Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

MKAZI WA JIJI LA DAR AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA MOROGORO.

$
0
0
CHUMA BLOG

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei (kushoto), akiwaonyesha waandishi wa habari magunia ya bangi yaliyokamatwa katika eneo la Mindu.



JESHI la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Bungoni Ilala, jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi kilo 60 akisafirisha kuelekea jiji humo.

Akizungumza mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 5, mwaka huu, saa 1:00 asubuhi, katika eneo la Mindu barabara ya Iringa – Morogoro.

Alisema askari wa jeshi hilo wakiwa katika doria ya kawaida katika barabara hiyo, walilishuku gari aina ya Toyota Carina lilokuwa likiendeshwa na mtuhumiwa na kuamua kulisimamisha.

Alisema baada ya kulisimamisha gari hilo, polisi walifanya upekuzi na ndipo walipokuta bangi hiyo katika buti la nyuma ikiwa imewekwa katika magunia, huku ikiwa imefichwa na mifuko ya plastiki.

“Hizo gunia za bangi zilikuwa zimefungwa kwa ustadi mkubwa katika vigunia vitatu na kufichwa kwenye mifuko ya plastiki, huyo jamaa anaonekana ni mtaalam sana," alisema. 


Kamanda Matei alisema mtuhumiwa alipohojiwa alisema kuwa amekuwa akifanya kazi ya kuuza bangi jijini Dar es Salaam kwa kipindi kirefu na kwamba uchunguzi unaendelea na atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Trending Articles