania)The Most Stylish Artiste East Africa – Alikiba (Tanzania)
The Most Stylish Couple – Annabel Onyango na Marek Fuchs (Kenya)
Fashionista Of The Year Male – Abduz (Uganda)
Fashionista Of The Year East Africa – Hamisa Mobetto (Tanzania)
Most Fashionable Music Video – Bebe Cool (Uganda)
Best Dressed Celebrity East Africa Female – Wema Sepetu (Tanzania)
Best Dressed Celebrity East Africa Male – Jamal Gaddafi (Kenya)
Most Fashionable Music Video Africa – AJE – Alikiba (Tanzania)Best Dressed Media Personality/Entertainer – Idris Sultan (Tanzania)

New AUDIO | Tekno - RARA

New AUDIO | Dada Hood - Hola Holaaa

JPM Akutana na Kuzungumza na Bilionea Dangote, Pia Amuapisha Ole Sendeka na Watumishi wa Wizara

$
0
0
CHUMA BLOG
magufuli-na-dangote
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.
Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.
Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu ambao walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.
Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.
”Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili ” amesema Rais Magufuli.
Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43 kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.
Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje.
Katika kuthibitisha hilo, tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.
Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania na kamwe hana nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Katika hatua nyingine Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).
Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam.
10 Desemba, 2016.

magufuli-na-dangote1
Rais Dkt John Pombe Magufuli (kulia) akimkaribisha Mkurugenzi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Cement Industries cha jijini Mtwara ambaye ni raia wa Nigeria na Bilionea Namba Moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 10, 2016.
ole-sendeka-akiapaRais Dkt. Magufuli akiwapisha Christopher Olonyokie Ole -Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

MSAIDIZI wa Mbowe, Ben Saanane Adaiwa Kupotea Tangu Nov 18, Hata Simu Zake Hazipatikani

$
0
0
CHUMA BLOG
Moja kati ya wasaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa siku 22 hadi leo.

Taarifa zilizothibitishwa na ndugu zake pamoja na Chadema zimeeleza kuwa Ben Saanane ambaye ni Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa chama hicho alitoweka tangu Novemba 18 mwaka huu na kwamba hata simu zake zote hazipatikani tangu wakati huo.

Kufuatia hali hiyo, familia yake imesema iliripoti katika kituo cha polisi kilichoko Tabata jijini Dar es Salaam anakoishi Saanane na kupewa jalada lenye kumbukumbu namba TBT/RB/8150/2016.

“Kaka anafanya kazi Chadema akiwa miongoni mwa wasaidizi wa Mwenyekiti Freeman Mbowe. Ametoweka katika mazingira ya kutatanisha maana kazini wanamtafuta na nyumbani wanamtafuta bila mafanikio,” mdogo wake Ben aliyejitambulisha kwa jina la Erasto Saanane anakaririwa na Tanzania Daima.

Aliongeza kuwa wamefanya jitahada zote wakisaidiana na Jeshi la Polisi, kuangalia katika hospitali zote pamoja na vyumba vya kuhifadhia maiti jijini Dar es Salaam lakini hawakupata jibu.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanaendelea na jitihada za kumtafuta ikiwa ni pamoja na kuandaa utaratibu wa kichama kufahamu undani wa tukio hilo.

Hata hivyo, Kamadna wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdun alipotafutwa na gazeti hilo alieleza kuwa ofisi yake haijapokea taarifa za tukio hilo.

Chanzo: Tanzania Daima

Washindi Wa Tuzo Za EATV 2016 Hawa Hapa

$
0
0
CHUMA BLOG
jide
MWANAMUZIKI BORA CHIPUKIZI
Feza Kessy
Mayunga Nalimi (Mayunga)
Amani Hamisi (Man Fongo) – Mshindi
Rashid Said (Bright)
Rukia Jumbe (Rucky Beby)


KUNDI BORA LA MWAKANavy Kenzo – Mshindi
Mashauzi Classic
Team Mistari (Kenya)
Sauti Sol (Kenya)
Wakali Wao


MUIGIZAJI BORA WA KIKEChuchu Hansy – Mshindi
Rachel Bithulo
Frida Kajala Masanja
Khadija Ally


MUIGIZAJI BORA WA KIUME
Meya Shabani Hamisi
Salim Ahmed (Gabo) – Mshindi
Daudi Michael (Duma)
Dotto Hussein Matotola
Saidi Mkukila
VIDEO BORA YA MWAKA
Namjua – Shetta
Njogereza – Navio
Aje – Ali Kiba – Mshindi
Don’t Bother – Joh Makini
NdiNdiNdi – Lady Jay Dee
WIMBO BORA WA MWAKA
Don’t Bother – Joh Makini
NdiNdiNdi – Lady JayDee
Kamatia Chini – Navy Kenzo
Aje – Alikiba – Mshindi
Moyo Mashine – Ben Pol
FILAMU BORA YA MWAKA
Facebook Profile
Safari ya Gwalu – Mshindi
Mfadhili Wangu
Hii ni Laana
Nimekosea Wapi
MWANAMUZIKI BORA WA KIKE
Lilian Mbabazi (Uganda)
Ruby
Lady Jay Dee – Mshindi
Linah
Vanessa Mdee
TUZO YA HESHIMA KACHUKUA BONNY LOVE

MWANAMUZIKI BORA WA KIUME
Gnako
Shetta
Mwana FA
Ben Pol
Alikiba – Mshindi
Viewing all 2614 articles
Browse latest View live