Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all 2614 articles
Browse latest View live

JENGO LA GHOROFA 16 LINAENDELEA KUBOMOLEWA

$
0
0
 Mafundi ambao hawakuweza kufahamika mara moja kuwa ni wa Kampuni gani wakiwa juu ya jingo la Ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indilagandh jijini Dar es Salaam,wakiendelea na zoezi la ubomoaji wa jingo hilo lililoamuliwa kubomolewa baada ya kuonekana halikidhi viwango vya ujenzi. Ikumbukwe kuwa pembeni mwa jengo hilo liliporomoka jingo la ghorofa lililokuwa likiendelea kujengwa na kusababisha vifo vya watu kadhaa,majeruhi na uhalibifu wa mali mnamo mwaka juzi.
Pamoja na kuwepo kwa tahadahali na kutolewa tangazo kwa wakazi wa maeneo hayo kuhama kwenye nyumba zao zilizo karibu na jingo hilo lakini bado inaonyesha bado kuna wananchi wanaoendelea kuishi karibu na jengo hilo pamoja na kuendelea kwa zoezi hilo la ubomoaji jambo ambalo linaweza kusababisha athari,kama inavyoonekana kwenye jengo hilo la pembeni yake kukiwa kuna nguo zilizoanikwa kuashiria bado kuna watu wanaoishi.
 Ubomoaji unaendelea na maisha yanaendelea jengola pili yake......
Jengo hilo linavyoonekana likiwa katikati ya majengo

Shule zakabiliwa na ukata wa madawati Arusha

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Fidelis Lumato akielezea juu bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mjini kwa mwaka 2015/2016
Wakizungumza wanafunzi hao Miriam Michael na Light Samweli Wamesema kuwa wamekuwa wakikaa chini wawapo darasani hivyo wanahitaji madawati ili waweze kusoma katika mazingira rafiki wawapo darasani.
Kufuatia hali hiyo uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha umekabidhi madawati 100 kwa shule hiyo kati ya madawati 200 yaliyotolewa na halmashauri hiyo kwa ajili ya shule za serikali.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Noah Lembris amesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kusikia kuwa wanafunzi wanakaa chini, pia amewataka wazazi kuuelewa waraka wa serikali wa elimu bure ambao unaainisha maeneo ambayo serikali imetamka bure na yale ambayo wananchi wataendelea kuchangia ikiwemo chakula.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Arusha Fidelis Lumato amesema kuwa halmashauri hiyo imetoa madawati hayo ili kupunguza kadhia ya wanafunzi kukaa chini hivyo amewataka wadau wengine kujitokeza kwani bado shule nyingi zinakabiliwa na uhaba wa madawati, huku akimuagiza mzabuni kukamilisha kazi ya kutengeneza madawati hayo.
Licha ya serikali kutoa waraka wa elimu bure bado kuna maeneo ambayo yanahitaji ushiriki wa wananchi na wadau mbalimbali ili kufanikisha azma ya serikali kutoa elimu bora kwa wananchi.

Huu ndio ushauri wa Mramba kwa serikali

$
0
0

Aliyekuwa  Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba, ameishauri Serikali kuhakikisha inawatumia wafungwa kutumikia jamii badala ya kuwarundika magerezani.

Amesema pamoja na hayo, maisha ya gerezani si salama na si njia pekee ya kumrekebisha mhalifu aliyehukumiwa na mahakama.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja kwa Serikali kuanza kutumia sheria namba 6 ya huduma kwa jamii kuwaangalia wafungwa wenye taaluma kutumika adhabu zao katika fani au taasisi za umma ili kupunguza gharama kuwahudumia watu ambao wanaweza kuisaidia jamii.

Mramba alitoa kauli hiyo jana, wakati yeye na mwenzake aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, walipomaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kutumikia adhabu ya kifungo chao cha nje baada ya wiki iliyopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuridhia kuwa wanastahili kutumikia jamii kwa kipindi cha miezi sita hadi Novemba 5.

Alisema imekuwa ni kawaida jamii kuwa na mtazamo kwamba mtu yeyote anayekutwa na hatia lazima atapelekwa jela ajirekebishe na kuacha tabia aliyonayo jambo ambalo si sahihi.

“Jamii inaamini jela ni sehemu salama na mtu akishikwa na hatia kwa kosa lolote, mahala sahihi ni jela tu, kule anakutana na watu wa kila aina, wenye makosa tofauti, hali ambayo inamfanya ajifunze mambo mengine mapya.

“Unakuta mtu amefanya uhalifu wa kuiba kitu, anafungwa na kupelekwa gerezani, anakutana na majambazi sugu wanaompa mbinu zaidi, sasa akitoka jela anakuja akiwa ameiva, anarudia kwenye matukio akiwa amekamilika,” alisema Mramba.

Alisema kuwapeleka wafungwa katika huduma za kijamii kutasaidia kupunguza gharama kwa Serikali na msongamano ndani ya magereza.

Akizungumzia suala la kuwatumia wafungwa ambao ni wanataaluma, Mramba alisema sheria hiyo ikitumika vizuri italisaidia taifa kwani wapo baadhi ya wafungwa wana taaluma ya udaktari, ualimu, ufundi na uhasibu, ambao wanaweza kutumika katika fani zao kwenye taasisi za umma.

“Kuna maeneo mengine yana uhaba wa wataalamu ambao wengine wapo magerezani wanahudumiwa na Serikali kuanzia chakula, malazi na hata afya zao, hivyo wakiwatumia hao itakuwa faida kwa taifa kwa kuwa watafanya kazi bila malipo,” alisema Mramba.

Alisema suala la kuwatumia wafungwa katika huduma za kijamii si geni kwa nchi zilizoendelea ambako kwa kiasi kikubwa wamesaidia kuinua uchumi wa nchi zao.

Kwa siku ya jana, Mramba na Yona walianza kufanya usafi saa 2 asubuhi kwa kufagia nyuma ya jengo la wazazi katika hospitali hiyo.

Naye Ofisa Huduma za Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Deogratius Shirima, alisema gharama zinazotumika kuwahudumia wafungwa magerezani ni kubwa, hivyo ni vyema wale wanaoguswa na sheria ya huduma za jamii namba 6 ya mwaka 2002 kutumikia kifungo cha nje.

“Sheria hii ni vyema ikatumika kwa wale inaowagusa kwani itapunguza gharama za kuwahudumia magerezani, na pia adhabu wanayopata wafungwa wa nje ni wazi jamii ambayo ndiyo iliyokosewa inaona utekelezaji wake kwa uwazi,” alisema Shirima.

Alisema mataifa mengine ikiwamo nchi ya Kenya wanatumia sheria hiyo ambapo nusu ya wafungwa nchini humo wapo katika huduma za jamii.

Februari 6, mwaka huu mawaziri hao walibadilishiwa adhabu ya jela na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha nje mwishoni mwa wiki iliyopita na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukamilika kwa mchakato wa kufikia hatua hiyo.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, alisema sheria ya huduma kwa jamii namba 6 kifungu namba 3(1) ya mwaka 2002 inasema mtu yeyote anayetiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni miaka mitatu kushuka chini mahakama inaweza kumpa adhabu ya kutumikia jamii.

Mramba na Yona, ambao baada ya rufaa walibakiwa na adhabu ya miaka miwili, walitiwa hatiani kwa kutumia madaraka vibaya ambapo walitakiwa kumaliza kifungo Novemba mwaka huu.

Hata hivyo, hakimu huyo alisema magereza walifikisha barua mahakamani hapo Desemba 5, mwaka jana yenye kumbukumbu namba 151/DAR/3/11/223, wakipendekeza kifungo cha nje kwa mawaziri hao.

Hakimu Mkeha alisema baada ya kupokea barua hiyo, mahakama iliamuru watu wa huduma za jamii kuchunguza kama wanastahili kupewa adhabu hiyo na kwamba walifanya hivyo na kurudisha ripoti kwamba wanastahili.

Alivitaja vigezo vya kupewa adhabu hiyo kuwa ni umri ambapo Mramba na Yona wana miaka 75.

Rais Magufuli akumbana na kero lukuki Muhimbili.

$
0
0
Rais Magufuli ametembelea kwa ghafla wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam, na kujionea hali ya msongamano mkubwa wa wazazi uliosababishwa na uhaba wa vitanda na nafasi finyu katika wodi hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea kwa ghafla wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam, na kujionea hali ya msongamano mkubwa wa wazazi uliosababishwa na uhaba wa vitanda na nafasi finyu katika wodi hiyo.

Rais Magufuli aliyekuwa akitoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokwenda kumuona na kumjulia hali Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubery Bin Ally, amelazimika kwenda katika wodi hiyo baada ya msafara wake kusimamishwa na kundi la akina mama, waliomtaka kwenda katika wodi ya wazazi ili akajionee jinsi wazazi wanavyokabiliwa na kero mbalimbali ikiwemo ya kulala chini kutokana na kukosa vitanda.

Baada ya kujionea mwenyewe kero ya msongamano na kuzungumza baadhi wazazi waliojifungua, Rais Magufuli amewaahidi wazazi hao kuwa atashughulikia kero alizozishuhudia.
"Nimeiona hali halisi mimi mwenyewe, watu wanapata shida, watu wana mateso, na ndio maana nimeamua kuja kwa makusudi, sikuomba ruhusa ili nijionee hali ilivyo, nimejifunza mengi, ninayabeba na nitajua namna ya kuyatatua" Alisema Rais Magufuli.
Kabla ya kutembelea wodi ya wazazi, Dkt. Magufuli amemjulia hali Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubery Ally aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo amempa pole na kumuombea apone haraka.

Pamoja na kupokea pole ya Rais, Mufti wa Tanzania ameongoza dua ya kumuombea heri Rais Magufuli ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake katika kuwahudumia watanzania.
Dua kama hiyo pia imefanywa na wananchi wengine waliokuwa wakimsubiri nje ya majengo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo katika dua hiyo wamemuomba Mwenyezi Mungu kumlinda na kumuongoza katika majukumu yake ya kuiongoza nchi.


"Mwenyezi Mungu mbariki Rais wetu, mpe hekima, busara na upendo katika kazi zake za kuiongoza nchi hii ili watanzania wote wanufaike" ilisema sehemu ya dua hiyo iliyoongozwa na mmoja wa akina Mama.

JAMBO LA KUSHANGAZA NDEGE YATOBOKA SHIMO SOMALIA

$
0
0
Ndege hiyo ililazimika kutua muda mfupi baada ya kupaa

Ndege ya kubeba abiria imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege mjini Mogadishu, Somalia ikiwa na shimo kubwa kwenye kiunzi chake.

Shimo hilo kwenye ndege hiyo lilitoboka muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka Mogadishu, ikiwa futi 10,000 (3,048m) juu angani, jamaa wa mmoja wa abiria ameambia BBC.

Haijabainika ni nini kilichotoboa shimbo hilo.

Maafisa wanasema abiria wawili waliumia.

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Daallo, iliyokuwa ikielekea Djibouti, ilikuwa imebeba watu karibu 60, afisa wa polisi ameambia shirika la habari la Bloomberg.

Baadhi ya ripoti zinasema ndege hiyo ilishika moto muda mfupi baada ya kupaa.

Darren Howe, ambaye mwenzake alikuwa ameabiri ndege hiyo, alipiga picha inayoonyesha shimo hilo muda mfupi baada ya ndege hiyo kutua.

"Hakukutokea mlipuko. Ni kiunzi cha ndege kilichopata hitilafu ndege ikiwa futi 10,000 angani,”


Ndege za shirika la Daallo husafiri mara kwa mara kati ya Dubai, Somalia na Djibouti.

MAGAZETI YOTE YA LEO ,FEB 11

HABARI ZA HIVI PUNDE BASI LA SIMBA MTOTO LAPATA AJALI

$
0
0
Watu kadhaa wamejuruhiwa katika ajili iliyohusisha basi la Simba Mtoto na Lori la mizigo,Korogwe Mkoani Tanga,watu kadhaa waahofiwa kupoteza maisha,Kamanda wa Polisi Mkoani humo athibitisha kutokea kwa ajali hiyo.taarifa za awali waliofariki wafikia kumi mpaka sasa.

Picha na Habari hii kwa hisani ya mdau aliyekuwa kwenye tukio
Tutaendelea kufatilia habari

Habari Picha, Yatokea Sitofahamu katika Pantoni La Kigamboni baada Ya Kugoma Leo Asubuhi

$
0
0
Tutaendelea kufatilia habari

Mkuu wa majeshi wa Korea ya Kaskazini amenyongwa kwa tuhuma za ufisadi

$
0
0
[​IMG]
Mkuu wa majeshi ya Korea Kaskazini kanyongwa kwa tuhuma uhujumu/ufisadi kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Korea ya kusini. Mkuu huyo wa jeshi la Korea Kaskazini hajatajwa kwenye vyombo vya habari vya Korea tangu katikati mwa Januari.

Generali Ri Yong-gil inaripotiwa alinyongwa wiki iliyopita na tukio hilo linatokea wakati dunia ikiinyooshea kidole Korea ya Kaskazini juu ya urushwaji roketi ya masafa marefu Jumapili iliyopita.





English
 North Korea has executed its army chief of staff, Ri Yong Gil, South Korea's Yonhap news agency reported on Wednesday, which, if true, would be the latest in a series of executions, purges and disappearances under its young leader.

The news comes amid heightened tension surrounding isolated North Korea after its Sunday launch of a long-range rocket, which came about a month after it drew international condemnation for conducting its fourth nuclear test.

A source familiar with North Korean affairs also told Reuters that Ri had been executed. The source declined to be identified, given the sensitivity of the matter.

Ri, who was chief of the Korean People's Army (KPA) General Staff, was executed this month for corruption and factional conspiracy, Yonhap and other South Korean media reported.

Yonhap did not identify its sources. The source who told Reuters the news declined to comment on how the information about the execution had been obtained.

South Korea's National Intelligence Service declined to comment and it was not possible to independently verify the report.

The North rarely issues public announcement related to purges or executions of high-level officials.

A rare official confirmation of a high-profile execution came after Jang Song Thaek, leader Kim Jong Un's uncle and the man who was once considered the second most powerful figure in the country, was executed for corruption in 2013.

In May last year, the North executed its defense chief by anti-aircraft gun at a firing range, the South's spy agency said in a report to members of parliament.

The North's military leadership has been in a state of perpetual reshuffle since Kim Jong Un took power after the death of his father in 2011. He has changed his armed forces chief several times since then.

Some other high-ranking officials in the North have been absent from public view for extended periods, fuelling speculation they may have been purged or removed, only to resurface.

CLINTON "APIGWA", TAJIRI DONALD TRUMP ASHINDA KURA ZA MCHUJO

$
0
0
HILARY Clincton, (Pichani juu), ambaye anaomba kuteuliwa na chama chake cha Democrat, kuwania kiti charais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo, ameshindwa kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo na New Hamshire.

Pia Mgombea wa chama cha Republican,  Donald Trump, ameshinda kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo hilo la New Hamshire uliofanyika Jumanne usiku.

Seneta wa Vermont Bernie Sanders, ndiye aliyemshinda Hillary Clinton, huku Trump, tajiri mkubwa kutokaNew York, na ambaye amekuwa akiwashutumu wageni hususan Waislamu kuwa wanaleta “shobo” nchini humo yeye amewabwaga mahasimu wake wa karibu Gavana wa Ohio, John Kasich aliyeshika nafasi ya pili, Gavana wa Florida, Jeb Bush, Seneta wa Texas, Ted Cruz na Seneta wa Florida, Marco Rubio.

Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari wamekuwa kwenye mfumo wa utawala wa nchi hiyo.

Clinton ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mamboya Nje wa Marekani kwenye utawala wa sasa wa Obama, tayari amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kila kura kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic.

Seneta Bernie Sanders (kushoto) na Tajiri Donald Trump.

MWANAMKE WA KIKURYA APAMBNA NA KUWAPOKONYA MAJAMBAZI WATATU BUNDUKI AINA YA SMG.

$
0
0
Mwanamke wa kitongoji cha Buriba, kata ya Sirari, wilayani Tarime, anayejishughulisha na biashara ya kuuza kibanda cha duka, Sophia Manguye (46), amefanikiwa kuwanyang'anya majambazi watatu bunduki moja aina ya SMG yenye risasi 27, baada ya kupambana nao ndani ya kibanda chake cha biashara.

Majambazi hayo kabla ya kunyang'anywa bunduki, yalifanya uporaji katika vibanda kadhaa vya maduka na kufanikiwa kujikusanyia zaidi ya Sh. 180,000, pamoja na vocha za simu za mkononi kutoka maduka matatu tofauti.

Jambazi aliyeporwa bunduki hiyo na Sophia ni Gesanta Matinde (19), mkazi wa kijiji cha Kebeyo, kata ya Mbogi, ikiwa na risasi 27.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Gemini Mushi, jana alisema tukio hilo la uvamizi na unyang'anyi kwa wafanyabiashara lilitokea juzi saa 2:00 usiku katika kitongoji cha Buriba, mji mdogo wa Sirari, baada ya majambazi watatu waliokuwa na silaha aina ya SMG namba UK 5115 kuwavamia wafanyabiashara hao.

“Awali majambazi hao waliingia duka la Zaituni Magasi lililopo jirani na la Sophia na kupora fedha taslimu Sh. 100,000 kabla ya kuingia dukani kwa Sophia na kupora 80,000 za mauzo, lakini hawakuridhika na kiasi hicho, hivyo kuingia ndani na kuanza kutafuta fedha nyingine,” alisema Kamanda Mushi.

Hata hivyo, Kamanda Mushi alisema wakati wakiendelea kupekua kutafuta fedha nyingine, mwanamke huyo alimvamia jambazi aliyekuwa na silaha kisha kumng’ang’ania kwa nguvu, huku akipiga kelele za kuomba msaada hadi walipojitokeza wananchi na polisi waliokuwa karibu kutoa msaada.

Kamanda Mushi alisema baada ya tukio hilo, majambazi wawili walifanikiwa kutoroka, huku mwanamke huyo akipata majeraha usoni na mikononi wakati wa kupambana na majambazi hao.

Alisema Jeshi la Polisi limempongeza mwanamke huyo kwa ujasiri aliouonyesha pamoja na wananchi waliojitokeza na kuongeza nguvu na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na bunduki hiyo ambayo ingeleta madhara makubwa kwa wananchi.

Aliwaomba wananchi kushiriki ulinzi shirikishi kwa kutoa taarifa za uhalifu kwa jeshi hilo mapema kabla ya matukio.

Alisema kwa sasa wanaendelea kumhoji mtuhumiwa na wengine wawili waliotoroka wakitafutwa ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Majangili 9 Wanaotuhumiwa Kutungua Helkopta Wafikishwa Mahakamani

$
0
0

  Njile Gonga (28) Huyu ndiye Jangili anadaiwa kutungua helkopta katika pori la Akiba la Maswa lililopo katika Wilaya ya Meatu Mkoani, ambapo katika tukio hilo rubani wa helkopta hiyo Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo.

Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha Interejensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa kiunganishi Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo.

Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa imehimarsihwa mahakamani pamoja na kituo cha polisi Bariadi.
Watu tisa wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutungua helikopta iliyokuwa ikifanya doria kwenye Pori la Akiba la Maswa wilayani Meatu, Simiyu na na kumuua rubani wake.

Mbali na kutungua chopa na kumuua rubani wake, Rogers Gower, raia wa Uingereza, watu hao pia wameshtakiwa kwa kukutwa na nyara za Serikali, kuuza na kumiliki silaha kinyume cha sheria.


Washtakiwa hao walifikishwa mbele ya Mahakama ya Mkoa wa Simiyu jana wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, huku umati wa wananchi wakifurika na kusababisha hekaheka mahakamani hapo.


Yamiko Mlekano, ambaye ni wakili mwandamizi wa Serikali, alidai kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na kesi tatu; uhujumu uchumi, mauaji na umiliki wa silaha bila ya kibali.


Katika kesi namba mbili ya mauaji, Wakili Yamiko alidai kuwa Shija Mjika (38), Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42) na Moses Mandagu walitungua helikopta hiyo Januari 29 kwenye Hifadhi ya Mwiba iliyoko Kijiji cha Makao wilayani Meatu na kumuua rubani Gower.


Mlekano alidai kuwa katika kesi ya uhujumu, mshtakiwa namba moja Iddy Mashaka (49) anadaiwa kujihusisha na kuratibu tukio la uhujumu uchumi kinyume na sheria.


Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, John Nkwabi, wakili huyo alida kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 6 na Februari Mosi wilayani Meatu kwa kumshauri mshtakiwa namba mbili, Shija Mjika (38) kuua wanyama wasioruhusiwa.

Katika shtaka la pili, watu saba; Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42), Moses Mandagu (48), Dotto Huya (45), Mwigulu Kanga (40), Mapolu Njige (50) na Mange Barumu (47) pia wanashtakiwa kwa kuhujumu uchumi.


Aliieleza mahakama kuwa kati ya Januari 21 na 29 katika wilayani Meatu, washtakiwa walipanga na kuratibu tukio la kuwinda wanyama aina ya tembo bila ya kibali cha Serikali.


Wakili Mlekano alidai kuwa shtaka la tatu la uwindaji wanyama wasioruhusiwa linawakabili mshtakiwa wa pili hadi tisa na wanadaiwa kutenda Januari 26 na 29 kwenye Hifadhi ya Mwiba Kijiji cha Makao wilayani Meatu wa kumuua tembo mwenye thamani ya Sh32,891,100 bila ya kibali.


Katika shtaka la nne, mshtakiwa namba mbili na tisa wanatuhumiwa kumiliki nyara za Serikali kinyume na sheria.


Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari 29 na Februari Mosi wilayani Meatu ambako walikamatwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilo 31 na thamani ya Sh32,891,100.


Katika shtaka namba tano, Mashaka na Mjika wanashtakiwa kwa kuuzaji nyara za Serikali kinyume na sheria na kwamba walitenda kosa hilo kati ya Januari 6 na Februari Mosi wilayani Meatu.


Hakimu Nkwabi alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na aliahirisha hadi Februari 24 zitakapotajwa tena.


Katika kesi ya tatu ambayo ni kukutwa na silaha kinyume cha sheria iliyosomwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya, Mary Mrio, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka matano.


Washtakiwa hao ni Buluma, Mjika, Pangani, Ngunga, Mandagu, Huya na Kanga ambao baadhi yao walikiri kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria akiwamo Njile anayedaiwa kutungua helikopta hiyo.


Washtakiwa hao walikiri mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na bunduki aina ya Riffle 303, wakati Ngunga na Mandagu walikiri shtaka la tatu, nne na tano la kukutwa na silaha na risasi bila ya kibali.


Hata hivyo, Hakimu Mrio alishindwa kutoa hukumu kwa washtakiwa waliokiri kosa kutokana na kutokuwapo kwa vielelezo mahakamani hapo, hivyo kesi hiyo iliahirishwa hadi leo.

Waziri Mwigulu Nchemba afukuza uongozi wote machinjio ya Ukonga

$
0
0

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba afukuza uongozi wote machinjio ya Ukonga, atua usiku wa Manane na kukamata ng'ombe 200 waakichinjwa bila kibali"Ukonga Mazizi kwenye Machinjio usiku wa kuamkia leo ,safari ya kupambana na kuwakamata wanaohujumu kodi/mapato ya serikali.Nimekamata ng'ombe 200 wakiwa wanaingizwa kwenye machinjio bila kibali halali, ni ng'ombe 20 tu kati ya hao 200 ndio wanakibali cha kuchinjwa.
Kwa maana hiyo ushuru wa ng'ombe 180 umekwenda mifukoni mwa watumishi waovu na wenye lengo baya dhidi ya serikali yetu.
Hivyo basi, nimewasimamisha kazi kuanzia mkuu wa mnada wa Pugu ambaye siku si nyingi aliaminiwa na serikali na kupewa jukumu ili aongoze mnada huo,watumishi wote waliotajwa kwenye ubadhilifu huo,wakati huohuo kuanzia usiku huu nimeagiza kwa vyombo vya dola watumishi hao wakamatwe na wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo.
Hatua zingine za kiofisi zinaanza kutekelezwa mapema leo ." Mwigulu Nchemba

MAPITIO YA MAGAZETI YA LEO IJUMAA

AFRIKA KUSINI, BUNGE LAWAKA MOTO, WABUNGE WATOLEWA NJE

$
0
0


Julius Malema na wafuasi wake wakitoka bungeni'
Kumetokea malumbano makali bungeni nchini Afrika Kusini ambapo wanasiasa wa upinzani wamechelewesha hotuba ya rais Jacob Zuma aliyekuwa akilihutubia taifa na kuzua maswali kuhusu utaratibu.
Baadhi ya wanasiasa wanasema rais huyo hakupaswa kuhutubia bunge kutokana na kashfa mbali mbali alizonazo
Ni mvutano huo baada ya spika wa bunge la Afrika Kusini mama Baleka Mbete na wafuasi wa upinzani wengi wao kutoka chama cha Ecoomic Freedom Fighters EFF wakiongozwa na Juliasi Malema ambao walikuwa wanadai kutaka utaratibu na kuvuruga hotuba ya Rais Jacob Zuma..
Hatimaye uvumilivu ukamshsinda spika wa bunge Baleka Mbete na kumuru kiongozi wa EFF Julias Malema kutolewa nje ya ukumbi wa bunge.
Baada ya fujo hizo Rais Jacob Zuma alijaribu kuendelea kuhutubia lakini wabunge wa upinzani walibaki wakarudia tena kumkatiza
Baada fujo hizo baadae angalau kidogo pakawa na utulivu ambapo Rais Zuma aliweza kumalizia hotuba yake na Katika hotuba hiyo Rais Zuma mbali na mambo mengine alisema serikali yake imekuwa akibana matumizi lakini anaona bado hatua zaidi zinahitajika.
"Tumekuwa tukichukua hatua za kubana matumizi ya fedha za umma kwa hekima ikiwa ni pamoja na kubana matumizi yasiyo ya lazima. Lakini bila kuathiri wajibu muhimu wa serikali na kutoa huduma kwa raia. Mwaka 2013 waziri wa fedha alitangaza hatua za kubana matumizi. Matumizi ya ziada na yale yasiyo ya lazima yamepunguzwa lakini bado hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa kubana upotevu wa fedha za umma."
Rais Zuma anakabiliwa na kashfa kadhaa lakini kubwa la hivi karibuni ni hatua ya kutumia fedha za umma kufanya ukarabati wa kasri lake la kifahari la Nkandla. 
BBC

ZIARA YA GHAFLA YA WAZIRI MKUU BANDARINI YAIBUA MAPYA KITENGO CHA MAFUTA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya ghafla kwenye kitengo cha upimaji mafuta bandarini (Oil Flow Metres) na kukuta zimejaa kutu baada ya kutelekezwa kwa miaka zaidi ya mitano. Pia alitembelea mita za kupimia mafuta zinazoendelea kujengwa Kigamboni.

Aidha, Waziri Mkuu amempa saa nne tu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa aandike barua ya kujieleza ni kwa nini aliamua kufunga mita hizo zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na amletee barua hiyo ofisini kwake ifikapo saa 11 leo jioni.

“Nataka unieleze ni kwa nini ulitoa maelekezo ya kufunga mita hizo, na kwa nini jana uliamua kubadili uamuzi huo? Ni kwa nini umeamua kuchukua maamuzi haya baada ya kupokea ujumbe wa simu ya mkononi (sms) wakati mita zimekaa bila kufanya kazi kwa miaka mitano? Ni kwa nini umeamua kufanyia kazi ujumbe wa sms wakati unajua Serikali inafanya kazi kwa maandishi rasmi?” alisema Waziri Mkuu.

“Umesema mlikuwa mnatumia utaratibu wa kupima kwa kijiti. Huu hauna uhakika na huwezi kutegemea taarifa ya mtu mwingine au kuingia kwenye meli ya mtu na kuanza kuchukua vipimo hadi ujiridhishe. Nataka kujua ni kwa nini mlikuwa na utaratibu wa ku-bypass mafuta ili yasipite kwenye mita za kupimia mafuta? Ni kwa nini umetoa amri zianze kutengenezwa jana na siyo mwaka 2012 au 2013?” alihoji Waziri Mkuu.


Waziri Mkuu ambaye aliwasili Kurasini leo saaa 4: 30 asubuhi (Alhamisi, Februari 11, 2016) kwenye kitengo hicho kilichopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty), alikagua mita hizo na kisha kwenda kukagua meli iliyokuwa ikishusha mafuta bila kutumia mita hiyo ya kupima mafuta yanayopokelewa kwa sababu mafundi walikuwa bado wanaendelea na ukarabati.

Akiwa Kurasini, Waziri Mkuu alielezwa na Bibi Chuwa kwamba mita hizo zilianza kufanyiwa ukarabati jana na leo asubuhi moja imekamilika ambayo ni ya kupokelea mafuta ya petroli. Ya dizeli ilikuwa inafunguliwa na mafundi na kukutwa imejaa kutu sababu ya kutotumika kwa muda mrefu.

“Hii ya dizeli imefunguliwa leo na ile ya mafuta ya kula, haijawahi kufanya kazi tangu ilipofungwa mwaka 2011,” alielezwa Waziri Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei.



Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea na kukagua mita mpya za kupimia mafuta ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni 6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).

Vilevile, Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia bainaya Serikali na kampuni ya Oryx Energies.

Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.

“Natoa mwezi mmoja hili bomba liondolewe kwenye mfumo huu na kama yapo mabomba mengine pia yaondolewe,” alisema huku akionyesha karatasi iliyokuwa mfukoni kwake yenye mchoro unaobainisha kuwa kuna bomba jingine la inchi 10 limeungwa kinyemela kwenye bomba kuu.

“Kila mmoja anapaswa aje kuchukua pale kwenye manfold ili tujue nani kachukua nini. Msajili wa Hazina hili ni eneo lako na wewe unamiliki TIPER kwa asilimia 50, hebu simamia hili. Ninyi TPA leteni mapendekezo yenu Serikalini ili tuone tunaweza kudhibiti vipi vitendo kama hivi,” alisema Waziri Mkuu.

Pia alimtaka Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru awasiliane na Mwanasheria Mkuu ili waangalie upya mkataba na umiliki wa matenki hayo uwe chini ya Serikali kwa asilimia 100 ili mafuta yanayoagizwa na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency) yaweze kuhifadhiwa huko.

Mapema, Waziri Mkuu ambaye alifuatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alikagua eneo la manfold ya Mamlaka ya Bandari iliyopo Kigamboni na kukuta ni kampuni nne tu zenye matenki Kigamboni ambazo zinachukua mafuta yao hapo.

Kampuni hizo ni HASS, WORLD OIL, LAKE OIL na MOIL. TIPER haikutaka kufuata mfumo huo licha ya kuwa nafasi ya kufanya hivyo ipo. Kampuni nyingine zenye matenki yake nchi kavu, zinachukulia mafuta kwenye manfold ya Kurasini.

Askari wa Kike wa Usalama Barabarani na Mpenzi wake Waungua moto Hadi Kufa

$
0
0
Askari wa kike wa Usalama Barabarani, Attuganile Mwakibete (37) na mpenzi wake Sunday Mhagama (36), wameteketea kwa moto baada ya nyumba walimokuwa ndani kuungua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema tukio hilo lilitokea Februari 2, mwaka huu saa 7:15 mchana katika kitongoji cha Maporomoko, Kata na Tarafa ya Laela Wilaya ya Kipolisi ya Laela.

Inadaiwa kuwa nyumba hiyo iliyoteketea kwa moto ambayo askari Attuganile alikuwa amepanga vyumba viwili, ni mali Yaiyela Mwamahonje aliyokuwa akiishi na watoto wake wawili wadogo ambao wamenusurika kufa, licha ya kuwemo ndani ya nyumba hiyo wakati wa ajali hiyo.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Mhagama aliyekuwa rafiki wa trafiki huyo wa kike, ni mkazi wa Mbeya ambako mkewe anaishi, na alikuwa na mazoea ya kumtembelea mpenzi wake huyo mara kwa mara.

Inadaiwa askari Attuganile alikuwa ameachana na mumewe wa ndoa. “Vyumba viwili yaani sebule na chumba walimokuwemo Attuganile na Mhagama viliwaka moto baada ya jenereta lililokuwa likifanya kazi likiwa sebuleni humo kulipuka na kuwajeruhi vibaya,” alieleza.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, Attuganile alifariki dunia Februari 8, mwaka huu saa 2:30 asubuhi akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga.

Mhagama alikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya jijini Mbeya ambako alifariki dunia Februari 9, mwaka huu. Kamanda Mwaruanda alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

DJMwanga dot Com Ipo Play Store..Unaweza Download Kwenye Smart Phone yako Hapa

$
0
0
https://goo.gl/Dpx8j4
Download DJMwanga dot Com Android Application CLICK HERE From Play Store

Au Bonyeza hii picha hapa chini

 Official android App for www.djmwanga.com
This application is developed with the following key features:
• Listening Music online with latest collection of tracks
• Download Music for listening offline
• Create your playlists
• Add songs to your favorites list to easily playback
• Listen to Music and do other things with a convenient way with playing background modes, customizeble through the Notification bar (notification).

Download DJMwanga Android Application Click HERE
https://goo.gl/Dpx8j4

CUF Yasema Ipo Tayari Kwa Mazungumzo ila Sio Kurudia Uchaguzi...ZEC Yagoma Kuondoa Picha

$
0
0
Zikiwa  zimebaki siku chache kabla ya kurudiwa kwa uchaguzi Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad amehoji sababu za chama tawala, CCM kuhofia CUF kuongoza visiwa hivyo.

Maalim Seif, ambaye aligombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa Oktoba 25 ambao matokeo yake yalifutwa, pia amesema endapo CCM itasitisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika siku 36 zijazo, CUF watakuwa tayari kufanya mazungumzo lakini si kwa wakati huu ambao maandalizi ya kupiga kura yanaendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, katibu huyo mkuu wa CUF aliitoa hofu CCM kuwa chama chake hakina ajenda ya kulipiza kisasi.

Matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani yalifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha siku ambayo chombo hicho kilitakiwa kumtangaza mshindi, na mwezi uliopita alitangaza Machi 20 kuwa siku ya uchaguzi wa marudio visiwani humo.

Wakati CUF ikipinga vikali kufutwa matokeo na kutangaza tarehe mpya, Serikali imesema kuna nafasi ya kufanya mazungumzo kabla ya uchaguzi wa marudio kwa kuwa kuna muda  mrefu wa kufanya hivyo.

Jecha alitangaza uamuzi huo wakati tayari matokeo ya urais ya majimbo 31 yalishatangazwa, na ya majimbo tisa yaliyosalia yalishahakikiwa, huku washindi wa viti vya uwakilishi na udiwani wakiwa wametangazwa na kupewa vyeti vya ushindi. 

“Sijui kwa nini CCM wanaogopa sisi tukiongoza?” alihoji Maalim Seif kwenye mkutano huo na waandishi akiwa pamoja na aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.

“Wana wasiwasi gani, kwamba CUF ikiongoza kutatokea nini? Sisi hatuna ajenda ya kulipiza kisasi,” alisema.

Katika mkutano huo, Maalim Seif mbaye pia ni katibu mkuu wa chama hicho alisema kama CCM ina wasiwasi na idadi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), haina budi kuondoa shaka kwa kuwa idadi kwa pande zote inakaribiana.

“Hawa wanahisi hawatapata uwakilishi mkubwa, lakini mbona miaka yote tunakuwa na idadi isiyopishana ya wawakilishi?” alihoji.

Kuna Vitisho  Zanzibar 
Katika mkutano huo, Maalim Seif alisema kumekuwapo vitendo vya wananchi kupigwa na vikundi vya watu wasiojulikana. 

Alidai wafanyakazi wa Serikali na taasisi zake wameamrishwa kupeleka vitambulisho vyao vya kazi na vya kura serikalini ili vikahakikiwe.

“Hii si mara ya kwanza wafanyakazi wa Serikali kutakiwa kupeleka vitambulisho, sisi tunajua kuwa wanataka wawatishe kuwa watajua nani kapiga kura na nani hajapiga,” alisema na kusisitiza:

“Hii ni kama kitisho cha kuwalazimisha wakapige kura, zaidi hasa hizo ni dhuluma ambazo wananchi wanafanyiwa.”

Kadhalika Maalim Seif alizungumzia uwapo wa watu wanaovaa soksi usoni na kuwashambulia raia, akisema Serikali haijachukua hatua stahiki kudhibiti hali hiyo.

Alisema watu hao ambao wamepachikwa jina la mazombi, wamevamia maeneo kadhaa kama Baraza la CUF, Jang’ombe na yaleambayo yana wafuasi wa chama hicho kikuu cha upinzani visiwani humo.

“Wanawapiga watu, wanawajeruhi na wanaiba mali, lakini inashangaza sana mambo haya na si Serikali wala polisi iliyochukua hatua,” alisema.

Maalim Seif alisema amezungumza na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuhusu matukio hayo ya uharamia wanaofanyiwa wananchi, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Alisema CCM wanatafuta sababu ili machafuko zaidi yatokee visiwani humo wapate kisingizio.

Aliwataka wafuasi wa CUF kuvumilia hali hiyo ili nchi isiingie kwenye machafuko kama yaliyotokea mwaka 2000, wakati watu zaidi ya 20 waliuawa na wengine kukimbilia Shimoni, Mombasa nchini Kenya ambako waliishi kama wakimbizi.

 Lowassa Azungumza
Kwa upande wake, Lowassa aliwataka viongozi wa ngazi za juu wachukue   hatua kumaliza mgogoro wa Zanzibar.

“Hili tulichukulie kwa umakini sana. Viongozi wafanye vikao vya maridhiano, tunaipenda sana amani tuliyonayo,” alisema.

Lowassa alisema anashangazwa na jinsi CCM wanavyoshindwa kuheshimu makubaliano ya SUK na kukataa kukubali matokeo. 

ZEC  yagoma  kuondoa  picha  ya  Maalim 
Wakati huohuo, habari zinaarifu kuwa Tume  ya  Uchaguzi  Zanzibar( ZEC)  imegoma  kuondoa  picha  za  wagombea  Urais,Udiwani  na Uwakilishi  kutoka  vyama  vilivyotangaza  kutoshiriki  uchaguzi  wa  marudio,ikiwemo  jina  na  picha  Maalim Seif Sharif Hamad.

Hilo  lilifahamika  jana mjini Unguja  baada  ya  kigogo  mmoja  wa  ZEC ambaye  hakuwa  tayari  kutaja  jina  kusema  kuwa  sheria  hazimruhusu  mgombea  yeyote  kujitoa  mwenyewe  kwa  utashi  wake  binafsi.

Kiongozi  huyo  alisema  kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  36  cha  sheria  ya  uchaguzi  namba  11  ya  mwaka  1984,mgombea  hawezi  kujiondoa  kwa  utashi  wake  baada  ya  Tume  kukamilisha  kazi    ya  uteuzi  ambayo  ilifanyika  kabla  ya  Oktoba  25  mwaka  jana.

"Ieleweke  kwamba mgombea  urais  anaweza  kujiondoa  katika  kinyang'anyiro  kwa  kuwasilisha  taarifa  za  maandishi  yeye  mwenyewe  ofisi  za  ZEC  kabla  ya  saa 10  jioni  ya  siku  ya  uteuzi."Alisema  ofisa  huyo  akinukuu  kifungu  cha  katiba.

Alisema  uteuzi  wa  mgombea  mwingine  unaweza  kufanyika  ndani  ya  siku 21  kama  mgombea  hatafariki dunia,lakini  hakuna  ruhusa  ya  kujitoa  kabla  ya  kukamilika  kwa  uchaguzi.

Alisema  ZEC  tayari  imeviandikia  vyama  kuvitaka  vithibitishe  iwapo  wagombea  wao  wangali  hai  au  kuna  waliofariki dunia, na si kutaka  kufahamu  kama  watashiriki  uchaguzi  wa  marudio  au  la.

Mkurugenzi  wa  Mipango  na  Uchaguzi CUF  anena
Mkurugenzi  wa  Mipango  na  Uchaguzi  wa  CUF, Omar Ali Shehe  amesema  ZEC  inasuka  mkakati  wa  siri  wa  kutaka  kuzitumia  picha  na  taarifa  za  wagombea wao  kwa  lengo  la  kuidanganya  dunia  na  jumuiya  za  kimataifa  kwamba  CUF  walishiriki  uchaguzi  huo.

Shehe  amesema  CUF  kilitangaza  mapema  kabisa  kutoshiriki  uchaguzi  wa  marudio,hivyo  dunia  nzima  inaelewa  kabisa  kwamba  CUF  haishiriki  uchaguzi  huo  na  kitendo  cha  kuendelea  kuchapisha  picha  na  taarifa  za  wagombea  wao  katika  karatasi  za  wapiga  kura  si  sahihi.

Mwanamke Aliyemkaba Jambazi Na Kumpora Bunduki Aina Ya SMG Azawadiwa Laki 5 Na Jeshi La Polisi

$
0
0
Mwanamke aliyepambana na jambazi na kufanikiwa kumnyang’anya bunduki aina ya SMG, Sophia Manguye (46), amepewa zawadi ya Sh 500,000 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Gemini Mushy.

Mwanamke huyo ambaye aliomba Serikali kumpa silaha ili kujilinda, alisema kuwa hajaridhika na zawadi hiyo kwa kuwa kama asingemmudu jambazi huyo watu wengi wangepoteza maisha.

Hata hivyo, Mushy alimwomba Manguye kupokea kiasi hicho japokuwa ni kidogo kwa kuwa ni zawadi kutoka ofisi yake.

Tukio hilo lilitokea Februari 9, saa 2.42 usiku, baada ya watu watatu kufika dukani kwake, mmoja wao akiwa na bunduki kisha kumwamuru atoe fedha alizokuwa nazo.

Manguye alisema alichukua Sh80,000 alizokuwa nazo na kumkabidhi jambazi huyo, lakini hakuridhika na kumlazimisha aongeze kiasi kingine.

“Nilipandwa hasira nikanyanyuka wakati jambazi anainama kuangalia kwenye kiboksi cha fedha, nikamkamata kifuani na kung’ang’ania mkanda wa bunduki, akaanza kunivuta kwenda nje, nami nikamvutia ndani, lakini alifanikiwa kunitoa nje akaniangusha chini, lakini sikuachia mkanda wa bunduki,” alisema Manguye na kuongeza:

“Aliposikia wananchi wameanza kupiga yowe akaniachia na kutoa mkanda wa silaha begani, akakimbia na kuniachia bunduki. Wakati huo huo jambazi mwingine alikuwa amekamatwa kwenye duka la Zaituni Magasi, wananchi walipofika wakaanza kumshambulia, wakati huo taarifa ilikuwa tayari imetolewa Kituo cha Polisi Sirari, wakafika kumchukua,” alisema.
Hii ni mara ya pili kwa Manguya kuvamiwa na majambazi wenye silaha, ambapo mwaka 2014 alivamiwa dukani kwake na majambazi waliokuwa na bunduki, lakini alifanikiwa kumpiga kwa kigoda aliyekuwa na bunduki na alianguka chini.

Magasi alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa amevamiwa na majambazi waliokuwa na bunduki, mapanga na nondo.

“Wakati anatoka mvunguni mdogo wangu alimkamata kwa nyuma na kummudu huku akipiga kelele, watu wakafika wakaanza kumpiga hadi akazimia, polisi walipofika wakamwokoa kwani kidogo wamuue,” alisema. 

Viewing all 2614 articles
Browse latest View live