Quantcast
Channel: CHUMA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Katibu Mkuu wa UN, Kofi Annan Azomewa Nchini Myanmar

$
0
0
CHUMA BLOG
Joint Special Envoy Kofi Annan spoke with the media at the United Nations Office at Geneva following the June 30, 2012 Meeting of the Action Group for Syria.Wanaharakati wa Kibudha nchini Myanmar wamemzomea na kumkemea Katibu Mkuu wa Zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan.
Bw Annan alizomewa baada ya kuwasili katika jimbo la Rakhine kuchunguza mzozo wa kidini katika eneo hilo.
Maelfu ya Waislamu wa jamii ya Rohingya wametimuliwa kwenye makao yao baada mashambulizi yaliyotekelezwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni Wabudha, huku wengi wao wakinyimwa uraia na kulazimika kuikimbia nchi hiyo.
Mashambulio hayo yamepelekea baadhi ya watu kutilia shaka kujitolea kwa kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi kutetea haki za kibinadamu.
Bi Suu Kyi alimwita Bw Annan kuchunguza na kupendekeza njia za kupunguza uhasama baina ya jamii zinazoishi eneo hilo.
Bw Annan alihusika kupatanisha pande hasimu wakati wa vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Trending Articles