CHUMA BLOG
Ama kweli mtoto wa nyoka huwa ni nyoka na Chura hawezi kuzaa Ng'ombe Mtoto wa Osama Anayeitwa Hamza Bin Laden ameonyesha kuanza kufata nyayo za Marehemu baba yake, Ametoa ujumbe wa nne kwa dunia kwa kutumia dakika 26.
![]() |
Hamza Bin Laden |
Ambapo kundi la kigaidi la AL QAEDA ndiyo walioachia ujumbe huo wa mtoto wa Gaidi aliyetikisa Dunia Osama Bin Laden.
Katika Ujumbe Huo Hamza anasisitiza waislamu kuungana na Kupambana na Saudi Arabia ambao wamekuwa kama Kibaraka wa mataifa ya Magharibi. Hamza katika ujumbe huo kuwa anaamini waislamu wote ni Osama (Wafuasi wa Sera za Osama) kwa hiyo ni lazima waungane kuwapinga Saudi Arabia na sera zote za Nchi za Magharibi kama Marekani.