Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all 2614 articles
Browse latest View live

Lowassa Aunga Mkono Maamuzi Ya CUF Kutoshiriki Uchaguzi Zanzibar

$
0
0

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch UKAWA, Mh. Edwrad Lowassa amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwaka huu.
Mh. Edward Lowassa amesema hayo ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na wazee kutoka chama cha Chadema ambapo amesema  anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya mach 20 huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika.

Aidha amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na uongozi mzima wa UKAWA wako imara katika kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanaznia ambapo pia amemshukuru waziri mkuu kwa kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa fursa ya kuajipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura mapema 25 ,huku pia akiigusia katiba ya Tanzania.

Kwa mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enec Ngombare wamempongeza Mh. Lowassa kwa na uvumilivu wake baada ya uchaguzi ambapo pia wamemhakikishia kuwa wako pamoja nae katika safari ya kuelekea mwaka 2020.

Katika mkutano huo pia uliohudhuliwa na kada wa siku nyingi Kingune Ngombare Mwiru, Mh Lowassa amewataka wazanzibar na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu na kuhakikisha wanadumisha amani ya nchi hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi za kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani Zanzibar.
 Source: ITV

Mke wa Kafulila atimuliwa nje ya ukumbi wa bunge

$
0
0
Mbunge wa Viti maalum Chadema Jesca Kishoa ametolewa nje ya ukumbi wa bunge na kutakiwa kutohudhuria vikao viwili vya bunge linaloendelea mjini Dodoma.

Hayo yamejiri katika mkutano wa 7 wa bunge la 11 linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma ambapo Mwenyekiti wa kikao cha leo Andrew Chenge amelikumbusha bunge kuhusiana na kauli aliyoitoa mbunge huyo tarehe 01/02/2016.
  
Mbunge huyo alisema kwamba Waziri Harrison Mwakyembe alihusika kununua mabehewa feki 274 jambo ambalo lilizua mjadala mkali na bunge kumtaka mbunge huyo atoe ushahidi ndani ya siku 3.

Mwenyekiti Andrew chenge amesema kuwa mbunge huyo alitakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge kanuni ya 63(6) atoe ushahidi kwa ofisi ya bunge na ndani ya siku zote ofisi ya bunge haijapata ushahidi huo.

Kutokana na Mbunge huyo ambaye pia ni mke wa aliyekuwa mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila NCCR Mageuzi kushindwa kutekeleza maamuzi ya bunge mwenyekiti wa bunge amemtaka kufuta kauli yake na mbunge huyo akakaidi ndipo Mwenyekiti akamuamuru atoke nje mara moja na kutohudhuria vikao vya bunge kwa siku zilizobakia 2.

RAIS POMBE MAGUFULI YAMBIDI KUSIMAMA KUWASALIMIA WAKAZI WA MOROGORO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Msamvu mjini Morogoro wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa eneo la Magole mkoani Morogoro
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika eneo la  Msamvu mjini Morogoro kuelekea Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa . sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa . sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa . sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS.
********************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watu wote waliotelekeza Mashamba na Viwanda walivyouziwa na serikali, kuhakikisha wanafufua mashamba na viwanda hivyo mapema iwezekanavyo, kabla serikali haijavinyang'anya na kuwagawia wanaoweza kuviendesha.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake njiani, wakati akisafiri kwa gari kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma.

Amesema mkoa wa Morogoro ulikuwa na viwanda vingi na mashamba mengi makubwa ambayo kama waliouziwa wangeyaendeleza, yangezalisha ajira na kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani na Mazao ya kilimo, lakini waliouziwa mashamba na viwanda hivyo wameamua kutekeleza ama kubadilisha matumizi, huku wengine wakitumia rasilimali hizo kuombea mikopo katika mabenki jambo ambalo serikali yake haitalikubali.

"Kama nilivyowaahidi wakati wa kampeni na leo narudia, wote walioamua kutumia mashamba na viwanda walivyouziwa na serikali kwa ajili ya kuchukulia mikopo kwenye mabenki badala ya kufanya uzalishaji wavifufue haraka, vinginevyo tutawanyang'anya" amesisitiza Rais Magufuli huku akishangiliwa na wananchi waliomsimamisha katika eneo la Msamvu Mjini Morogoro.

Rais Magufuli pia amesimamishwa na kuwasalimu wananchi wa Wami Dakawa, Magole na Dumila ambako pamoja na kuwahakikishia kuwa atatekeleza ahadi yake ya kuwapa mashamba atakayonyang'anya kutoka kwa walioyatelekeza, amewataka kuachana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji na badala yake watatue migogoro hiyo kwa kutumia njia za kisheria.

Aidha, amewataka viongozi wote wa Mkoa hadi vitongoji kushirikiana kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji kabla haijasababisha madhara, na ameonya kuwa migogoro hiyo ikileta madhara itakuwa ni kigezo tosha kuwa viongozi hao wameshindwa kutekeleza wajibu wao na wanapaswa kuachia ngazi.

Pamoja na hayo Rais Magufuli amewahimiza wananchi hao kuchapa kazi kwa juhudi hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha, na pia wahakikishe kuwa watoto wote wanaopaswa kuandikishwa shule wanapelekwa shule, hasa baada ya serikali kuamua kutoa elimu bure ya kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

"Tumeamua kutoa elimu bure na tutatoa elimu bure, na jambo hili limeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa hata shule zilizotarajia kuandikisha wanafunzi 45 zimejikuta zikiandikisha hadi wanafunzi 600 kwa darasa moja" alibainisha Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekagua kipande cha barabara kuu ya Morogoro - Dodoma kilichoharibiwa na maji ya mvua katika eneo la Kibaigwa Mkoani Dodoma, na kujionea kazi za ukarabati zinazofanywa na wakala wa barabara nchini (TANROADS).

Amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuongeza wakandalasi wa kukarabati eneo hilo ili kazi ikamilike haraka badala ya kusubiri mpaka baada ya miezi miwili ilivyopangwa na wizara.


Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 06 Januari, 2016 atashiriki maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zitakazofanyika katika uwanja wa Namfua, Mjini Singida.

KAMPUNI YA UDALALI YAVUNJA NYUMBA SHEKILANGO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kijiko cha Kampuni ya Udalali ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd kikibomoa nyumba za makazi ya watu na biashara zilizojengwa katika eneo la Kampuni ya Dar es Salaam Cold Makers Ltd lililopo Shekilango Sinza jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mwananchi akiangalia mabaki ya nyumba zilizobomolewa katika eneo hilo.

 Kijiko kikibomowa moja ya baa zilizokuwepo eneo hilo jirani na Baa ya Rego iliyopo Sinza jijini Dar.
 Wananchi, wamiliki wa nyumba na mabaa katika eneo wakiwa wamepigwa butwaa
 Mabati yakiondolewa eneo hilo.
 Hapa ni kupiga picha eneo la tukio na huzuni tupu.
 Wananchi wakiwa eneo la tukio.
 Kijiko kikibomoa nyumba ya ghorofa katika eneo hilo.
 Askari Polisi na mgambo wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi.
Kontena likiondolewa katika eneo hilo inadaiwa mmiliki wa kontenta hilo aliuziwa eneo hilo miezi ya hivi karibuni kwa sh.milioni 400. hakika ni hasara kubwa.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Udalali ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd imebomoa nyumba za makazi ya watu na biashara zilizojengwa katika eneo la Kampuni ya Dar es Salaam Cold Makers Ltd lililopo Shekilango Zinza jijini Dar es Salaam.

Uvunjaji wa nyumba hizo uliofanyika Dar es Salaam leo ambao ulisimamiwa na jeshi la polisi na mgambo uliwaanja mdomo wazi na wasijue cha kufanya wamiliki wa nyumba hizo na wafanyabiashara wa nyama choma ya nguruwe ambao wengi wao walishindwa kuondoa mali zao na kujikuta wakiingia hasara kubwa.

Akizungumza na wanahabari eneo la tukio Meneja wa Biashara wa kampuni hiyo ya udalali, Elieza Mbwambo alisema wamebomoa nyumba hilo kwa agizo la mahakama baada ya mteja wao Dar es Salaam Cold Makers kushinda kesi ya msingi iliyofunguliwa na mtu aliyetajwa kwa jina la Ondolo Chacha aliyekuwa akidai eneo hilo ni lake.

Mbwambo alisema kuwa eneo hilo lililokuwa linadaiwa kuwa ni mali ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kampuni hiyo lilikuwa na mgogoro tangu mwaka 1993 kati ya wamiliki halali na wavamizi ambayo ilikuwa ikisikilizwa kwa nyakati tofauti ambapo mmiliki wake halali alikuwa akishinda lakini watu wanaodaiwa wavamizi wakawa wanaweka pingamizi hadi aliposhinda tena hivi karibuni.

"Baada ya mmiliki halali kushinda kesi hiyo mahakama ilitupa kibali cha kuwaondoa wavamizi ambao tumekuja kwaondoa baada ya kuwapa notisi lakini mfungua kesi hakuweza kuwapa notisi hiyo jambo lililoleta changamoto ya kwa watu waliokuwa wakitumia eneo hilo kushindwa kuokoa vitu vyao" alisema Mbwambo.

Mbwambo alisema mteja wao kwa zaidi ya miaka 20 alishindwa kutumia eneo hilo kwa shughuli zake za uzalishaji mali kutokana na mgogoro.

Mmoja wa wafanyabiashara katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la James alisema yeye alipangishwa katika eneo hilo kwa kulipa sh.milioni 20 hivyo ameingia hasara kubwa ya ujenzi wa mabanda na vitu vilivyokuwemo ambapo amepoteza zaidi ya sh.milioni 70.

Mfanyabiashara huyo alisema eneo hilo walikuwa wakipangishwa na watu waliouziwa na mtu aliyedai ni lake na miezi michache iliyopita kuna mzee mmoja aliuziwa sehemu ya barabara na kutoa sh.milioni 400 na kujikuta akiingia katika hasara kubwa.

"Tuta watafuta waliotuuzia maeneo katika eneo hilo na kutupangisha ili waweze kuturudishia fedha zetu" alisema James.

Magazeti ya leo january 06 jumamosi 2016 yapo hapa

Waasi Wa Burundi Wakimbilia Nchini Kushawishi Watanzania Wajiunge Na Vikundi Vya Waasi

$
0
0

BAADHI ya askari waasi wa Burundi, wamebainika kukimbilia nchini na kuanza kushawishi vijana wajisajili ili wajiunge na vikundi vya waasi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema hayo jana alipokuwa akifunga Mkutano wa Pili wa Bunge mjini Dodoma jana na kuwataka wakimbizi na wananchi, kushirikiana na vyombo vya usalama, kutoa taarifa za uhalifu.

“Kutokana na ujio wa wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Burundi, kumejitokeza matukio ya uhalifu wa kutumia silaha za moto ndani na nje ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.“ 

"Aidha, kutokana na upekuzi na ukaguzi kwa wakimbizi unaofanywa kwa pamoja na vyombo vya dola sanjari na taarifa za ki-intelijensia, imebainika kuwepo kwa askari waasi waliokimbia pamoja na raia wa kawaida, ambao wanajaribu kuwashawishi vijana kujisajili ili kujiunga na vikundi vya waasi,” alisema Majaliwa.

Pamoja na changamoto hiyo, ambapo kambi za wakimbizi zilizoko mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora na Tanga zinahifadhi wakimbizi wapatao 218,895 kutoka mataifa ya Burundi (156,377), Congo-DRC (62,176), Somalia (150) na mataifa mchanganyiko (192) ikiwemo Rwanda, Uganda, Sudan Kusini na Ethiopia, hali usalama katika nchi kwa ujumla ni shwari.

Akizungumzia kuimarisha maadili na utendaji serikalini, Majaliwa alisema Serikali imedhamiria kurejesha nidhamu na maadili ya watendaji wa Serikali na watumishi wa umma katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

“Katika kuhakikisha watumishi wa umma na Watanzania wote wanafanya kazi, Mheshimiwa Dk John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuja na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

 “Tafsiri ya falsafa hii ni kuwataka Watanzania wote katika nafasi mbalimbali walizopo, kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na vitendo vya uzembe, urasimu na kutenda kazi kwa mazoea,” alisema.

Alimtaka kila mwananchi, kuwa na nidhamu ya kazi na kuhakikisha anafikia malengo yaliyowekwa na kuwakumbusha watumishi wa umma kuwa, wamepewa dhamana ya kuwahudumia wananchi kwa niaba ya Serikali.

Kwa kuzingatia wajibu huo, amewataka watumishi hao kuhakikisha wanawahudumia wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na kwa taaluma zao na kuhakikisha kuwa wanatatua kero za wananchi.

Waziri Mkuu alisema wanatambua kuwa wapo watumishi wanaotekeleza vyema majukumu yao, lakini pia wapo watumishi ambao hawazingatii maadili ya kazi zao na pia wanafanya kazi kwa uzembe.

“Serikali haitaacha kuchukua hatua za nidhamu kwa watumishi wote wasiozingatia kikamilifu sheria, kanuni na taratibu katika utumishi wa Umma. 

"Aidha, kwa kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Rais, viongozi na watumishi wote wa umma lazima tufanye kazi kwa kuzingatia weledi na kujiamini. Kila mtu anapaswa kujitathmini kama dhamana aliyopewa anaitendea haki,” alisema.

Kuhusu dhana ya kutumbua majipu, Majaliwa alisema Rais ametumia dhana hiyo kusimamia uwajibikaji, hasa kwa wale wenye dalili ya kukosa maadili ya utumishi wa umma.

“Tafsiri ya dhana hii ya “Kutumbua jipu” inalenga katika kuwarejesha watumishi wa umma na walioko serikalini katika mstari mzuri wa utendaji. Nitoe mwito kwa waheshimiwa wabunge wote kama tulivyo na kwa umoja wetu tumuunge mkono Mheshimiwa Rais katika vita hii kubwa ya ‘Kutumbua Majipu’. 

“Tukiwa pamoja na kwa kushirikiana tutaweza kuibadilisha nchi yetu kuwa nchi ya maadili na yenye sifa ya juu katika utendaji wa utumishi wa umma,” alisema.

Kuhusu elimu, Majaliwa alisema tangu Rais Magufuli atoe maelezo ya utekelezaji wa elimu msingi bila malipo, kumekuwa na umuhimu wa kutoa elimu na ufafanuzi zaidi juu ya utekelezaji wa agizo la elimu bila malipo kwa Watanzania kuanzia darasa la awali hadi kidato cha nne katika shule za umma.

Alisema katika mpango huo, Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa mwanafunzi atasoma kuanzia darasa la awali hadi kidato cha nne bila ya wazazi na walezi kulipa ada ya shule, gharama za mitihani na michango mbalimbali.

“Hata hivyo, yapo majukumu ambayo yataendelea kutekelezwa na wazazi na walezi ambayo ni pamoja na kununua sare za shule na michezo, madaftari, kalamu na chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa. 

“Maeneo mengine ni kulipia nauli ya kwenda na kurudi shule, na mahitaji mengine kama kununua godoro, shuka na vifaa vya usafi binafsi. Mzazi au mlezi ana wajibu wa kugharamia matibabu ya mtoto wake,” amesema.

Kuhusu elimu ya juu, amesema hadi kufikia mwishoni mwa Januari 2016, Serikali ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 207.9 kwa wanafunzi 122,786 wa elimu ya juu, wakiwemo wanafunzi wa mwaka wa kwanza 53,850 ambao ni asilimia 98.9 ya wanafunzi 55,254 walioomba mikopo hiyo.

Kuhusu uendeshaji wa Bunge, Majaliwa alisema uzoefu alioupata katika muda mfupi aliokaa pamoja na wabunge Dodoma, amegundua kuwa kuna wabunge mahiri waliobobea katika nyanja mbalimbali.

Alisema amebaini wapo wasomi wa ngazi zote, wazee kwa vijana ambao wana uzoefu na utaalamu mkubwa na kuongeza kuwa wakitumia utaalamu na uwezo mkubwa walionao katika kuijenga nchi, nchi itapiga hatua.

Aliwataka wabunge watangulize uzalendo katika kila jambo wafanyalo kwa manufaa ya Taifa na watu wake, ili nchi ifike mahali ambapo kwa elimu, busara na hekima na kwa kuacha ushabiki wa kisiasa, watazame mbele katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Nitaendelea kufanya kazi niliyotumwa na CCM - JPM

$
0
0
Rais John Magufuli amewataka watendaji wote wa serikali kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo matakwa ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa ndicho kinachoongoza nchi kwa sasa.





Magufuli ametoa agizo hilo leo kwenye sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi zilizofanyika katika uwanja wa Namfua mjini Singida.
Rais Magufuli ambaye alikuwa ni miongoni viongozi wakuu wa serikali waliohudhuria sherehe hizo akiambatana na makamu wake Samiah Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema yeye na serikali yake wamejipanga kutekeleza kikamilifu ilani ya CCM na kwamba hawezi kukiangusha chama hicho.
Akitoa salam zake katika sherehe hizo, Magufuli ametumia muda usiozidi dakika 10 kueleza mambo ambayo tayari serikali yake imeanza kuyafanya na ambayo itaendelea kuyafanya ikiwa ni pamoja na "kutumbua majipu" kwa ustawi wa maisha ya watanzania wote bila kujali vyama vyao.
Ametumia nafasi hiyo kuwaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya pamoja na watendaji wote serikalini kufanya kazi kwa nguvu, uadilifu na uzalendo ili kuwaletea watanzania maendeleo, na kwamba atakayeona hawezi atamuweka pembeni ili wengine wafanye kazi.
“Nawaeleza watendaji wote serikalini kuwa atakayeshindwa kufanya kazi, nitamueleza kwa upole sana maana mimi ni mtu mpole, nitamuambia akae pembeni apishe wengine”
Rais Magufuli pia ameupongeza uongozi wa CCM mkoa wa Singida kwa kuchangia madawati 1000 kwa shule za Singida na kuwaagiza wakuu wote wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanafunzi hawakai chini.
“Mh mwenyekiti inasikitisha sana kuona sisi tunajifungia kwenye maofisi makubwa yenye viyoyozi, na maviti ya kuzunguka lakini tukitoka tu nje tunakuta wanafunzi wamekaa chini kwenye mavumbi, sasa nawaagiza wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa hakikisheni wanafunzi hawakai chini”
Rais Magufuli pia ametumia nafasi hiyo kukishukuru Chama cha Mapinduzi kufanikisha yeye kuwa Rais kwa kuwa bila chama hicho yeye asingekuwa Rais.
“Nataka watanzania wote wajue kuwa bila CCM mimi nisingekuwa Rais wao, kwa hiyo huwezi kunitenganisha mimi na CCM, ndiyo maana leo nimekuja nimevaa kijani yangu hapa”
Pia amesema haoni kama kuna chama kingine chochote kitakachokuja kutawala Tanzania zaidi ya CCM
"Nataka ifikie hatua watanzanie wote wasiwaze wala kuota vyama vingine, tutafanya yale ambayo wao wanataka kuyafanya, ... Hakuna mtawala anayetaka kutawaliwa, tena kwa bahati mbaya atawaliwe na vyama vya hovyohovyo, CCM itaendelea kutawala"

Picha Za Maadhimisho Ya Miaka 39 Ya CCM Kitaifa Mkoani Singida

$
0
0
Msafara wa Mh. Rais John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida tayari kwa kuhudhuria sherehe hizo.

Mh.Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Mh. Dk. Parseko Kone
Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili uwanjani hapo katikati ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono wana CCM na wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akipokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya CCM yanayofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mh. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na Mh. Rais John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mh.Mama Samia Hassan Suluhu, Kushoto ni Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Move waliohudhuria katika maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.

Karibu magazetini leo

$
0
0

Tumekuwekea hapa vichwa vya habari katika magazeti ya leo jumapili ya Th 07 February 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATATU

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WATUNUKIWA TUZO ZA HESHIMA KUTOKA CHUO KIKUU AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY CHA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa akimvika kofia Mwimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel wakati akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano katika mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe.
Hapa Stella Joel akipongezwa na ndugu yake.

Askofu Gwajima Azushiwa Kifo

$
0
0

Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, jana alizushiwa kuwa amefariki dunia.

Taarifa hizo zilizozagaa katika mitandao ya kijamii zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia katika hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilienea  kuanzia ya saa tano asubuhi, zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia kwa shinikizo la damu. 
 
Hata hiyo, taarifa hizo zilikanushwa vikali na mwanasheria wake, wakili wa kujitegemea Peter Kibatala.

Kibatala jana alisema taarifa hizo ni za uzushi ambao haelewi chanzo chake.

“Nimesikitishwa na taarifa hizi na nimepigiwa simu nyingi sana leo kuniuliza juu ya kifo cha Askofu Gwajima na nimebaki nashangaa kwani ni mzima wa afya,” alisema Kibata.

Majira ya jioni jana picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii ziliomwonyesha Askofu Gwajima akiwa mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.

Mawaziri Yona na Mramba Waanza Kutumikia Kifungo cha nje...Wakabidhiwa Vifaa vya Usafi

$
0
0
Mawaziri wa zamani Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona wameripoti leo katika hospitali ya Sinza Palestina na kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kufanya usafi.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliridhia Mawaziri hawa  wastaafu kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA GARI NA 4 WAMEJERUHIWA AKIWEMO MAMA TUNU PINDA MKOANI MOROGORO.

$
0
0
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke wa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda baada ya gari walilokuwa wakisafiria kumgonga mwendesha pikipiki wakati akikatisha barabara katika eneo la Mkundi barabara ya Morogoro Dodoma manispaa ya Morogoro.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Mkundi ikihusisha gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda likitokea Dodoma kwenda jijini Dar-es-Salaam  na pikipiki ambapo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Rajabu Rutengwe anaelezea kuhusiana na ajali hiyo.
Majeruhi wengine wa ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bw Anjelo Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudensi Tembo na kijana wa familia ya Mama Tunu Pinda Bwana Gilbert Sampa.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dr Rita Liamuya amesema hali ya mke wa waziri mkuu mstaafu na majeruhi wengine zinaendelea vizuri na kueleza kuwa  majeruhi hao wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAWATAKA WATU KUWA MAKINI NA MATAPELI WA VIKOBA


Mwigulu awasili eneo la mapigano yaliyoua mbuzi 75

$
0
0


Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Dihinda mkoani Morogoro kufuatia mgogoro mkubwa kuzuka kati ya Wakulima na wafugaji,ambapo inaelezwa kuwa katika tukio hilo mbuzi na kandoo zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana.Waziri Mwigulu Nchema ameahidi kuwa sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati ya drafti),ikiwemo na Kamati ya Ulinzi na Usalama sambamba na wananchi wakishuhudia tukio la mgogoro wa Wakulima na Wafugaji,ambapo takribani mbuzi zaidi ya 70 wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota Likokola (wapili kulia ) wakati alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania katika Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi alioufungua kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha walimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 9, 216. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi baada ya kufungua mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. 

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Jeshi La Polisi Lakamata Majangili 9 Waliotungua Helkopta na Bunduki 29

$
0
0
Siku chache baada ya kutokea tukio la majangili katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, kuitungua ndege (helikopta) iliyokuwa doria na kuaawa kwa rubani wake Rodgers Gower (37),  watu 9 wamekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Katika watuhumiwa hao mmoja ni Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kitengo cha Interejensia, ambaye alitajwa kuwa mhusika Mkuu wa kufanikisha tukio hilo sambamba na kukamatwa mganga wa jadi.

Akitoa taarifa mbele za waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu Lazaro Mambosasa alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kufanya kazu usiku na mchana  kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA.

Kamanda Mambosasa alisema watuhumiwa wote walikamatwa na kukiri kuhusika na tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa uliofanywa na jeshi hilo mara baada ya tukio kutokea chini ya Mkuu wa upelelezi Mkoa Jonathan Shana.

Alisema katika msako huo baadhi ya watuhumiwa walibainika kuwa kiungo kikubwa kufanikisha tukio hilo kwa kutoa mbinu za uharifu, huku wakijihusisha na matukio ya ujangili kwa muda mrefu.

Aliongeza kuwa baadhi yao walibainika kuwa waganga wa jadi, ambapo walikuwa wakitoa dawa kwa majangili za kuosha silaha, ikiwa ni pamoja na  kuosha na kusafisha miili yao ili wasiweze  kukamatwa.

Mambosasa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shija Mjika (38), Njile Gonga (28) Mhazabe, Masasi Mandago (48) pamoja na Dotto Pangali (41) , ambao ndio walihusika kutungua helkopta hiyo.

Wengine ni Iddi Mashaka (49) ambaye Kamanda Mambosasa alimtaja kuwa Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro Kitengo cha Intelijensia na ndiye alikuwa kiungo Mkuu wa tukio hilo.

Aliwataja wengine kuwa ni Mapolu Njige (50) ambaye ni mganga wa jadi aiyekuwa anatumika kutoa dawa za kutokamatwa kwa majangili hao, Mwigulu Kanga (40) , Dotto Huya (45) , Pamoja na Mange Balumu.

Aidha Mambosasa alisema kuwa Mtuhumiwa Dotto Pangali alikamatiwa katika wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga mnamo tarehe 7/02/216 na kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake ambapo alikutwa na bunduki aina ya Riffle yenye namba .7209460 CAR Na.63229.

Mkuu huyo wa polisi alisema Mtuhumiwa huyo alikiri bunduki hiyo kutumika katika tukio la kuuawa kwa rubani huyo, ambapo ilibainika kuwa bunduki hiyo inamilikiwa na Mange Magima ambaye pia amekamatwa.

Alisema msako uliendelea nyumbani kwa Pangali na kufanikiwa kukamatwa kwa bunduki nyingine aina ya Riffle Na3478 CAR 458 ikiwa na risasi 6 ambayo ilibainika kumilikiwa na Nghomango Jilala ambaye mpaka sasa hajakamatwa.

Alieleza kuwa jeshi hilo liliendelea kupata taarifa ambapo mnamo tarehe 29/01/2016 walikamatwa Shija Mjika, Njile Gonga, pamoja na Masasi Mandago wakiwa na meno ya tembo 2 yakiwa na uzito wa Kilo 31 yakiwa yamefichwa chini ya daraja katika kijiji cha Itaba.

Aidha Mambosasa alieleza kuwa baada ya kukamatwa kwa wahusika wote ilibainika kuwa bunduki zilizotumika katika tukio hilo zinamilikiwa kihalali na watu ambao waliomba kuzimiliki kwa ajili kujilinda.

“Mbali na tukio hilo bunduki nyingi wamiliki wake wanawaazimisha majangili kwa ajili ya kutumika kwa uhalifu pamoja na kuua wanyama ndani ya hifadhi…lakini na hao wamiliki wanalipwa pesa baada ya uhalifu kufanyika” ,alisema.


Alisema baada ya kubaini hilo kulifanyika msako mwingine kwa wanaomiliki silaha, ambapo alisema asilimia kubwa wanaishi karibu na hifadhi, na jumla ya bunduki 27 zimekamatwa na mara baada ya uchunguzi wamiliki watarudishiwa.

“Tunajiandaa kupeleka zuio la silaha mahakamani ili kubaini kama wana sifa za umiliki…lakini mbali na hilo sasa kutaanzishwa oparesheni kwa watu wote wanaomiliki silaha hasa maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kuwanyanganya”, alisema.
 
Mkuu huyo wa polisi alisema kuwa upelelezi juu ya tukio hilo umekamilika na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani leo Jumanne ili kujibu tuhuma zinazowakabili, ambapo alioomba mahakama kuharakisha hukumu kwa vile uchunguzi umekamilika.

Kwa upande wake Mhifadhi mkuu wa Serengeti William Mwakilema amelipongeza jeshi la polisi ambapo amesema tukio hilo lilipotokea liliwasikitisha sana kwani hasara ilipatikana kutokana na kutunguliwa kwa helkopta.

Mnamo tarehe 29/01/2016 saa 11:30 jioni katika eneo la Gululu lililopo ndani ya hifadhi ya Maswa kata ya Mwangudo wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, majangili waliipiga risasi ndege (helkopta) 88HFCG iliyokuwa doria na kusababisha kifo cha rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Februari 10

Hii Ndio Idadi Kamili ya Vyama vya Siasa Vilivyogomea Uchaguzi wa Marudio Zanzibar Mpaka Sasa

$
0
0
Vyama tisa vya siasa kati ya 14 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu Zanzibar mwaka jana vimeungana na CUF kutoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, hadi utakapopatikana mwafaka wa kumaliza mgogoro wa kisiasa.

Mratibu wa umoja wa vyama hivyo, Kassim Bakari Ali alisema jana kuwa vyama hivyo vilikutana Unguja na kupitisha maazimio mawili ya kutoshiriki uchaguzi huo.

Vyama hivyo ni UMD, Jahazi Asilia, Chaumma, UPDP, DP, CCK na ACT Wazalendo. Ushiriki wa vyama vya ADC na CCK bado una utata kutokana na wagombea wake kutangaza kushiriki licha ya vyama vyao kuwa na msimamo tofauti, hali iliyosababisha wagombea hao kusimamishwa.

Vyama ambavyo vimetangaza kushiriki marudio hayo hadi sasa ni CCM, Tadea, TLP, Sau na AFP.

Kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita, Zanzibar imeendelea kuwa kwenye mgogoro wa kisiasa kati ya vyama vikubwa vinavyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) baada ya CUF kususia marudio ya uchaguzi baada ya ule wa awali kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Akitaja maazimio ya vyama hivyo, Kassim alisema wamekubaliana kutoshiriki marudio ya uchaguzi huo hadi mgogoro wa CCM na CUF utakapomalizika na wameunda kamati ya wajumbe 18 ya wenyeviti na makatibu wa kila chama ili kuanzisha meza ya kutafuta suluhu ya mvutano uliopo kati ya CCM na CUF.

 “Tutaanza kukaa na viongozi wa vyama hivyo kila upande kujua ni nini hasa hatima ya mvutano huo na tunajikwamuaje,” alisema.

Ali ambaye pia ni mwenyekiti wa Jahazi Asilia alisema mgogoro wa Zanzibar utamalizwa na Wazanzibari wenyewe, hivyo ni vyema viongozi hao wa kisiasa wakajenga uvumilivu katika kutafuta mwafaka.

Alisema tatizo la vyama hivyo siyo kushiriki marudio ya uchaguzi huo tu bali ni kuangalia chanzo na hatima ya mgogoro huo kwa masilahi ya Wazanzibari.

Mwenyekiti wa CCK, Constatine Akitanda aliwaambia waandishi wa habari kuwa uamuzi wa kusimamishwa uanachama kwa mgombea wake wa urais, Ali Khatibu Ali, unakwenda sanjari na kutoshiriki uchaguzi hadi maridhiano ya CUF na CCM yapatikane.

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia AFP, Said Soud Said alisema jana kwamba, chama hicho kimekubali kurudia uchaguzi huo.

 “Lengo la chama chetu ni kushika dola, sasa tusiposhiriki itakuwaje? Kwanza hatuamini kama CUF haijatendewa haki kwa sababu ni kweli kulikuwa na udhaifu, mfano vurugu za kituo cha kupigia kura cha Matrekta Wawi,” alisema.

Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema kama vyama hivyo viliiamini ZEC katika uchaguzi uliopita, vinatakiwa kuiamini kwenye marudio hayo kwa kuwa hakuna mbadala.

“Naomba wakubali kurudia uchaguzi kwani ‘maji yalishamwagika na kuzoleka haiwezekani... Nani aliyekwenda mahakamani kupinga? Wanachoogopa kurudia ni kitu gani kama walishinda?” alihoji Mrema.
Viewing all 2614 articles
Browse latest View live