Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Mtangazaji wa Clouds Tv ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya

CHUMA BLOG
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuteua watangazaji kushika nyadhifa mbalimbali kwani alimteua aliyekuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Leo Septemba 10, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.

Miongoni mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo pia mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku kuanzia jumatatu hadi Ijumaa.

Hudson Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2614

Trending Articles