Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

WAZIRI WA TAMISEMI SULEIMAN JAFO ALIVYONUSURIKA KIFO AJALINI MBEYA

$
0
0
CHUMA BLOG

Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo  jana amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.


Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.


Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari Waziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo.


Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa! Lakin bahat nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguzi alisema hakuumia popote ni wazima.


Alisema baada ya hapo Waziri na watu waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge


Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.

Askari wa usalama barabaran wilayani Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea

Picha zote kwa hisani ya Mbeya yetu

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Trending Articles