Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

BODA BODA AGONGA MTI NA KUFALIKI HAPO HAPO MOROGORO

$
0
0
CHUMA BLOG
Wananchi wakiuangalia mti huo ukiwa katikati ya barabara ya Mazimbu

 Muonekano wa pikipiki
 Muonekana wa boda boda ya Marehemu kwa nyumba yenye namba za usajiri MC 673 AXE
 Baada ya kuanguka mti huo pia uliangusha nyaya za umeme

            Baadhi ya madereva wakipita kando ya mti huo kwa tahadhari kubwa     
 
KIJANA Said Hamis Maarufu kwa jina la 'Popo' ambaye ni dereva wa Boda boda Mjini hapa,amefariki dunia baada ya kugonga Mti uliokuwa Umedondoka barabarani katika eneo la Mazimbu Majira ya Saa 2 usiku. 
Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mti huo uliangushwa na Upepo Mkali uliokuwa ukivuma ambapo ulidondoka na kuangusha nguzo za Umeme kisha kuziba barabara hiyo muda mchache tu baada ya boda boda huyo kupita akiwa na abiria.
" Alikuwa anapaki  hapa hapa karibu sasa akapata abiria akampeleka Kihonda wakati huo mti ulikuwa haujaanguka sasa wakati anarudi akiwa kwenye Mwendo Mkali  ndio akaparamia matawi ya huu mti na yakamchana tumbo akafariki hapo hapo"alisema Juma Athuman. 
Naye Jacob Joseph alisema "lngawa tunaweza kusema ahadi yake ilikuwa imefika lakini pia tunatakiwa kuchukua tahadhari tuwapo barabarani tatizo la hawa Vijana kila Mahari wanaendesha Pikipiki kwa mwendo kasi katoka Mbali Kihonda kafika hapa kijiweni alitakiwa kupunguza mwendo kwa sababu licha ya Mti kuanguka hapa pia kuna reli dereva makini angepunguza mwendo tangu mbali kama angekuwa katika mwendo wa kawaida angeuona Mti huu  na kupita pembeni kama hawa wenzake wanavyofanya"
 Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Boma 'A' Kata ya Mazimbu Kilewa Bohari amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo katika Mtaa wake. 
" Kweli tukio hilo limetokea jana majira ya saa 2 -30 usiku Marehemu Said Hamis Popo alikuwa akiegesha boda boda yake eneo la Kiti motojirani kabisa na eneo alilopata ajari"alisema mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa vijana wenzake walifika ofini kwake kwa lengo la kuchangisha Michango  akawaambia yeye hausiki kwa kuwa marehemu hakuwa Mkazi wa eneo hilo. 
Marehemu alisafirishwa kwenda kwao Muheza Mkoani Tanga kwa mazishi.
 
Na Dustan

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Trending Articles