Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all 2614 articles
Browse latest View live

iJUE DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAYOTUMIKA SANA NA MASTARI WA BONGO (PUTULUU)

$
0
0
CHUMA BLOG



Naambatanisha picha ya muonekano wa supu ya Aspergers ili ukienda kwenye super market uweze kuitambua. Hii inapatikana kwenye super market na maduka madogo.


 Kwanza poleni na majukumu ya wiki nzima ya kupambana na maisha na wale waliopo ofisini hata leo jumamosi pia niwape pole kwa kupambana na maisha. Nimekuwa nikifuatilia kila nikipata fulsa kusoma hii mada inayohusu NGUVU ZA KIUME.
Labda niingie kidogo kuongeza ninayoyajua,nguvu za kiume ni asili ya mtu kuwa na nguvu hizo na sio madawa kama tunavyodhani. Mtu unaweza kuwa na nguvu za kiume tokea ujana wako mpaka unapofikia uzee wako.Kuna baadhi ya vijana hukosa nguvu za kiume kwa sababu kadhaa na kadhaa. Wengi wa watu hukosa nguvu za kiume kwa kuwa na msongo mkubwa wa mawazo na wengine hukosa nguvu za kiume kwa kufanya kazi nzito.


Watu wenye msongo wa mawazo hukosa nguvu za kiume kwa kuwa kila dakika iendayo kwa MUNGU wao huwa na stress zao ambazo haziepukiki.Na kuna watu huwa wanafanya kazi ngumu sana kutokana na ugumu wa maisha bila kujua kuwa kazi zile zinawasababishia kupoteza nguvu za kiume.Kwa upande wa vijana wengi wale wanaopendelea kuangalia picha au video za (x) hupoteza nguvu zao bila kujielewa.


Kwa wale wanaofanya kazi nzito kama kubeba mizigo mizito au kufanya kazi kwa muda mrefu nao hupoteza nguvu zao bila ya wao kujielewa, hata kwa wafanyakazi wa maofisini kadhalika kwa kukaa kwa muda mrefu kwenye viti vyao hupoteza nguvu za kiume bila wao kujielewa.

VICHOCHEO VYA NGUVU ZA KIUME.
Kuna baadhi ya waungwana wamejaribu kutuwekea baadhi ya vyakula/vinywaji kwa kusema vinaongeza nguvu za kiume...kwa upande wangu siwezi kubisha kwamba haviongezi nguvu za kiume ila mtazamo wangu ni kwamba hivyo ni vichocheo vya hisia za mapenzi na sio 100% kwamba vinaongeza nguvu za kiume.Nguvu za kiume ni asili ya mtu na jinsi unavyoujali mwili wako.nikisema kuujali mwili wako nina maana kwamba unapokula vizuri na kuupa muda wa kutosha mwili wako basi always utajikuta hukosi nguvu za kutosha za starehe ya tendo la ndoa.


Jitahidi sana kuupa mwili mapumziko ya kutosha,fanya mazoezi mara kwa mara kwani mazoezi ni moja ya kigezo cha kufanya mapenzi kwa kutumia nguvu ukiwa huna nguvu za kutosha hutaweza kufanya mapenzi kwa ubora na kiwango cha kuridhisha. Nikisema nguvu sina maana unapofanya mapenzi lazima uwe na mabavu ya kumtimbatimba mwenza wako lahasha... nina maana ukiwa na pumzi ya kutosha utakuwa na uwezo wa kuyafurahia mapenzi kwa kuwa utatumia muda wa kutosha kumfikisha mwenza wako na wewe ukamaliza kwa muda muafaka bila kuvunja rekodi ya dunia.


ASPERGERS SOEP
Kuna kichocheo hiki ambacho sio siri ni kizuri sana endapo utakuwa unakunywa kila siku au mara kwa mara. Ni supu ambayo hata mimi napendelea kuitumia kila weekend hata leo asubuhi nimeitumia,jina la Supu hiyo ni ASPERGERS kwa yoyote mwenye kupenda kuwa na kichocheo cha mwili wake kuufanya uwe na hisia za mapenzi basi ajaribu kunywa supu hiyo.Ila ni vyema kwa wale wana ndoa kama mimi kwani awe na uhakika kwamba usiku au baadae anaingia shambani kulima vinginevyo itakupa tabu sana kwani ina kichocheo kikubwa sana mwilini.


TAHADHALI
Kwa wale wanaopenda kutumia madawa ya kuongeza nguvu za kiume,Binafsi nawashauri sio vyema kabisa kwani madhara yake ni makubwa sana kulinganisha na faida unayoipata kwa muda mfupi. Unaharibu moyo bila kujua na ukiwa sugu wa kutumia madawa hayo kumbuka siku za usoni kupoteza kabisa nguvu hizo za kume na kuukaribisha upofu.

USHAURI WA BURE
Mapenzi ni starehe hivyo kina baba wenzangu tuyafanye kwa sterehe na sio kama unamkomoa huyo mwenza,tujaribu kufanya mapenzi kwa hamu na sio shibe.Maana kuna baadhi ya watu wanatafuta madawa ya kuongeza nguvu ili wakakomoe..mapenzi huwezi katu kumkomoa mwenza ila unapoteza nguvu nyingi kwa kuwa unatumia nguvu nyingi.


Huu ni ushauri wangu na maoni yangu kwenu ila kama kutakuwa na mapungufu niwatake radhi. Ahsanteni sana na nawatakia jumamosi njema.

Rais Kabila Wa Congo-DRC Aweka Jiwe La Msingi Bandarini Jijini Dar Es Salaam .......Kasema Nchi Yake Itaendelea Kutumia Bandari Yetu Kupitisha Mizigo

$
0
0
CHUMA BLOG
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange ameweka jiwe la msingi la jengo la Kituo cha Pamoja cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambalo limejengwa kwa lengo la kuwaweka pamoja wadau wote wanaotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma na kupunguza gharama kwa watumiaji wa bandari hiyo.

Hafla ya uwekaji jiwe la msingi la jengo hilo refu kuliko yote Afrika Mashariki na kati imefanyika leo tarehe 04 Oktoba, 2016 na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza kabla ya kuwekwa jiwe hilo la msingi Rais Magufuli ameishukuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuwa mteja mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam na amesema aliamua jiwe la msingi la jengo hilo liwekwe na Rais wa Kongo kwa kutambua umuhimu wa nchi yake katika biashara ya bandari ya Dar es Salaam na pia undugu na urafiki wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili.

Rais Magufuli amemhakikishia Rais Kabila kuwa kama ambavyo Serikali yake imechukua hatua kadhaa za kurekebisha kasoro zilizokuwepo katika bandari hiyo, itaendelea kujenga mazingira mazuri zaidi kwa wafanyabiashara wa Kongo kutumia bandari hiyo ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya rushwa, kuongeza muda wa kutunza mizigo inayoshushwa kutoka siku 14 hadi siku 30, kuanzisha bandari kavu katika eneo la Ruvu mkoani Pwani na kuinua ari ya wafanyakazi wa bandari kutoa huduma bora.

"Mhe. Rais Kabila bandari yetu ilifikia mahali pa kuandika rekodi ya kupotea kwa meli kwenye taarifa za bandari, kuna wakati hapa zilipotea meli 60, lakini pia mizigo ya watu ilikuwa inapotea na wafanyabiashara walikuwa wanaombwa rushwa.

"Kuna baadhi ya wafanyakazi wa bandari waliifanya hii bandari kama mali yao, walikuwa wanaondoka na fedha za rushwa kwenye buti za magari, naomba nikuhakikishie kuwa haya hayatatokea tena, na yakitokea Mhe. Balozi wa Kongo upo hapa njoo unieleze mimi au mwambie Makamu wa Rais au Waziri Mkuu"amesisitiza Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli pia amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha ujenzi wa jengo hilo la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na kwamba anaamini litasaidia kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Kongo na nchi nyingine zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange amemshukuru Rais Magufuli kwa heshimu kubwa aliyompa yeye na nchi ya Kongo ya kuweka jiwe la msingi la jengo hilo na amesema kutokana na Tanzania kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha huduma za bandari ya Dar es Salaam mizigo ya Kongo itapitia bandari hiyo.

"Mhe. Rais Magufuli bandari hii ipo Dar es Salaam lakini bandari hii ni ya kwetu sote, mashariki ya Kongo inapakana na nchi nne za Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda lakini asilimia 50 ya mizigo inatoka Tanzania hususani katika bandari ya Dar es Salaam.

"Nimefurahi pia kuwa katika juhudi za Tanzania kuboresha bandari pia mnaboresha barabara na bandari ndogo ndogo za ziwa Tanganyika, hili ni jambo muhimu kwa sababu sasa mizigo ya Kongo itasafiri kwa urahisi na wafanyabishara wa Kongo waliokuwa wameacha kutumia bandari ya Dar es Salaam watarudi"amesema Rais Kabila.

Mhe. Joseph Kabila Kabange amesema katika miaka ya 70 na 80 Kongo ilikuwa ikizalisha shaba kiasi cha tani laki 1 lakini hivi sasa inazalisha hadi tani Milioni 1.2 na zote hizi zinategemewa kusafirishwa nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kununua ndege mbili aina ya Bombardier Q400 na ameunga mkono mpango wa kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na Kongo huku akibainisha kuwa nchi yake pia itanunua ndege kwa ajili ya kuimarisha zaidi usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili.

Mapema kabla ya Marais wote wawili kuzungumza, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deodatus Kakoko alisema jengo hilo lina ghorofa 35, urefu wa meta 157, ukubwa wa meta za mraba 65,115 na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika tarehe 31 Desemba, 2016 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 130.

Rais Kabila ambaye aliingia hapa nchini jana tarehe 03 Oktoba, 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu, jioni ya leo atahudhuria dhifa ya kitaifa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa kwa ajili yake na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

04 Oktoba, 2016

PICHA 5: Tingatinga Lilivyofukua mamilioni yaliyokuwa Yamefichwa ardhini Arusha

$
0
0
CHUMA BLOG


eneo la Mianzini mjini Arusha , ambako kuna mradi mkubwa wa upanuzi wa barabara ya kutoka Mianzini Mataa hadi Ilkiding'a unaoendelea.

Picha : KIJANA MOJA AKUSANYA SEREKARI BAADA YA KUTAKA KUJITUPA JUU YA MTI JIONI HII MOROGORO

$
0
0
CHUMA BLOG
Ni kama sehemu yenyewe inavofamika kwa jina la kimarufu Mwembesongo (Mji mpya ) Morogoro

Leo imetokea tukia la kushangaza baada ya mtu moja aliyejulikana kwa jina moja tu la Juma (Wavigogo) kupanda juu ya mti kwa muda nakukataa kushuka juu ya mti huo, hadi Chuma Blog inafika katika eneo ilo kijana huyo alikuwa juu ya mti.

Tukio hilo lilikusanya watu wengi na kila moja alikuwa na maneno yake kwani watu walikuwa na mshangao mkubwa kutokana na watu wengi walikuwa wakimjua huyo kijana. Kila moja alikuwa na maneno yake yakusema kuwa anamajini wengine wakisema kuwa ulevi. Baada ya watu wa usalama kufika na kutaka kumshusha alikuwa akitembea juu ya mti akiama matawi na kuwafanya watu wakitengo cha zima moto,Tanesco na Polisi kushindwa kumshusha nakuwa na wakati mgumu juu yake.



Mpaka Chuma Blog inatoka katika eneo hilo kijana huyo alikuwa ajashuka juu ya mti,tunaendelea kufatilia tukio hilo

Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Octobar 5

Afande Sele adai chama cha ACT-Wazalendo hakieleweki

$
0
0
CHUMA BLOG
Msanii mkongwe wa muziki kutoka mkoani Morogoro, Afande Sele ambaye alikuwa mgombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi uliopita kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka kwa kuonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Rapper huyo amesema viongozi wa chama chake hawaeleweki wapo upande gani kutokana na kubadilisha misimamo yao kila mara.

“Chama changu cha Act-Wazalendo bwana wakati flani hata mimi sikielewi kama ni malaika au shetani. Ni kama kiumbe aitwae mkunga haeleweki ni samaki au nyoka zaidi tumekuwa kama popo hatupo katika kundi la ndege au mnyama…labda hatueleweki au hatujielewi kwa mfano wakati wa kampeni viongozi wetu walijikita kuponda wapinzani wenzetu hasa mzee Lowasa na UKAWA na baada ya uchaguzi viongozi wetu wakampongeza Magufuli kiasi cha kujipendekeza hadi wakampa Ilani ya chama chetu akaitumie akiwa Ikulu. sasa ajabu leo hii tumegeuka tena kwa kiongozi mkuu kila siku anamponda Rais Magufuli na chama chake halafu kiongozi wangu mwingine comrade mchange yeye kila siku anamponda mzee Lowasa na ukawa yake” aliandika kupitia facebook.

Aliongeza “Katika mgogoro wa CUF unaoendelea sasa hivi eti viongozi wote hao wa chama chetu wamejigeuza team Lipumba…sasa sielewi sisi kama wanachama tusimamie wapi….’Nyuma ya pazia’dilidilisha…mchongo=mchongoma…ni bora kuwa Moto au Baridi kuliko kuwa vuguvugu kwani vuguvugu ni ishara ya unafki ambao hata maandiko yanakataza…Kweli itatuweka huru,”

Rais Kabila : Sasa Mizigo yote ya DRC itapitia Bandari ya Dar.

$
0
0
CHUMA BLOG
Rais Joseph Kabange Kabila amekuwa na mazungumzo na Rais Magufuli kabla ya kukutana na waandishi wa habari Ikulu Dsm leo.Katika mambo waliyoongea na kuwashirikisha waandishi wa habari ni ushirikiano wa kibiashara,ulinzi na Usalama pamoja na ujirani mwema.

Rais Kabila anasema baada ya maongezi na Rais JPM amejiridhisha sasa kuwa bandari ya Dsm ni salama na ataanza tena kupitisha mizigo yote ya DRC ktk bandari hii,ambayo kwa kipindi fulani walisitisha na kuanza kutumia kwingine kutokana na kodi,urasimu na upotevu wa mizigo.Katika mazungumzo ya leo,Serikali ya Tz imemuhakikishia Rais Kabila kuwa mizigo yote ya DRC itakuwa na "Grace period" ya siku 14 hadi 30 bandarini.

Pia Rais Kabila anasema wamefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Tanzania kupunguza vituo vya ukaguzi wa mizigo itakayokuwa inatoka bandarini kwenda Congo DR,hali hii ya kupunguza vituo vya ukaguzi itarahisisha wafanyabiashara kufikisha mizigo kwa wakati na kupunguza ghalama za usafirishaji.Rais Kabila pia amemuahidi Rais JPM mara afikapo DRC atahakikisha anafanya mabadiliko makubwa ktk Mamlaka ya Kodi ya DRC ambayo imekuwa ikalalamikiwa na wafanyabiashara wengi kutokana na urasimu na ukiritimba unaokuwa kama kikwazo ktk maendeleo ya biashara.

Rais Kabila pia amezungumzia suala la amani mashariki mwa DRC,na kusema hali si kama inavyolipotiwa na vyomba vya habari vya nje,japo kuna vikundi vichache vya uasi vinavyohatarisha usalama wa raia na mali zao.Amerishukuru JWTZ chini ya Umoja wa Mataifa kuendelea kutunza amani ya DRC.

Naye Rais Magufuli alianza kwa kumwambia Rais Kabila "Kuonesha kuwa Tanzania na DRC tuna uhusiano Mzuri nimemwambia Rais Kabila kuwa Watanzania wengi wanapenda Miziki ya Zaire".
image.jpeg
Rais Magufuli akimpa Rais Kabila zawadi ya kinyago cha #UMOJA mgeni wake Ikulu Dsm

Pia Rais Magufuli ameendelea kumuhakikishia Rais Kabila kumpa ushirikiano wa kiulinzi kwa kuwakutanisha viongozi wa vyombo vya ulinza na usalama vya DRC na Tanzania.Rais Magufuli kamshukuru Kabila kurudisha nia yake ya kutumia bandari ya Dsm kwa kupitisha mizigo yake.

Rais Magufuli ameongelea kuwa wamegusia suala la uchaguzi wa DRC ambapo Kabila amemwambia amelipeleka mbele ili kuhakikisha watu wote wanapiga kura,kwani miaka mitano iliyopita kulikuwa na wapiga kura milioni 35 na sasa ni milioni 45,hivyo wanahitaji muda ili kujumuisha wapiga kura wengi ambao wengi wao ni vijana.

Rais Magufuli amewataka raia wote wa DRC walioko kwenye makambi ya wakimbizi Tz,kurudi DRC kujiandikisha na kupiga kura ili kupata viongozi watakaorudisha amani ya nchi yao na kwafanya wao wasiwe wakimbizi ktk nchi za watu.

Katika ziara hii,Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na DRC wametiliana sahihi mkataba wa kutafuta mafuta ktk eneo la ziwa Tanganyika.Upatakinaji wa mafuta hayo na hatimaye kuchimbwa utaleta maendeleo na kukuza uchumi wa nchi zote mbili.


Baada ya kuongea na waandishi wa Habari,mchana wa saa nane wataweka jiwe la msingi Bandari ya Dsm na baadae kuwa na dhifa ya kitaifa Ikulu-Dsm

SHIRIKA LA NDEGE LA AIR TANZANIA LATANGAZA NAULI ZAKE NI SAWA NA BURE

$
0
0
CHUMA BLOG

img_8543
Baada ya Rais John Pombe Magufuli kuzindua ndege mbili mpya zitakazotumiwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) mwezi uliopita, shirika hilo limeatangaza rasmi maeneo ya safari za ndege hizo ikiwa na pamoja na nauli.
Kupitia ukurasa wa Twitter wa shirika hilo waliandika kuwa nauli ya safari ya ndege kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ni shilingi laki moja na sitini (160,000) ambapo nauli ya kutoka Dar es Salaam hadi Arusha ni bei hiyo hiyo, laki moja na sitini (160,000).

Aidha, shirika limatehadharisha kuwa nauli hizo ni za kwenda tu, na si kwenda na kurudi. Pia wameeleza kuwa nauli za safari kwenye mikoa mingine badi hazijapangwa ila ndio wapo kwenye mchakato

Lissu akosekana Kisutu, aibukia Mwanza

$
0
0
CHUMA BLOG
Simon Mkina, aliyekua Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mawio (Wakwanza),na Tundu Lissu, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wakizungumza na wanahabari baada ya kutoka Mahakamani
Simon Mkina, aliyekua Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mawio (Wakwanza),na Tundu Lissu, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wakizungumza na wanahabari baada ya kutoka Mahakamani
  TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujibu mashitaka ya uchochezi huku mdhamini wake akiieleza mahakama kuwa, yupo jijini Mwanza akisimamia kesi ya Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda katika Mahakama Kuu ya Mwanza, anaandika Faki Sosi.
Lissu ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu na mwansheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo anashitakiwa kwa uchochezi pamoja na washitakiwa wengine ambao ni ni Jabir Idrissa, mwandishi mwandamizi wa Gazeti la MAWIO, Simon Mkina, mhariri wa Gazeti hilo na Ismail Mehboob, meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint.
Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Hemed, ametoa taarifa ya kutofika kwa mdhamana wake mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Ibrahim amedai kwamba Lissu amempatia taarifa kuwa ameshindwa kufika kwa sababu yupo kwenye kesi ya uchaguzi huku Peter Kibatala wakili wa utetezi akiiomba mahakama ipokee taarifa za Lissu na ikubali kuhairisha kesi hiyo.
“Lissu ni wakili wa pekee wa mlalamikiwa Esther Bulaya katika kesi ya uchaguzi,” amesema Kibatala.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 31 mwaka huu.
Katika kesi hiyo Lissu anaunganishwa kama mshitakiwa kufuatia kunukuliwa akitoa maoni yake katika habari iliyochapishwa na gazeti la MAWIO ikiwa na kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar.”

Mfanyabiashara Morogoro Adaiwa Kumtoa Jicho Mpenzi Wake

$
0
0
CHUMA BLOG
Mmiliki wa Hoteli ya Tax Palace ya mkoani Morogoro, Focus Munishi ameingia matatani  baada ya kudaiwa kumpiga msichana anayedai kuwa ni mpenzi wake na kumharibu jicho kiasi cha kusababisha liondolewe.

Kwa sasa msichana huyo, Nanjiva Geofrey amepata ulemavu kutokana na jicho hilo kuondolewa na madaktari baada ya kuharibika kutokana na kipigo hicho.
Kisa:
Nanjiva alisema wakati wa tukio hilo,Uhusiano wao ulikuwa umelegalega na alikumbana na kipigo hicho wakati alipoenda ofisini kwake huyo kumweleza masuala ya masomo ya moja wa watoto wake (Munishi0 watatu ambao mama yao alishafariki.
Siku hiyo, Nilikuta mlango upo wazi. Nilipo ingia tu aliaza kuvua saa yake na kuaza kunipigangumi za uso hadi nikaanguka chini"Alisema Nanjiva baadaye akachukua viatu virefu nilivyokuwa nimevaa na akavitumia kunpigia usoni,kichwani na kusababisha damu zitoke kwa wingi.akaondoka na kufunga mlango kwa nje.
Kama dakika 40 akiwa ameongozana na polisi watatu,Mmoja wa kike na mmoja wao kati ya wawili wengine akiwa na silaha.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro , Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo,wakati mfanyabiashahuyo amekataa kuzungumzia suala hilo akisema liko kwenye vyombo vya sheria. 

Habari hii: Na mwananchi

AUDIO / Roma Ft. Geof Master - IVAN

Bunge Uganda Laimwagia Sifa Tanzania

$
0
0
CHUMA BLOG
BUNGE la Uganda limeipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na Baraza la Maadili lenye nguvu kuliko nchi nyingine Afrika ambalo linashughulikia watumishi wa umma ikiwemo kupambana na vitendo vya rushwa.

Akizungumza katika mkutano kati ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Uganda na Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma jana Dar es Salaam, Kiongozi wa kamati hiyo, Jacob Oboth-Oboth alisema kuwa katika nchi za Afrika, Tanzania pekee ndio lenye baraza imara na kwamba huenda Nigeria ndio inafuata.

Oboth ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Budama Kusini Wilaya ya Tororo, Uganda, alisema sababu ya kuja nchini ni kujifunza namna sekretarieti hiyo inavyofanya kazi kutokana na kupewa meno na sheria iliyopo kwenye Katiba.

"Uganda tuna mpango wa kufanya marekebisho ya sheria iliyotungwa mwaka 2002 kwa lengo la kuwa na watumishi wawajibikaji na utawala bora na kwamba bila ya kujifunza hawawezi kujua uzoefu uliopo na namna ya kuondokana na changamoto hizo," alisema.

Kamishna wa Maadili ya Utumishi wa Umma nchini, Jaji Salome Kaganda alisema wabunge hao wa Uganda waliomba kuja kubadilishana uzoefu na Sekretarieti ya Maadili ya Tanzania ili kuona inavyofanya kazi.

"Tumewashauri kwamba baraza letu ni chanzo cha Katiba ya mwaka 1977 na makatazo yake yamebainishwa katika katiba. Mfano, mbunge akionekana na hatia kinyume na katiba, anapoteza sifa kwamba haruhusiwi kugombea kwa miaka mitano kupigwa faini au kupewa onyo," alisema Jaji Kaganda.

Alifafanua kuwa walichokuja kujifunza wabunge wa Uganda ni kutokana na sheria yao ya maadili kuwepo kwenye vitabu vya sheria pekee wakati kinachotakiwa, sheria itakayotungwa iendane na katiba yenyewe ili kuipa meno.

Saida Karoli " Nilitumiwa, Ukiona Ninapoishi Utasikitika

$
0
0
CHUMA BLOG
Saida Karoli anaogopa kugusa hata jani, akidhanini nyoka anayetaka kumng’ata

Ni kwasababu licha ya kufanya vizuri kimuzi miaka kadhaa iliyopita, hakupata chochote na bado anaishi katika mazingira magumu.“Niliumizwa kuanzia mwanzo, ni vitu vichachenilivyovipata, kama mkibahatika waandishi wahabari wenye makamera na wakija kwanguwatashuti kulingana na nilivyo, wataona mazingira ninayoishi ndipo watanzania watazidikufunguka zaidi,” Kwa sasa Saida Karoli anaishi jijini Mwanza. Hivi karibuni amerejea tena kwenye midomo ya watu baada ya Diamond kurudia wimbo wake Salome.

The East African Tabasamu Mwanangu Awards 2016 Washindi Hawa Hapa

Kizza Besigye Azuiwa Kutoka Nje Ya Nyumba Yake

$
0
0
CHUMA BLOG
kizaKizza Besigye akizungumza na ofisa wa polisi.
KAMPALA: Mwanasiasa wa siku nyingi nchini Uganda, Kizza Besigye leo amezuiliwa na polisi wa Kayihura kutoka nje ya nyumba yake.kizza-1  …Baada ya kushuka garini.
Polisi hao wamemweleza mwanasiasa huyo kwamba wamepewa amri kutoka juu kwamba haruhusiwi kutoka nje ya nyumba yake.
kizza-2…Polisi wakiwa wameweka kizuizi.
Kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa Twitter mwanasiasa huyo ameandika:
“ Happening just now, Kayihura Police officers say their orders are not to allow me out of my home at all- period! Impunity at its highest.”

Magazeti ya Leo Alhamisi ya Oc toba 6

Paul James ‘PJ’ arejea Clouds FM

$
0
0
CHUMA BLOG
Paul James ‘PJ’ amerejea tena Clouds FM akitokea EFM. Anakuwa mtangazaji wa pili wa EFM kuchukuliwa na Clouds katika kipindi cha mwezi mmoja, baada ya Kicheko.

PJ aliyeondoka Clouds mwanzoni mwa mwaka huu akiwa na Gerald Hando, ametambulishwa rasmi Jumatano hii. Anamfuata mtangazaji mwingine aliyehama Clouds akaenda EFM na kisha kurejea tena kwenye kituo hicho, Gardiner G Habash.

Mtangazaji huyo anayesifika kwa uhodari wa kuchambua magazeti, alikuwa na mchango mkubwa wa kukifanya kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM kujipatia umaarufu ndani ya muda mfupi. Kupokonywa kwa PJ EFM kunachocheza zaidi uhasama kati yake na Clouds FM.

VIDEO : Utani wa Mchekeshaji Eric Omondi Kwa Wanaotaka Kuwa Kama Rais Magufuli

$
0
0
CHUMA BLOG
Eric Omondi raia wa Kenya ambaye ni moja kati ya watu waliobarikiwa vipaji vingi ikiwemo uwezo binafsi wa kuchekesha kupitia maneno na mwili wake pia.

Baada ya kufanya ile ya mambo ya kuzingatia kwa wale wanaotaka kuwa kama Diamond Platnumz, Akothee, leo katusogezea nyingine ambayo inamhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli. Eric Omondi katuletea mambo muhimu unapaswa kuyazingatia kama unatamani kuwa kama Rais Magufuli

Unaweza kumtazama Omondi kwenye hii video hapa chini…

Rais Magufuli Aagana na Rais Kabila na kufanya ziara ya kushtukiza uwanja wa ndege

$
0
0
CHUMA BLOG
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange  jana tarehe 05 Oktoba, 2016 amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kurejea nchini kwake.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Kabila aliagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Viongozi wengine walioungana na Rais Magufuli wakati wa kumuaga Rais Kabila ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda na Viongozi wa Dini.

Katika hatua nyingine, mara baada ya kuondoka kwa Rais Kabila, Rais Magufuli alifanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal One ambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.

Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.

Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili  waliotoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.


"Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua"alisisitiza Dkt. Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni  wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kurejea DRC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakipunga mkono kuagana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila (hayupo pichani) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One kuangalia ufanisi wa mashine hizo.

Jinsi ya Kumtuliza Mumeo Asitoke

$
0
0
CHUMA BLOG
Siku hizi wa naume licha ya kukimbia nyumba zao kwa kisingizio cha kazi maajabu weekend hasa Jumamosi utasikia wanaaga nafika hapo njiani naja naenda kununua gazeti.

Kumbe wanaenda kunywa supu na mambo mengine unasubiri wee mpaka alasiri au jioni
Hivyo wanandoa wengi hili limekuwa tatizo mwanaume kiguu na njia asb mchana na njia kumuacha mama na watoto.
Nini kifanyike hasa weekenda Mwanaume ashinde NYUMBANI akikupumzikia??
Zipo njia nyingi mojawapo SUPU YA WEEKEND NA MAZUNGUMZO NA MKAO
Ni kweli wanawake wengi hamjuagi kuwakalisha waume home.

Anza hivi
Siku uko home wewe amka mapema kabla yake anza makeke jikoni…
Mara blenda priiiii… juice… ama milk shake…. hahahaha..Utaona anasogea jikoni..
Wakati anakunywa juice ama milk shake…Anza kukuna nazi…Chambua mnafu…

Hapo jikoni kuna kanyama kanachemka… katia kitunguu tupia viazi 2 na ndizi.Hahaha..
ile harufu ikianza kutoka utasikia anafuata maji jikoni… hahahaha kwenye friji… wala hatumi..
Hahaahha… utasikia nini kiko jikoni?Hahahaa.
Mmiminie supu…
Na ndizi mbili na kiazi kimoja kapilipili mbuzi pembeni..
Muulize kuna chapati…Mpe.. hahahahaha..Akimaliza supu nakuapia atasinzia..
Akishtuka ugali na mnafu na nyama umeiva…Mpe ale..Mshushie na glass ya mtindi…Hahahaha..
analewa full Hata kama kuna mama junior anaambiwa usipige…Hahahahahaha….Baada ya hapo acha apumzike… aoge…Kisha funga ka khanga kako kepesi jilaze pembeni.. woiiiiiiiii..
Mkimaliza muombe pesa ya sokoni…

NAKUAPIA HATA KAMA JANA YAKE ALIKUPA ATAKUPA TENA.
Hahahahaha.. jamani…Hahahahaha… yani kwa raha ya supu… nakuapia utaambiwa hata mama alipiga simu jana… hahahaha.. ama utasikia mamii.. njoo uone njoo… unaitiwa kitu cha kwenye tv.. hahaha.
Hata hujaona mwanzo ila kwa raha yakasupu utaitwa…
Hata kama huna kalio nakuambia utapigwa kibao hata cha mgongo…. hahahahahahahahahaha.

Sasa wewe unaamka chai na mkate kama chuo cha uhazili…
Wali maharage kama jeshi...
Viewing all 2614 articles
Browse latest View live