Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Picha : Scorpion ‘Mtoboa Macho’ Apandishwa Kizimbani

$
0
0
CHUMA BLOG
SCORPION CHINI YA ULINZI: Mtuhumiwa wa unyang'anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete maarufu 'Scorpion' akisindikizwa chini ya ulinzi wa polisi na askari magereza kuelekea kwenye basi la magereza kurudishwa rumande huku akicheka baada ya waandishi kubaini mbinu zake za kubadilisha nguo ili wasimtambue baada ya kusomewa shitaka lake katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam jana. Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumvamia na kumtoboa macho mkazi mmoja wa Dar es Salaam hivi karibuni. (Na Mpigapicha Wetu).Scorpion.
MKAZI wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama Scorpion, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumtoboa macho yote mawili Said Mrisho.
Scorpion alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Adelf Sachore na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Munde Kalombola.
Akisoma mashitaka hayo, Kalombola alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu eneo la Buguruni Sheli wilaya ya Ilala.
Munde alidai, Njwele aliiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili na fedha taslimu Sh 331,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Mrisho.
Kalombola alidai kuwa mshitakiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu machoni, tumboni na mabegani mlalamikaji ili ajipatie mali hizo.
Hata hivyo, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na upande wa mashitaka uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutaja.
Hakimu Sachore aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 19, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. Mshitakiwa alirudishwa rumande kutokana na mashitaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Trending Articles