CHUMA BLOG
![]()
![]()
![]()
![]()
Gari aina ya Suzuki 'Kilikuu' lenye namba za Usajiri T 609 CKW Muda huu linaendelea kuteketea kwa Moto eneo la Masika katikati ya Mji wa Morogoro.
Mashuhuda wa tukio hilo " Huyu dereva wa kilikuu alikuwa akitokea upande wa Msamvu na alipofika hapa Masika jirani na Mzunguko wa barabara tulishuhuida gari lake likiwaka Moto upande wa Nyumba na yeye hakuwa na habari aliendelea na safari hivyo boda boda mmoja aliamua kuwasha pikipiki yake na kumkimbilia na kumjulisha tukio hilo ambapo alisimama na kushuhudia gari hilo likiendele kuwaka moto"walisema Mashuhuda hao
Dereva wa gari hilo Michael Agostino alisema " Nashangaa sana huu moto ulikotokea gari hili injini iko mbele iweje moto utokee huku nyuma ambako hakuna kitu chochote na kama unavyoona sikuwa na mzigo wowote ndani ya gari na washukuru hawa boda boda wa hapa Masika wamenikimbilia na kunipa taarifa za Moto huo vinginevyo ungefika huku mbele kiwa kwenye mwendo nahisi milango ingejirock na mimi kuungua vibaya namshukuru Mungu kwa hili"alisema Agostino huku akipiga simu kwa mmiliki wa gari hilo
Askali wa kikosi cha Zima moto Mwenye nyota Moja akimhoji dereva wa gari hilo huku wakikagua kifaa Maarumu cha kuzima moto kilichokuwa ndani ya gari hilo.