CHUMA BLOG
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Kijana Alhaji Hussein Kulia akiwa chini ya Ulinzi.
Wazazi wa watoto hao wakipanda kwenye Difenda
KIJANA Alhaji Hussein[27]ambaye ni Fundi wa Magari Mjini hapa amenaswa na Polisi akidaiwa kuwalawiti watoto wawili wa kiume wenye umri wa Miaka mitatu na Mitano ambao majina yao yanahifadhiwa kwa kuzingatia Maadili.
Tukio hilo la kusigitisha lilijiri katika eneo lenye gereji nyingi jirani na shule ya Msingi Kiwanja cha Ndenge Mtaa wa Ukutu Kata ya Uwanja wa Taifa Manispaa ya Morogoro.
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo Mwandishi wa habari hizi alitinga fasta eneo la tukio na kushuhudia umati wa watu ukiongozwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro kwa[Chadema] Devotha Minja wakimkamatwa Mtuhumiwa huyo.
Akisimulia Kisa na Mkasa Mmoja wa wazazi wa watoto hao Zainabu Abdul alikuwa na haya ya kusema.
"Mwanangu aliludi nyumbani akilalamika Maumivu makali sehemu za siri nilipomchunguza nilistuka na kubaini alilawitiwa nilipomuuliza nani alimfanyia kitendo hicho hakumtaja lakini akasema hakufanyiwa wenyewe bali alikuwa na mwenzake akamtaja jina.
Nilikwenda kwa Mama wa huyo mtoto tukakubaliana tuwabane watoto wetu ndipo ndipo wakasema walifanyiwa kitendo hicho kwenye moja ya gereji zilizopo jirani na nyumba zetu.
Tuliongozana na watoto wetu hadi kwenye gereji hiyo wote wakamuonyesha kijana huyo ambaye ni Alhaji Hussein tulipomuuliza alibisha ndio tukatoa taarifa kw amwenyekiti wa Mtaa ambaye naye alitoa taarifa polisi wapo wengine walitoa taarifa kwa Devota Minja"alisema mama huyo.
Polisi walipofika eneo la tukio wazazi hao walitoa maelezo ambayo piawalikwenda kuyatoa kituo kikuu cha polisina kupewa jalada la kesi lR/5687/2016 ULAWITI.
Pamoja na fomu ya PF3 kwa ajili ya vipimo vya matibabu ya watoto hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo Kulwa Tobelo alithibitisha tukio hilo kutokea kwenye Mtaa wake.