Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all 2614 articles
Browse latest View live

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba na Katibu wa Mkoa Watumbuliwa

$
0
0
CHUMA BLOG
Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi Said - RTX1TYDQ
Rais John Magufuli.
Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo “Kamati Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha.
Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.
Taarifa hiyo  iliyotolewa na Waziri Mkuu, Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo.
Kadhalika Rais Magufuli leo amepokea msaada wa Shilingi Milioni 545milioni kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba, 2016.

RAY C Ashindwa Kuvumilia Anavyompenda Diamond

$
0
0
CHUMA BLOG
Ray C Ashindwa Kuvumilia Anavyompenda Diamond....Aamua kufunguka kama hivi kupitia mtandao wa Instagram:

From Rayc1982 - Seriously Namaste lil bhaia!ngoja niwe mkweli wa nafsi yangu nipate nafuu dude!that Salome of Yours is damn hot!The Powerful couple in this industry kwa sasa bila ubishi wangu ni hawa wachapakazi wawili,bidii katika kila walifanyalo,go getters,wanavyopeana nguvu katika kazi zao,team work team work team makes everything go the it should be and that makes me fall in love with these two hard working souls!everysecond of the day,lil bro u really smart dude,i respect you for that roho ya upendo ulionayo ndio inayozaa matunda bora ya vipaji lukuki vinavyotamba sasa angalia Raymond!Harmonize!!!! Angalia upendo wako unavyozaa matunda bora,Mungu sio kipofu anaona lil bro!Baraka zake kwako hazitaisha dogo you deserve every penny lil bhaia! am a fan all the way keep chasing tht paper,i admire your management team,how serious you guys are in ths industry of ours..I don't call u Simba no more dude! I call you THE GURU OF THE INDUSTRY!haaaaaaaaaa nilitaka kusahau mama weee baiiiiiiiii the wayyyyyyyyyyyyy kale kapicha kangu kalikobandikwa wasafi studios weeee eeeeee weeeee nimejishauaje sasa weweeeee mpaka mama angu nimemringishiaaaaaaaa kaka angu nimemringishiaaaaa mjomba nimemringishiaaaa yani acha weweeee nimefurahi saaaaana sana umenipa moyo mdogo wng ASANTE SAAAAANA ,Thats very kind of you lil bro!STAY BLESSED LIL BHAIA! @diamondplatnumz And I am Your Shabikj Makini without any reasonable doubt......

Rais Magufuli Apokea Msaada Wa Tsh.milioni 545 Kutoka Serikali Ya India Kwa Ajili Ya Waathirika Wa Tetemeko La Ardhi Lililotokea Mkoani Kagera

$
0
0
CHUMA BLOG
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 27 Septemba, 2016 amepokea msaada wa Shilingi Milioni 545 kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba, 2016.

Hundi ya fedha hizo imekabidhiwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na Balozi wa India hapa nchini Mhe. Sandeep Arya na baadaye Rais Magufuli akaikabidhi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Katika barua yake kwa Rais Magufuli iliyosomwa na Balozi Sandeep Arya, Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi amesema Serikali na Wananchi wa India wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kutokea kwa maafa hayo yaliyosababisha vifo vya watu na uharibifu wa mali.

"Tunaziombea amani na uvumilivu familia zote zilizopatwa na madhara na pia tunapenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja na marafiki zetu Serikali ya Tanzania katika kipindi hiki kigumu" amesema Waziri Mkuu Modi.

Kwa Upande wake Rais Magufuli amemshukuru Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi na Serikali yake kwa kutoa mchango huo na kutuma salamu za rambirambi, na amesema Serikali yake imeguswa na moyo wa upendo waliounesha.

"Mhe. Balozi Sandeep Arya naomba unifikishie shukrani zangu za dhati kwa Waziri Mkuu Mhe. Narendra Modi, mwambie kwa niaba ya Serikali yangu tunamshukuru sana kwa kutoa msaada huu muhimu kwa ajili ya Watanzania wenzetu waliopatwa na maafa kule Kagera.

"Mwambie ameonesha moyo wa upendo na ushirikiano kwetu na tumefarijika kwamba marafiki zetu mmeguswa kwa namna ya kipekee na tatizo lililoipata nchi yetu" amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo "Kamati Maafa Kagera" kwa lengo la kujipatia fedha.

Taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.

Hata hivyo Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya "Kamati Maafa Kagera" ambayo imetangazwa na Serikali.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

27 Septemba, 2016
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima. .

Magazeti ya Leo Jumatano ya Septemba 28

$
0
0
CHUMA BLOG

Add caption

Jinsi ya Kumlinda Mumeo Asichepuke

$
0
0
CHUMA BLOG
Wanawake wengi hawajui nafasi ya mume, hivyo kufanya mambo kiholela na kujikuta NDOA inaanza kuleta matatzo.

Jinsi ya kumlinda mumeo:

1. MAPISHI
Unapokua upo jikoni unaandaa chakula, ni lazima ujue kuwa anaekula ni mumeo, hivyo ni vizuri ukatumia ujuzi wako wote kuhakikisha mumeo anakula chakula kizuri. Wanawake wanapika chakula kizuri siku za sikukuu ndo anajitahidi kutumia uelewa wake wote katika kupika ili tu aonekane na majirani.
Au siku ukisikia mumeo anakuja na mgeni rafki yake alafu yamkini ni mtu mwenye cheo fulani ndo unataka upike vizuri.
KWA IYO USITAKE KUPIKA VIZURI ETI KWA SABABU KUNA MGENI AMEKUTEMBELEA BALI IWE NDO TABIA YAKO KWA MUMEO

2. USAFI
Wanawake bado hawajajua kuwa usafi ni kivutio pia kikubwa kwa mwanamume. Na kama tunavyojua kuwa usafi maana yake ni "kila kitu mahali pake"
Sasa wanawake utakuta vijiko vya chakula vipo kwenye kitanda eti kwa sababu tu ana mtoto mdogo. Au nguo za mikojo ya mtoto unaweka chini ya kitanda mpaka zinaanza kutoa harufu. USAFI NI MUHIMU SANA, IWE KWAKO MKE, AU MAZINGIRA YA NYUMBA. NA HAPA SIMAANISHI KUWA MSAFI KWA MAANA YA KUJIPODOA.

3. MANENO MAZURI
Mke ni lazma ujue maneno ya kuongea na mumeo. Maneno mazuri yatamlinda mumeo pale atakapoyasikia kwa wengine. NA HATA KAMA MUMEO HATAONYESHA KUJALI, BADO WEWE MKE UNATAKIWA KUENDELEA KUKAA KWNYE HIYO NAFASI.

Mungu akusaidie ewe mke kuitumia nafasi yako.

Alikiba Atajwa Kuwania Tuzo za MTV EMA 2016..Diamonda Aachwa Mwaka Huu

$
0
0
CHUMA BLOG

Anakuwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki kutajwa kuwania kipengele hicho. Kiba atachuana na wasanii wengine wakiwemo Wizkid na Olamide wa Nigeria na Black Coffee na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini.

Kama ilivyokuwa mwaka jana, mshindi katika hatua ya kwanza ataendelea kwenda kuwania kipengele cha Worldwide Act: Africa/India ambacho mwaka jana alishinda Diamond Platnumz

HUU NDIO UTANI WA MO DEWJI KWA MASHABIKI WA YANGA

$
0
0
CHUMA BLOG

Tukiwa tumebakisha siku chache za watani wajadi, Simba na Yanga kuingia Dimbani, MO Dewji ameshaanzisha tambwe zake kwa klabu ya Yanga.
Mshabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ‘MO’ ameandika ujumbe wa utani kwa mashabiki wa Yanga kwa kusema kwamba “Yanga lazima wakae, “Kandambili mahali pake ni uwani #SimbaNguvuMoja,” aliandika MO.
Follow
Mohammed Dewji MO ✔@moodewji


Yanga lazima wakae, kandambili mahali pake ni uwani.#SimbaNguvuMoja

Tamasha La Vyakula Vya Asili Kufanyika Zanzibar

$
0
0


CHUMA BLOG
food-festival-logo

Dear Partner,
Greetings from Tanzania.
My name is Lilian, Marketing and Communication Executive from Park Hyatt Zanzibar. We believe Travelers need to receive updated live stream information regarding the new trip experience or to hear different stories from the usual place they used to go.
We are delighted to share very exciting news about upcoming the First Stone Town Food Festival which will be held in Zanzibar (Stone Town) during October 13-16, 2016. This event will be the first experience for tourists from different countries to enjoy the best variation of cuisine from most popular restaurants in Stone Town, a unique and rich cultural heritage site in Tanzania recognized by UNESCO.
Kindly find attached Press release with more detail, I appreciate you taking the time to review and if you have any inquiry, feel free to ask any question through my contacts below.
With best regards,
Lilian,
LILIAN KISASA
Marketing and Communications Executive
_______________________
Park Hyatt Zanzibar
P.O. Box 4255, Shangani St.
Stone Town, Zanzibar
T: + 255 24 550 1234
lilian.kisasa@hyatt.com
zanzibar.park.hyatt.com
CONTACT:
Katia Wellving.
Committee Member, Stone Town Food Festival
Tel: +255 774814243
stffestival@gmail.com
Garry Friend
General Manager
Park Hyatt Zanzibar
Tel: +255 24 223 1234
garry.friend@hyatt.com
FOR IMMEDIATE RELEASE
INAUGURAL STONE TOWN FOOD FESTIVAL TO BE HELD IN OCTOBER
ZANZIBAR, TANZANIA (27th September, 2016) – The first Stone Town Food Festival, showcasing the city’s culinary traditions, will be held 13 to 16 October 2016 with hotels and eateries across the city taking part.
Coinciding with World Food Day on 16 October, each hotel and restaurant participating will offer a specially designed menu sold exclusively during the period of the festival and costing 5.000 to 38.000 TSH.

During the event there will be other events includes an open kitchen in the Forodhani Corner where vendors can showcase their food offerings on the 15th October and Cultural events with music performances and art exhibitions at participating restaurants.
Stone Town Food Festival will feature other participants which   are Emerson Spice Tea House restaurant, Emerson on Hurumzi Tea House restaurant, Secret Garden at Emerson Spice, 6 degrees South, Africa house, Jafferji House, Ocean grill, Stone Town Café, Café Foro, Archipelago, Taarab at Doubletree by Hilton, Beyt Al Salam, Park Hyatt Zanzibar, Kisiwa House, Ocean Grill, Monsoon, Golden Tulip Boutique, Golden Tulip Resort, Mashariki Palace Hotel, Tapería Wine & Tapas Bar, La Taverna, House of Kakao, Local Food Bazaar at Zanzibar Airport, Maru Maru, and Zanzibar Serena Hotel.
“The organising committee held its first meeting on 6 September to coordinate all aspects of the festival
and so far 25 establishments have joined in,” said Katia Wellving, one of the organizer for Stone Town Food Festival.

She added that, “Stone Town’s unique and rich cultural heritage has been recognized by UNESCO and
this is a great opportunity to showcase both that and its rich food traditions.”

You can keep up to date with the food festival on its Facebook page: Stone Town Food Festival @stonetownfoodfestival. Any queries may be directed to Katia by email stffestival@gmail.com.

Salam za Mama Diamond Platnumz kwa Wema Sepetu

$
0
0


CHUMA BLOG
September 28, 2016 ni siku ambayo anazaliwa mrembo na mwigizaji wa Filamu, Wema Sepetu ambapo pamoja na watu wengi kumtakia kila la kheri  yupo pia Mama mzazi wa Diamond Platnumz ambaye kwenye akaunti yake ya Instagram amepost picha ya Mama yake Diamond akaisindikizia na maneno haya .. >>>Happy birthday.. Mamy akee @wemasepetu mungu akuongezee umri na akujali kheri akufungulie Mlango wa baraka kwa kila uliombalo.Amin
sw12

Etihad Yaanzisha Huduma Ya Malezi Kwa Watoto Ndani Ya Ndege

$
0
0
CHUMA BLOG
 
etihad-1
Kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za wateja wa Etihad, Turky Alhammadi, Makamu wa rais wa huduma za wateja Bw.Calum Laming na Makamu wa Rais wa Huduma na Mapokezi Sajida Ismail, wakikata keki katika sherehe za uzinduzi wa vifaa vya michezo ya watoto na malezi.
etihad-2
Watoto wakifurahia katika sherehe za uzinduzi wa vifaa vya watoto zilizofanyika Abu Dhabi.
Wakati familia nyingi zikijiandaa kwa ajili ya kwenda mapumzikoni katika nchi mbalimbali, Shirika la Ndege la Etihad  limepiga hatua nyingine katika ubunifu  kwa kuajiri wasaidizi watakaosaidia kulea watoto ndani ya ndege na  kuweka vifaa maalumu vya michezo ya watoto wakati wote watakapokuwa safarini.
Mkusanyiko wa vifaa vya watoto ni huduma mpya katika shirika hilo, vifaa hivyo vitakavyojumuisha vitafunwa na michezo mbalimbali ya watoto vinalenga kuwaburudisha watoto watakapokuwa ndani ya ndege.
Vifaa hivyo, vimezinduliwa katika sherehe ya watoto ilioyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Sanaa na Uvumbuzi cha Shirika hilo mjini Abu Dhabi.
Katika ndege zinazoingia Abu Dhabi, kutakuwa na vifaa vya michezo kwa watoto wenye umri wa miaka mitatu hadi miaka minane. Katika umri huo, vifaa hivyo vitajumuisha vijitabu vidogo, kalamu za rangi, karata na sura za bandia zenye rangi mbalimbali. Ndege zinakazotoka Abu Dhabi zitakuwa na sanduku maalumu la michezo hiyo litakaloongezwa vionjo zaidi.
Watoto wenye miaka 9-13 watakuwa na michezo ya rika lao kama vile; Chemsha bongo na uundaji wa maumbo mbalimbali, pia kutakuwa na makasha maalumu ya Abu Dhabi yenye kalamu rula, peni na vitabu vya nukuu.
Watoto wanaopenda michezo ya kompyuta na teknolojia pia watapata nafasi ya kufurahia filamu mbalimbali, vipindi vya runinga na programu za kisasa katika vifaa vya kidigitali na watakaosafiri umbali mrefu, watahudumiwa na wasaidizi waliopitia mafunzo maalumu. Wasaidizi hao walianza rasmi kuhudumu mwezi Septemba, 2013.
Makamu wa Rais wa  Huduma za Wageni katika Shirika la Etihad, Calum Laming alisema: “Tunaelewa ugumu uliopo wakati  wazazi wanaposafiri umbali mrefu na watoto, hii ndio sababu iliyotufanya kuandaa mazingira rafiki kwa watoto wanapokuwa safarini, pia ni sehemu ya juhudi zetu za kuboresha huduma za anga hasa kwa wanaosafiri kifamilia na watoto wadogo.”
 Vifaa vya watoto vimetengenezwa na kampuni inayotengeneza vifaa vya watoto ya Milk Jnr’s & KidWorks iliyopo Uingereza, ambayo ni mshirika wa kitengo cha Malezi ya Watoto- Etihad na Kitengo cha Maendeleo. Mradi huo pia unahusisha wahusika wa michezo ya watoto kama Simba kundai, Nyuki Zoe, Ngamia Jamool na Boo- Panda. Kampuni ya Milk Jnr’s & KidWorks imechapisha nembo za watoto zenye maumbo mbalimbali yanayowakilisha ardhi ya Abu Dhabi katika sare za wafanyakazi wa Etihad.
Katika kuboresha huduma zake, Etihad itazindua huduma mpya ya chakula kwa watoto  Desemba mwaka huu.
Mkurugenzi wa huduma za wateja Zoe Telfer alisema: “Lengo la mradi huu ni kupata suluhisho la changamoto ya kusafiri na watoto katika ndege zetu. Tunatoa huduma hii kwa safari ndefu na safari zenye umbali mfupi huku tukizingatia sifa za kipekee za Shirika letu.”

Chidi alikuwa apelekwe Ulaya kwenye matibabu – Kalapina

$
0
0
CHUMA BLOG
Rapper Kalapina mmoja kati ya wadau ambao walimsaidia Chidi Benz kumpeleka Sober House amefunguka kwa kusema kuwa kitendo cha Chidi Benz kukatisha muda wa matibabu akiwa Sober House kumemkosesha vitu vingi pamoja na kupelekwa Ulaya kwa ajili ya matibabu.

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumanne hii, Kalapina amesema Chid Benz alikuwa hajapata matibabu sahihi alipotoka ‘sober house’.

“Chid Benz hakumaliza muda wa matibabu alivyotoka ‘sober house’ ndani ya siku 28, kwahiyo mi namuomba afikirie faida alizozipata sober na faida anazozipata sasa hivi akiwa mtaani, nafasi bado ipo kwake kwa sababu tumeplay part kubwa hadi Chid Benz akae sawa, kwa hiyo anatakiwa atusikilize, nafasi ipo kubwa kwa Chid Benz kuweza kujisahihisha”, alisema Kalapina.

Kalapina amesema Chidi Benz alipata wafadhili wa kumpeleka nchi za nje kwa matibabu zaidi, lakini ikashindikana kutokana na kitendo hicho.

“Kulikuwa kuna safari ya yeye na Ray C kupelekwa Ulaya, wafadhili walikuwa wanataka kuwapeleka Ulaya kwa matibabu zaidi, lakini ilitakiwa subira kidogo, ndani ya siku 28 yeye amechoka kukaa sober anataka kukaa mtaani, sasa wafadhili wakishaona uko mtaani tena ku’invest hela yao inakuwa ngumu wanaona bado hujapona”, alisema Kalapina

Mahakama yakana kuitambua kampuni iliyotumiwa na NHC kumtimua Mbowe

$
0
0
CHUMA BLOG
bills
Vitu vya mbowe baada ya kutolewa nje na Kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders kwenye jengo la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC).
Mahakama Kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe kwenye jengo la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC).
Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema, Peter Kibatala wakati wa usikilizwaji wa maombi yaliyofunguliwa na mlalamikaji huyo kupitia kampuni ya Mbowe Hotels Ltd dhidi ya NHC na kampuni hiyo ya udalali.
Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo jana, pamoja na mambo mengine Mbowe aliiomba Mahakama iliamuru NHC na kampuni hiyo wamrejeshe katika jengo hilo pamoja na vifaa na mali zake zinazoshikiliwa na kampuni hiyo.
Wakili Kibatala aliieleza Mahakama kuwa mteja wake aliondolewa katika jengo hilo kinyume na sheria.
Alidai dalali aliyetumiwa na NHC kuziondoa kampuni za Mbowe katika jengo hilo hajasajiliwa na Mahakama kwa kuwa walimwandikia Msajili wa Mahakama barua kujua kama anatambulika, lakini alijibu kuwa haimtambui.
Kutokana na majibu ya msajilihuyo kupitia barua yake ambayo wameiwasilisha mahakamani kama kielelezo, Kibatala alidai sheria na mchakato mzima uliotumika vilikuwa ni batili.
Mawakili wa NHC, Ipilinga Panya na Aloyce Sekule walidai shirika hilo kabla ya kumtimua Mbowe lilimwandikia notisi ya siku 30 iliyokwisha kisha akaongezewa siku 30 zingine kama sheria inavyotaka ambazo ziliisha na kumpa tena siku 14, lakini hakulipa deni.
Wakili wa kampuni ya Foster Auctioneers and General Traders, Aliko Mwamanenge alidai madai ya kuwa mteja wake ni dalali wa Baraza la Usuluhishi na kwamba anayesajiliwa kama dalali ni mtu binafsi na siyo kampuni, hayana ukweli kwani upande wa mlalamikaji ulipoandika barua kuulizia uhalali wake ulipaswa kuuliza jina la mmiliki kampuni hiyo.
Hata hivyo, wakili wa mlalamikaji Kibatala alidai notisi zinazodaiwa kuandikwa na NHC zilipelekwa mahali pasipohusika kwa kampuni ya Free Media badala ya Mbowe Hotels ambayo ina mkataba na NHC. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Sivangilwa Mwangesi anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi Oktoba 18, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa maombi hayo ya mlalamikaji.
Septemba Mosi, wafanyakazi wa kampuni ya udalali ya Foster Auctioneers and General Traders walifika kwenye ofisi za kampuni ya Free Media na kuondoka vifaa mbalimbali vya kazi, zikiwamo kompyuta na viti kwa madai kwamba mmiliki wake, Mbowe anadaiwa na NHC fedha nyingi za kodi ya pango.

Mishikaki Sundays. Kila Jumapili, Na madj wakali. Usikose bonanza kabambe

Kosa Kubwa Alilofanya Jonas Savimbi Hadi Kuuawa

$
0
0
CHUMA BLOG
 savimbi-68
Jonas Savimbi akiwa amezungukwa na walinzi wake enzi za uhai wake. 
Vifo vya viongozi wengi duniani wa kisiasa mara nyingi huchangiwa na makosa yao wenyewe. Hufanya kosa moja kubwa ambalo hugharimu maisha yao, wengi wao wameuawa. Viongozi hawa huwa na imani kubwa kwamba hakuna mtu wa kuwazuia kutekeleza malengo yao na hapa ndipo wengi hutumbukia motoni.
Muammar Gaddafi akiwa Rais wa Libya na wakati huo nchi hiyo ikiwa imewaka moto kwa mapigano makali kati ya waasi na vikosi vya serikali, rafiki yake Rais Jacob Zuma alituma Jet yake hadi Tripoli, Libya kumfuata Gaddafi ambaye aligoma na miezi michache baadaye aliuawa na waasi.
savimbi-66Jonas Savimbi akiwahutubia wafuasi wake.
savimbi-58…Akiwa kwenye moja ya matukio muhimu ya kijeshi ya kikosi chake.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Jonas Savimbi ambaye kitendo chake cha kugomea kurudiwa kwa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo na kuamua kuingia msituni kulipelekea kuuawa kwake. Savimbi alifanya kosa moja kubwa alilazimisha vikosi vyake kuingia msituni kupambana na serikali akiwa bado hajajipanga vyema, ni bora angekubali kurudia uchaguzi dhidi ya Rais Dos Santos huku akijipanga.
Bahati mbaya hakulikumbuka hilo, aliwaza jambo moja tu kuingia msituni kuandaa kikosi chake tayari kuuondoa utawala wa Dos Santos.
Aliingia msituni kipindi ambacho tayari kikosi chake kilikuwa kimeingiliwa na vibaraka ‘spy’ kutoka ndani ya kabila lake, vibaraka hawa waliandaliwa kwa ustadi mkubwa na ndiyo walihusika kutoa siri zote za nini kilikuwa kinaendelea kwenye kikosi cha Savimbi.
TAARIFA YA KUUAWA KWAKE
Februari 22, 2002 vyombo vingi vya habari duniani kote vilitawaliwa na habari kubwa ya kuuawa kwa komando wa vita, mbabe wa wababe, mfalme wa pori na mwanaume aliyeisumbua serikali ya Angola kwa zaidi ya miaka 27 akiongoza vita vya msituni dhidi ya vikosi vya serikali.
savimbi-57…Akiongoza kikao cha juu cha viongozi wa kijeshi wa UNITA msituni.
savimbi-56 
…Akiwa mstari wa mbele kuongoza wanajeshi wake.
savimbi-49Akiwa nje ya ngome kuu ya UNITA, msituni.
savimbi-30 
…Akijadiliana jambo na wasaidizi wake.
HISTORIA YAKE
JonasMalheiroSavimbi, alikuwa mtoto wa pekee kwa baba yake Lote, aliyekuwa mfanyakazi wa reli ya Benguela na mhubiri wa kanisa la Protestanti lililokuwa likifadhiliwa na Wamarekani.
Pamoja na baba yake kuwa muumini wa dini kamwe Jonas hakuwa muumini, tangu utoto wake alikuwa mtukutu.
Wazazi wake wote wawili walikuwa wanatoka kabila la Bieno ambalo baadaye ndiyo likawa msingi wa nguvu kubwa ya Jonas Savimbi kijeshi, kwani aliunda jeshi imara kwa kuwachukua ndugu zake na watu wa kabila lake hali iliyopelekea kuwa na jeshi imara na lenye umoja na mshikamano.
Waliwasiliana kwa kutumia lugha yao na ilikuwa ngumu kwa mtu asiye kabila la Bieno kuingia. Alifanya hivyo lengo likiwa kuwakwepa vibaraka ‘spy’ wa serikali.
Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi alibahatika kwenda kusoma elimu ya sekondari nchini Ureno na akiwa huko alikutana na mwanaharakati Augustino Neto ambaye baadaye alikuja kuwa rais wa kwanza wa Angola.
HARAKATI ZAKE
Mwaka 1966 baada ya kurejea kutoka nchini China ambako alienda kupata mafunzo ya kijeshi alirudi na kuunda UNITA na kuanza kupambana na serikali ya kikoloni sambamba na vyama vingine ambavyo vyote vilikuwa vikipigana kumtoa mreno.
savimbi-7..Akisalimiana na wasaidizi wake.
Hapa ndipo jina la Jonas Savimbi likaanza kusikika kote duniani kutokana na mbinu kubwa za kijeshi alizonazo huku akisapotiwa na wananchi kutoka kabila lake la Bieno.
savimbi-26 
Akitoa maelekezo ya kijeshi kwa wasaidizi wake (hawako pichani)
Huku akipata sapoti kubwa kutoka China na baadaye Marekani, aliongoza vita vikali kwa muda wa miaka zaidi ya 20 huku akiwa ni tishio kubwa kwa Serikali ya Luanda. Kuna muda aliwahi karibia kuipindua serikali ya Rais Dos Santos.
Akiwa na uwezo wa kuzungumza lugha saba kiufasaha zikiwemo tatu za ndani ya bara la Afrika na nne nje ya bara aliweza kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali kuwaomba msaada wa zana za kivita na alifanikiwa kuwa na jeshi imara.
Aliwahi kunusurika kuuawa mara kadhaa likiwemo jaribio la Februari 1990 ambapo aliponea chupuchupu na kukimbilia nchini Marekani na kufanikiwa kuonana na Rais Bush ambaye alimuahidi kumuongezea zana zaidi za kijeshi na baada ya kupona alirejea nchini Angola kuendeleza mapambano.
Baada ya kunusurika kuuawa zaidi ya mara 20 na vikosi vya serikali ya Angola huku taarifa za kuuawa kwake zikiripotiwa zaidi ya mara 15 hatimaye 22 Februari 2002 Jonas Savimbi aliuawa.
Maauaji yake yalitokea kwenye mapigano baina ya vikosi vyake dhidi ya serikali kwenye mto uliopo jimbo la Moxico eneo ambalo alizaliwa. Mapigano hayo ya kushtukiza yalipangwa baada ya vibaraka kutoa siri za mahali alipo Savimbi na baadhi ya wasaidizi wake muhimu, haikuwa kazi rahisi kumuua.
Kwenye shambulio hilo kali kuwahi kufanywa na vikosi vya serikali dhidi ya kikosi cha Savimbi walifanikiwa kumpiga risasi 15 mwilini mwake, alipigwa kichwani, kifuani na sehemu za miguuni na aliweza kumudu na kuendeleza mapambano kwa zaidi ya saa nne kabla ya kuishiwa damu na kuanguka chini na kufariki.
savimbi-5…Akiwa na Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.
Tukio la kuuawa kwake bado limeacha maswali mengi mpaka leo inakuwaje na aliwezaje kuhimili kuendeleza mapambano hata baada ya kupigwa risasi 15 mwilini mwake?
Alizikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao ya Luena na kuhudhuriwa na wapiganaji mbalimbali wa UNITA. Mauaji yake yalimaanisha mwisho wa mapigano ya msituni nchini Angola, Chuma kilikuwa kimeangushwa, wasaidizi wake hawakuwa na mbinu na uwezo kama Savimbi. Baada ya kifo chake serikali kuu ilitangaza ya kwamba hatimaye wameangusha mbuyu wa chuma uliowasumbua miaka mingi.
Wapo wanaoamini mpaka kesho kwamba Jonas Savimbi hakuwa binadamu wa kawaida, walimuona ni binadamu wa pekee mwenye uwezo mkubwa kuliko binadamu wa kawaida. Wenye imani potofu walimfananisha na jini au mzimu unaotembea popote na wakati wowote bila kujali hatari iliyo mbele yake.
savimbi-10Wanafamilia wakiomboleza juu ya kaburi la Jonas Savimbi baada ya kukamilika kwa mazishi yake.
Hadi mauti yake yanamkuta ameacha watoto na wake wengi ambao idadi yake haijawekwa wazi kulingana na sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa akiishi msituni.

PICHA : Uwanja wa Taifa Kwa Juu Unavopendeza Tanzania National Main Stadium


WASANII WAWILI KIZIMBANI KWA KUMDHALILISHA NA KUMUUDHI RAIS MAGUFULI KWENYE MTANDAO WA YOU TUBE

$
0
0
CHUMA BLOG
WAFUASI wawili wa Chadema, akiwemo Mwanamuziki Fulgency Mapunda (32) “Mwana Cotide”, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kumuudhi Rais John Magufuli kupitia mtandao wa ‘YouTube’.




Mapunda na mtayarishaji wa muziki Mnesa Sikabwe (39), walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili wa Serikali, Dereck Mkabatunzi alidai, Agosti mwaka huu katika eneo la Manzese, washitakiwa hao walisambaza taarifa zenye lengo la kumuudhi Rais Magufuli.

Inadaiwa kwa makusudi, washitakiwa hao kupitia mtandao wa YouTube, walisambaza wimbo uliopewa jina la ‘Dikteta Uchwara’ ambao umebeba maudhui ya kumdhalilisha na kumuudhi Rais Magufuli.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa wote walikana kutenda kosa hilo. Wakili Mkabatunzi alidai upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea pia hawana pingamizi na dhamana kwa washitakiwa.

Hakimu Simba alisema, washitakiwa wataachiwa kwa dhamana endapo watakuwa na wadhamini wawili wakuaminika watakasaini hati ya dhamana ya Sh milioni 10. Washitakiwa walitimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana hadi Oktoba 12, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Uingereza Yachangia Bilioni 6 Kwa Ajili Ya Ukarabati Wa Shule Mkoani Kagera

$
0
0
CHUMA BLOG
balozi-sarah-catherine-cooke
Balozi Sarah Catherine Cooke (kulia) akimkabidhi mchango wa fedha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 
Uingereza imetoa mchango wa Shilingi Bilioni 6 kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule zilizopata madhara kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera tarehe 10 Septemba, 2016.
 
Mchango wa fedha hizo umewasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Catherine Cooke, Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya Balozi huyo kuwasilisha hati zake za utambulisho.
 
Balozi Sarah Catherine Cooke amemueleza Rais Magufuli kuwa pamoja na kutoa mchango wa fedha hizo Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Theresa May anatoa pole kwa Serikali ya Tanzania na kwa familia zote zilizopatwa na madhara ya tetemeko hilo na kwamba Uingereza imeona ishirikiane na Tanzania katika kukabiliana na madhara hayo.
 
“Uingereza imeguswa sana na maafa yaliyowakumba wananchi kufuatia tetemeko lililotokea Kagera, tunapenda kuona wananchi wanasaidiwa na wanafunzi wanaendelea na masomo” amesema Balozi Sarah Catherine Cooke.
 
Kwa Upande wake Rais Magufuli amemshukuru Waziri Mkuu wa Uingereza kwa mchango huo ambao utasaidia juhudi za Serikali za kuhakikisha inarejesha miundombinu iliyoharibika zikiwemo shule.
 
“Mhe. Balozi Sarah Catherine Cooke naomba unifikishie shukrani zangu za dhati kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Theresa May na umueleze kuwa kwa niaba ya watanzania hususani waliopatwa na madhara ya tetemeko la ardhi tumeguswa sana na moyo wake wa upendo kwetu” amesema Rais Magufuli.
 
Rais Magufuli na Balozi Sarah Catherine Cooke pia wamezungumzia uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uingereza ambapo Rais Magufuli ametoa wito kwa Balozi huyo kuendelea kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Uingereza kuongeza uwekezaji wao hapa nchini na kwamba Tanzania itaendeleza na kukuza uhusiano huo.
 
“Uingereza ni rafiki na ndugu wa kweli na wa kihistoria kwa Tanzania, tunatambua kuwa nchi yenu ni mdau mkubwa na muhimu wa maendeleo yetu, hivyo tusingependa kupoteza rafiki na ndugu yetu, tuendelee kushirikiana kwa manufaa ya wananchi.
 
“Natambua kuwa Uingereza ina utaalamu mkubwa katika masuala ya gesi hivyo nawakaribisha waje wawekeze katika sekta ya gesi” amesisitiza Rais Magufuli.
 
Aidha, Rais Magufuli amesema Serikali itahakikisha fedha zote zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na madhara ya maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera zinafikishwa kwa walengwa na ameonya kuwa watakaothubutu kuiba fedha hizo watashughulikiwa.
 
Dkt. Magufuli amebainisha kuwa baada ya kutengua uteuzi na kuchukua hatua nyingine dhidi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Amantius Msole na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Bw. Steven Makonda pamoja na kumsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Simbaufoo Swai, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei awachukulie hatua watumishi wa Benki hiyo walioshirikiana na watumishi hao kufanya njama za kuanzisha akaunti nyingine ya benki yenye jina linalofanana na akaunti rasmi ya “Kamati ya Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha”
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
 
28 Septemba, 2016

Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30

Makabuli Ya Kora ''Morogoro'' Yasafiswa Kwa Kuchomwa Moto Je Ni Sahihi....

$
0
0
CHUMA BLOG




                         Na Dustan ,Morogoro.
Baadhi ya majirani wanaoishi jirani na Makabuli hayo baada ya kushuhudia makabuli hayo yakiteketea kwa Moto

Wakizungumza baadhi ya wananchi hao walisema.

" Hii sio sawa  moto umeunguza mpaka alama'kumbukumbu' za maji ya marehemu sasa ndugu wa marehemu watakapo amua kuja kudhuru kwenye makaburi ya wapendwa wao watawatambuaje ili hali alama za majina ya wapendwa wao zimeunguzwa na moto"Alisema mmoja wamashuhuda hao Juma Athuman

Baadhi ya wananchi  walipoulizwa kama wanajua sababu za wahusika kuchoma makaburi hayo  walisema.

" Tunahisi moto huo umechomwa na mwendawazimu ambaye hupenda kukaa kwenye makabuli hayo huku akivuta sigara hivyo kutokana na ukavu wa majani baada ya kutupa kichungi cha siraha kilizaa moto huu  "alisema mmoja wawananchi wa eneo hilo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

lkumbukwe siku za nyuma Uongozi wa Kanisa Katoriki Jimbo la Morogoro kupitia Jumuiya zake za mitaa 'Vigango' walijiwekea zamu za kusafisa makaburi hayo Wakristo na Waislam kila mwezi, ambapo kwa sasa jambo hilo halipo tena jambo lililosababisha makabuli hayo kuzingirwa na msitu mkubwa.

WAFUGAJI KUTIMULIWA KWA NGUVU WILAYA BAGAMOYO NDANI YA SIKU 30 MKOANI PWANI

$
0
0
CHUMA BLOG
 

JAMII ya wafugaji waliovamia kwenye vijiji na vitongoji mbalimbali vinavyounda kata katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wamepewa siku 30 wawe wameshafungasha kila kilicho chao kisha kurejea walikotoka, lengo ikiwa ni kuondoa hali ya tishio la uvunjifu wa amani wilayani hapa.

Hatua hiyo imefikia katika mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Alhaj Majid Mwanga uliokutanisha jamii za wakulima, wafugaji na viongozi mbalimbali kutoka katika ngazi za Vijiji, Vitongoji, Kata, Tarafa na wilaya.


Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa ADEM uliopo mjini hapa na kuhudhuriwa na watu wengi ukiwa na madhumuni ya kupunguza kama si kumaliza kabisa migogoro, inayohusisha mifugo kuingia katika mashamba.


Akizungumza katika mkutano huo, Mwanga alisema wakulima na wafugaji walikuwepo miaka na miaka na kwamba katika vipindi vyote walikuwa wanaheshimiana na hakukuwepo na matukio ya uvunjifu wa amani.


Alisema anashangazwa kuibuka kwa migogoro mingi wilayani hapa na kuwa viongozi wanashindwa kufanya shughuli za kimaendeleo, badala yake wanashughulika na migogoro hiyo.


“Katika sekta ya elimu, baada ya kukamilisha kazi ya madawati katika shule zetu za msingi na sekondari, hivi sasa tuna mikakati ya kuboresha majengo pamoja na mashimo ya vyoo katika baadhi ya shule zetu.


“Lakini cha kusikitisha baada ya sisi viongozi kuelekeza nguvu huko, tumekuwa na kazi ya kusikiliza migogoro ya wafugaji kila kona hali inayokwamisha juhudi za uboreshaji wa sekta hiyo, sasa nimeitisha mkutano huu ili kwa pamoja tuweze kulipatia ufumbuzi,” alisema.


Naye Mohamed Leboi ambaye Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji mkoami Pwani, alisema kila upande uheshimike kwamba unafanya shughuli halali katika nchi na ipewe mahitaji yake kwa kutumia wataalamu wa ardhi na si kwa kutumia mikutano ya ardhi.


Alisema kama itatumika kwa kura hawatapewa nafasi katika maeneo hayo na kuwa maeneo ya vijiji 22 ni kweli yametengwa, lakini haikuheshimika na badala yake sehemu kubwa ipo kwa wawekezaji na matajiri kutoka jijini Dar es Salaam.


Wakichangia mada katika mkutano huo, Said Mnagusi ambaye ni Kaimu Ofisa Tarafa Miono, alisema katika eneo lake kuna matukio mengi ya uvunjifu wa amani yanayosababishwa na jamii ya wafugaji Wamang’ati, ambao wanaingiza mifugo katika mashamba kisha kushambulia wakulima.


Kwa upande wake Katibu wa Ofisi ya Mbunge Jimbo la Chalinze, Idd Swala alishauri iwekwe faini kubwa ili kukomesha vitendo vya baadhi ya jamii ya wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba kwa makusudi.


Akihitimisha mkutano Mwanga alisema kwa kiongozi yeyote ambaye atashindwa kusimamia, au kutekeleza maazimio hayo hatamwonea haya na kwamba serikali iliyopo madarakani ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwatetea wananchi wanyonge ambao ni wa hali ya chini wakiwemo wakulima.
Viewing all 2614 articles
Browse latest View live