CHUMA BLOG
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Eneo la Soko Kuu la Morogoro ambapo baada ya kuvunjwa kwa lengo la kumpisha mkandarasi kujenga soko la Kisasa ya ghoroga baadhi ya wamachinga waliendelea kupanga bidhaa zao eneo hilo la soko kando kando ya barabara ya Madaraka
Wamachinga wakisombelea matofari kutoka kwenye eneo hilo la Soko na kuyapanga katikatika ya barabara ya Madaraka muda huu
Pia walipanga meza zao zilizovunjwa na mgambo wa Manispaa kwa lengo la kuchoma moto katikatika ya barabara hiyo.
....wakizidi kupanga mawe barabarani.
...Wakiziba barabara hiyo kwa kamba
Umati wawatu ukishuhudia tukio hilo muda huu.
pia baadhi ya watu walipanmga juu ya maghorofa na kushuhudia vyema matukio hayo
Machinga Florida Lupengo eneo la tukio
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Regina Chonjo[kushoto] na Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga [Kulia] wakiwasili eneo la tukio.
Mkuu wa wilaya akisikiliza maelezo wa mmoja wa machinga hao ambaye alisema" Chanzo cha Vulugu hizi ni hawa viongozi wa Manispaa ambao walituambia kwamba wametupatia eneo la Manzese kwa lengo la kufanya biashara zetu lakini wakadai kila siku tuwape elfu 5 kwa lengo la kubeba kifusi hapa soko la zamani na kukipeleka eneo hilo la Manzese toka majuzi tunalipa pesa hiyo chaajabu leo Mgambo wa Mnispaa wamekuja ghafra na kutuondoa eneo hili huku wakipora biashara zetu wakati wengi tuna mikopo na tunasomesha watoto" alisema mama huyo.
Baada ya kusikia madai hayo mazito Mkuu huyo wa Wilaya aliwauliza kama wanawafahamu maafisa hao wa manispaa waliowachangisha fedha hizo ambapo kwa pamoja walisema wanawajua.
Hivyo Mkuu huyo aliwataka baadhi ya machinga hao wafike ofisini kwake kwa lengo la kuwataja Maafisa hao.
Chaajabu Wamachinga hao baada ya kuelekea ofisi za mkuu wa Wilaya waliandamana hadi Manispaa huku wakiimba ''Tunataka hela zatu'' walipofika Manispaa walikuta geti limefungwa na walizuiwa kuingia ndani na walipojaribu kufanya vulugu Askali polisi na Mgambo wa Manispaa walitoka nje ya geti na kuwakamata wamachinga hao.
Wamachinga hao wakiandamana kuelekea Manispaa.
mgambo hao wakiingiza ndani baadhi ya bidhaa za machinga hao baada ya kuzikamata mtaani
Mwanamke huyo akiingiza ndani ya ofisi za Manispaa baada ya kukamtwa kwenye vulugu hizo
Mgambo hao wakimwingiza ndani machinga huyo msobe msobe baada ya kumkamata.