Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza ofisi za gazeti la Uhuru

$
0
0
CHUMA BLOG
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Septemba, 2016 amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za Gazeti la Uhuru zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi.
Katika Mazungumzo hayo, wafanyakazi wa Gazeti la Uhuru linalomilikiwa na CCM wamelalamikia kutolipwa mishahara yao kwa miezi saba, kutotolewa kwa michango ya wafanyakazi kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti katika hali ya kutatanisha, kutotambuliwa katika ajira kwa baadhi ya wafanyakazi, kutolipwa kwa madeni wanayozidai taasisi za Serikali na wanaostaafu kutolipwa mafao yao.
Wafanyakazi hao pia wamemueleza Rais Magufuli kuwa Bodi na Menejimenti ya kampuni ya vyombo vya habari vya chama inayoendesha Gazeti la Uhuru na Redio Uhuru zimeshindwa kuendesha vyombo hivyo na wamemuomba aingilie kati ili kuvinusuru vyombo hivyo ambavyo kwa sasa vina hali mbaya kutokana na kukabiliwa na madeni makubwa, na biashara yake imeshuka kwa kiasi kikubwa.
Akijibu malalamiko hayo Rais Magufuli aliyetembelea ofisi za Gazeti la Uhuru akitokea Ofisini kwake katika jengo la Makao Makuu ya chama, Ofisi Ndogo ya Lumumba Jijini Dar es Salaam amemuagiza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahaman Kinana kuhakikisha mishahara yote wanayodai wafanyakazi inayofikia Shilingi Milioni 609 inalipwa ndani ya Mwezi huu wa Tisa.
Aidha ameagiza kupatiwa orodha ya taasisi za Serikali zinazodaiwa na Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, na pia ameagiza deni linalodaiwa na NSSF kutokana na kutowasilishwa kwa makato ya wafanyakazi lilipwe.
Kuhusu malalamiko dhidi ya Bodi na Menejimenti ya Kampuni hiyo, ajira za wafanyakazi, mafao kwa wastaafu, kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti na mazingira magumu ya kazi Dkt. Magufuli ameahidi kuyafanyia kazi.
79116
KK
Msanja Mkandamizaji akitoa neno huku akitumia kipaji chake cha uchekeshaji siku ya Jumamosi Septemba 17, 2016 kwenye siku ya tamasha la utamaduni wa Afrika Mashariki lililofanyika Olney, Maryland nchini Marekani. Katika onyesho hilo kulikuwepo na vikundi mbalimbali vya utamaduni kutoka Afrika Masahariki, wakiwembo wasanii wa nyimbo za injili na onyesho la mavazi kutoka nchi tano zinazounda jumuiya hiyo. Na mapema mchana tamasha lilianzia na nyama choma. Picha na Vijimambo Blog /Kwanza Production. Masanja Mkandamizaji akifanya vitu vyake. Masanja Mkandmizaji akiendelea kutoa neno la Mungu huku akiwaacha hoi watazamaji na watu wengine waliokua wakimsikiliza wakiwemo wachungaji. Watu wakimfuatilia kwa makini Masanja Mkandamizaji. Vikundi vingine vya utamaduni vikitumbuiza wakiwemo waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili. Watu wakifuatilia onyesho.

Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef

Trending Articles