CHUMA BLOG
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la Polisi
Gari la Polisi likiondoka eneo la tukio na maiti ya Hansi pamoja na Mtuhumiwa
Ofisi ya Hansi
Wananchi wakiangalia ofisi ya Hansi kwahuzuni kubwa.
lnasigitisha sana,Fundi Viatu Hassan Juma Msumi almaarufu Hans ambaye pia ni Mchoraji anadaiwa kuuwawa kwa kupigwa na jiwe kichwani na Jamaa aliyesemekana anamatatizo ya akili’Chizi.’
Tukio hilo baya lilijiri kwenye kibanda cha fundi viatu huyo kilichopo Mtaa wa Mbuyuni Kata ya Kihonda Maghorofani jirani na Stendi ya Mabasi ya Mikoani ya Msamvu Mjini hapa.
Mashuhuda wa tukio hilo Zawadi Haji alisimulia kwa masigitiko “Huyu fundi alisafisha viatu vya mteja wake kisha akavianika juani vikauke ili avipige kiwi ndipo huyu jamaa akapita na kuchukua kiatu kimoja.
“Hansi alianza kumkimbiza ili amnyang’anye walipofika mbele jirani na baa ya Msamvu Terminal Yule jamaa alisimama kisha akaokota jiwe. Hansi alivyoona hivyo naye alianza kukimbia lakini huyo mtuhumiwa alimuwahi na kumpiga jiwe kichwani ndipo Hansi alianguka na kutokwa na damu nyingi kabla ya kukata roho.
Baadhi ya Wananchi wenye hasira walitaka kumuua huyo Mtuhumiwa kwa kulipa kisasi cha kumpiga lakini wengine waliwakataza wasimuue walimfunga kamba na kutoa taarifa polisi. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Tatu Batoni au Mama Mwenda alikiri mauaji hayo kutokea kwenye Mtaa wake. Naye kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Na Dustan